Mtei akosoa mgombea binafsi kuruhusiwa kuwania urais


nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Likes
90
Points
145
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 90 145
Na Mussa Juma

Posted Jumanne,Juni4 2013 saa 21:3 PM

KWA UFUPI


  • Urais ni nafasi ya juu kabisa katika nchi, lazima Rais ajulikane anatoka chama gani, ana sera gani na kundi gani linamuunga mkono ambako atateua mawaziri wake.

Arusha. Mwanasiasa mkongwe, Edwin Mtei ameelezea kuridhishwa na rasimu ya Katiba Mpya, huku akikosoa kuruhusu mgombea binafsi nafasi ya Urais na kukataliwa kwa serikali za majimbo.

Akizungumza na Mwananchi jana, Mzee Mtei ambaye alikuwa Waziri wa Fedha Serikali ya Awamu ya Kwanza, alisema rasimu hiyo ni nzuri ila ana maoni tofauti kuhusu kuruhusiwa mgombea binafsi kwa nafasi ya Rais na kukataliwa pendekezo la serikali za majimbo.

"Urais ni nafasi ya juu kabisa katika nchi, lazima Rais ajulikane anatoka chama gani, ana sera gani na kundi gani linamuunga mkono ambako atateua mawaziri wake," alisema Mzee Mtei.

Mzee Mtei alisema lazima rais awe anawajibika kwa wananchi kupitia chama chake ambacho kitaunda serikali, lazima sera zake zijulikane na kwamba, nafasi hiyo ikiachwa huru atapatikana rais wa ajabu. "Pia, rasimu imefanya vizuri kupunguza Mamlaka ya Rais, ikiwamo uteuzi wa viongozi mbalimbali kama tume ya uchaguzi, hili ni moja ya mambo tangu enzi za utawala wa kwamza nilikuwa nashauri," alisema Mtei.

Kuhusu serikali ya majimbo, alisema ni vyema kuanza kufikiriwa kwani zitapunguza migogoro kama ulivyo sasa mgogoro wa gesi Mtwara.

"Serikali za majimbo zitaongeza uwajibikaji kwa viongozi, pia usimamizi mzuri wa rasilimali kila eneo kwa manufaa ya eneo husika ingawa ni kweli kuna gharama zake," alisema Mzee Mtei.

Alisema utaratibu wa kupatikana wabunge wa viti maalumu na tume ya uchaguzi na viongozi wengine uliopendekezwa na tume ni mzuri.

Mzee Mtei alisema rasimu hiyo inajaribu kujibu malalamiko mengi ambayo yamekuwa yakitolewa.

 
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Likes
90
Points
145
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 90 145

True That... Tutakuwa ni NCHI PEKEE DUNIANI yenye MGOMBEA BINAFSI na hii ni kwasababu ya VIONGOZI waliobaki NCHINI hawakuwa VIONGOZi walipewa nafasi kuzijaza tuuu kwasababu ya UNYENYEKEVU na SIO UELEWA wa SIASA...

Sasa we ARE GOING TO PAY DEARLY...
 
Kobello

Kobello

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2011
Messages
6,553
Likes
1,606
Points
280
Kobello

Kobello

JF-Expert Member
Joined Feb 20, 2011
6,553 1,606 280
Wrong!! rais anachaguliwa na wananchi na anawajibika kwao tu, na siyo kwa vyama vya siasa. Haya mambo ya kamati kuu za vyama hayana maana.
 
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2008
Messages
13,595
Likes
534
Points
280
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined May 11, 2008
13,595 534 280
Mtei muda wake umeshapita...
 
MNAMBOWA

MNAMBOWA

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2011
Messages
2,013
Likes
81
Points
145
MNAMBOWA

MNAMBOWA

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2011
2,013 81 145
C wao hujifanya ndo watetezi wa democrasia? Anakosoa nn sasa.
 
Mkwawa

Mkwawa

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2011
Messages
1,335
Likes
300
Points
180
Mkwawa

Mkwawa

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2011
1,335 300 180
Katiba ikipita swala la kuwakilisha wananchi litakuwa ni mfuko wako tu. Ingawa bado sijaisoma Rasimu yote sijaona bado matumizi ya fedha za uchaguzi na auditing yake. Kuna matajiri wengi sana duniani wanauwezo kabisa wa kumsimika Raisi na wabunge wa kutosha kwa fedha zao na wakashinda kwa kivuli cha mgombea binafsi.

Lazima tuichambue hii Rasimu vizuri na kuhakikisha demokrasia yenye mipaka ipo. Naunga mkono 100% Mgombea binafsi ila katiba lazima iweke wazi matumizi ya fedha za kampeni na jinsi zinavyoweza kupatikana.
 
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
43,026
Likes
18,242
Points
280
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
43,026 18,242 280
Mtei akae kimya tu. Anajitia aibu na kujiondolea gravita.

Demokrasia ina maana kuongoza nchi kwa mujibu wa matakwa ya watu.

Ukileta ulazima wa wagombea kutoka vyamani, unapunguza nguvu za watu, unaongeza nguvu za vyama. Kuna watu wengine hatutaki vyama. Hatuna vyama.

Kama mtu anachagulika, aweze kuchaguliwa hata kama hana chama. Hii ni haki ya kikatiba. Mwananchi kutopewa nafasi ya kugombea uongozi kwa sababu si mwanachama wa chama fulani ni kinyume na katiba. Ndiyo maana wanazuoni wameona mapungufu haya wakataka kuyaondoa. Huwezi kusema watanzania wote wenye umri na akili za kufikia masharti wana haki ya kugombea uongozi, halafu ukasema watakaogombea uongozi ni wale wenye kupendekezwa na vyama tu. Kama wasio na vyama ndio wanaofaa zaidi je? Kama wananchi hawawataki walio vyamani je?

This vyama business is developing to be one big guild.

Kama mtu hachaguliki, asichagulike hata kama kapendekezwa na chama gani.

Ndiyo demokrasia hiyo.

Kukataa mgombea binafsi ni kukataa demokrasia.

This coming from Mtei, muasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, is a disapointment. Anaonekana anataka kuibana demokrasia ya kweli kwa sababu ana chama kama vile watu wa CCM walivyokuwa chama pekee cha kisiasa walivyotaka kuminya kusiwe na multiparty system.

Its only a matter of time. You cant stop entropy increasing in any closed system.
 
T

tongi

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2012
Messages
452
Likes
14
Points
35
T

tongi

JF-Expert Member
Joined Mar 18, 2012
452 14 35
Hata mgombea binafsi lazima atakuwa na sera yake, na kuwa mgombea binafsi hakuna maana ya kuwa peke yako tu, wagombea binafsi huwa na timu zao zinazojulikana kabisa hasa wakati wa kampeni na humo ndio watapata mawaziri wao, afterall, awe binafsi au toka kwa chama, ni lazima asimamie na kufuata katiba ya nchi, wapi tatizo
 
Tangopori

Tangopori

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2012
Messages
1,635
Likes
329
Points
180
Tangopori

Tangopori

JF-Expert Member
Joined May 11, 2012
1,635 329 180
Mgombea binafsi awepo ila kuwepo na kipengele kinachomtaka aoneshe vyanzo vyake vya fedha za kampeni ili kuepuka mataifa ya magharibi kutuwekea mgombea kwa matakwa yao na wakampa hela za kutosha!
 
Ritz

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Messages
42,249
Likes
4,698
Points
280
Ritz

Ritz

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2011
42,249 4,698 280
Rais siyo wa chama cha siasa Rais ni wa Wananchi. Wananchi ndiyo wana haki ya kuchaguwa ni mtu wa gani ambae wanataka hawaongoze siyo lazima chama.

Mfano mdogo bungeni watu wapo kwa ajili ya vyama siyo Wananchi.

Mtei pumzika tu mzee wetu kwanza ulilalamika hii tume imejaa udini Waislam wengi.

Kuna watu hawataki mambo ya vyama vya siasa.
 
Elungata

Elungata

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Messages
30,632
Likes
13,034
Points
280
Elungata

Elungata

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2011
30,632 13,034 280
C wao hujifanya ndo watetezi wa democrasia? Anakosoa nn sasa.
labda anahofia kura kugawanyika sana na hivyo kuwapunguzia wao uwezekano wa kushinda.
 
CHAMVIGA

CHAMVIGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Messages
7,693
Likes
30
Points
145
CHAMVIGA

CHAMVIGA

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2012
7,693 30 145
Mzee mtei anawasiwasi na kijana zitto manake jamaa akisimama kama yeye baada ya kumbania basi chadema wanaweza ambulia aibu.
 
Buldoza

Buldoza

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2013
Messages
2,304
Likes
94
Points
145
Buldoza

Buldoza

JF-Expert Member
Joined May 2, 2013
2,304 94 145
Rais siyo wa chama cha siasa Rais ni wa Wananchi. Wananchi ndiyo wana haki ya kuchaguwa ni mtu wa gani ambae wanataka hawaongoze siyo lazima chama.

Mfano mdogo bungeni watu wapo kwa ajili ya vyama siyo Wananchi.

Mtei pumzika tu mzee wetu kwanza ulilalamika hii tume imejaa udini Waislam wengi.

Kuna watu hawataki mambo ya vyama vya siasa.
Wakati ule Mtikila ameshinda kesi yake ya kutaka Mgombea binafsi NA serikali kumbania, wewe Ritz NA ndugu zako akina Malaria sugu mlikuwa mstari WA mbele sana kumpinga mgombea binafsi. Leo hii, wamemkubali mmeamua kuwa Bender

a! Duh!
 
H

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Messages
6,946
Likes
818
Points
280
H

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2011
6,946 818 280
Mtei kaa pembeni, hii katiba si yako wala ya CHADEMA. Hayo ndiyo matakwa ya watanzania wengi.
 
Mzito Kabwela

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Messages
17,774
Likes
2,023
Points
280
Age
36
Mzito Kabwela

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2009
17,774 2,023 280
Mtei kaa pembeni, hii katiba si yako wala ya CHADEMA. Hayo ndiyo matakwa ya watanzania wengi.
Unajua maana ya Rasimu? Unajua mzee Mtei anawakilisha maoni ya watu wangapi?
 
D

Deony

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2013
Messages
284
Likes
0
Points
0
D

Deony

JF-Expert Member
Joined May 23, 2013
284 0 0
Katiba ikipita swala la kuwakilisha wananchi litakuwa ni mfuko wako tu. Ingawa bado sijaisoma Rasimu yote sijaona bado matumizi ya fedha za uchaguzi na auditing yake. Kuna matajiri wengi sana duniani wanauwezo kabisa wa kumsimika Raisi na wabunge wa kutosha kwa fedha zao na wakashinda kwa kivuli cha mgombea binafsi.

Lazima tuichambue hii Rasimu vizuri na kuhakikisha demokrasia yenye mipaka ipo. Naunga mkono 100% Mgombea binafsi ila katiba lazima iweke wazi matumizi ya fedha za kampeni na jinsi zinavyoweza kupatikana.
Hii itasaidia kupunguza wagombea ambao hawakubaliki kwa wananchi lkn wanabebwa tu na chama kulinda maslahi ya watu ndani ya chama!Si kweli kwamba matajiri watatumia ugombea binafsi kama rungu,kwani Kuna matajiri wenye uwezo hata wa kuhodhi chama cha siasa!
 
H

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Messages
6,946
Likes
818
Points
280
H

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2011
6,946 818 280
Unajua maana ya Rasimu? Unajua mzee Mtei anawakilisha maoni ya watu wangapi?
Aende zake huko, kwanza maoni ya watu watu kama yeye hayana tija kwa taifa, au humjui kuwa alikuwa mnafiki kwa baba yetu wa Taifa?

Hayo maoni yake amelenga kuiokoa CHADEMA, kwani baada ya upuuzi wa majimbo kutoingizwa kwenye rasimu, hajaridhika na mgombea binafsi ili aendelee kumkandamiza Zitto, yeye na genge lake.
 

Forum statistics

Threads 1,273,821
Members 490,485
Posts 30,493,055