Mtei akosoa mgombea binafsi kuruhusiwa kuwania urais

Tafadhali sana Angalia Candidate Ralf Nadar na pia Candidate Ross Perot... Wote nilikuwambia walikuwa na VYAMA

YearPresidential Candidates
(winner in bold)
Political Parties*Electoral Votes**Popular VotesVP Candidates
(winner in bold)
2008Barack Obama (44th Pres.)
John McCain
Ralph Nader
Bob Barr
Chuck Baldwin
Cynthia McKinney
Democratic
Republican
Independent
Libertarian
Constitution
Green
365
173
0
0
0
0
69,456,897
59,934,814
738,475
523,686
199,314
161,603
Joe Biden
Sarah Palin
Matt Gonzalez
Wayne Root
Darrell Castle
Rosa Clemente

2004George W. Bush (43rd)
John Kerry
Ralph Nader
Michael Badnarik
Michael Peroutka
David Cobb
Republican
Democratic
Independent
Libertarian
Constitution
Green
286
251*
0
0
0
0
62,040,610
59,028,439
463,655
397,265
144,499
119,859
Dick Cheney
John Edwards
Peter Camejo
Richard Campagna
Charles Baldwin
Pat LaMarche
*One elector from Minnesota cast a vote for John Edwards.

2000George W. Bush (43rd)
Al Gore
Ralph Nader
Pat Buchanan
Harry Browne
Republican
Democratic
Green
Reform
Libertarian
271
266*
0
0
0
50,456,002
50,999,897**
2,882,955
448,895
384,431
Dick Cheney
Joe Lieberman
Winona LaDuke
Ezola B. Foster
Art Olivier
*One elector from the District of Columbia left her ballot blank to protest the city's lack of representation in Congress.
**Although Gore received more popular votes, Bush received more electoral votes and therefore won the presidency.

1996Bill Clinton (42nd)
Bob Dole
Ross Perot
Ralph Nader
Harry Browne
Howard Phillips
Democratic
Republican
Reform
Green
Libertarian
Taxpayers
379
159
0
0
0
0
45,590,703
37,816,307
7,866,284
685,128
485,798
184,820
Al Gore
Jack Kemp
Pat Choate
Winona LaDuke
Jo Jorgensen
Herbert Titus

1992Bill Clinton (42nd)
George H.W. Bush
Ross Perot
Andre Marrou
James "Bo" Gritz
Democratic
Republican
Independent
Libertarian
Populist
370
168
0
0
0
44,909,326
39,103,882
19,741,657
291,627
107,014
Al Gore
Dan Quayle
James Stockdale
Nancy Lord
Cy Minett

Kwenye political parties Ross Perot 1992 na Ralph Nader 2004 na 2008 wameandika "Independent". Unajua maana yake nini hii?

Hujaelewa kwamba "kuwa na chama" hakuhusiani na kuwa "private candidate". Nimetoa mfano wa Lowassa hapo juu hujauelewa bado?

Marekani mtu anaweza kuwa Democrat, akaona wanakoenda Democrats huko siko ninakokutaka mimi, akataka kupata nomination akashindwa.

Kushindwa kupata nomination ya chama chake hakumzuii kuendeleza kampeni yake ya kutaka urais, kwa sababu ataendelea kutafuta urais kama Independent. Nimekupa mfano wa Lowassa hapo ju, ama hujui kusoma, ama mgumu wa kuelewa. Inawezekana kabisa ni mgumu wa kuelewa kwa sababu hujui kusoma na hujui kusoma kwa sababu ni mgumu wa kuelewa.

A vicious cycle of ignorance.

Private candidacy inampa mtu ambaye hana chama, au yule ambaye ana chama lakini hataki/ hawezi kutumia tiketi ya chama aweze kugombea urais.

Wewe unachanganya madawa gani sijui kwa ku assume kwamba private candidates wanatakiwa wasiwe na vyama, nani kasema hilo? Wapi?

Unashindwa kutenganisha mtu kutohitaji chama cha kumdhamini katika uchaguzi na mtu kutokuwa na chama.

Haya ni mambo mawili tofauti.
 
nngu007 hivi unasoma unapo quote au?

Ralph Nader (Ind) - 2008 Election - ProCon.org

Ralph Nader
space.gif
Independent Presidential Candidate

Attorney, Author, and Political Activist
 
Kwenye political parties Ross Perot 1992 na Ralph Nader 2004 na 2008 wameandika "Independent". Unajua maana yake nini hii?

Hujaelewa kwamba "kuwa na chama" hakuhusiani na kuwa "private candidate". Nimetoa mfano wa Lowassa hapo juu hujauelewa bado?

Marekani mtu anaweza kuwa Democrat, akaona wanakoenda Democrats huko siko ninakokutaka mimi, akataka kupata nomination akashindwa.

Kushindwa kupata nomination ya chama chake hakumzuii kuendeleza kampeni yake ya kutaka urais, kwa sababu ataendelea kutafuta urais kama Independent. Nimekupa mfano wa Lowassa hapo ju, ama hujui kusoma, ama mgumu wa kuelewa. Inawezekana kabisa ni mgumu wa kuelewa kwa sababu hujui kusoma na hujui kusoma kwa sababu ni mgumu wa kuelewa.

A vicious cycle of ignorance.

Private candidacy inampa mtu ambaye hana chama, au yule ambaye ana chama lakini hataki/ hawezi kutumia tiketi ya chama aweze kugombea urais.

Wewe unachanganya madawa gani sijui kwa ku assume kwamba private candidates wanatakiwa wasiwe na vyama, nani kasema hilo? Wapi?

Unashindwa kutenganisha mtu kutohitaji chama cha kumdhamini katika uchaguzi na mtu kutokuwa na chama.

Haya ni mambo mawili tofauti.

Yes, It does matter in USA Unakumbuka OBAMA na HILLARY CLINTON ? wote ni Democrat na Hillary ndie aliyetegemewa kushinda kwa UPANDE wa Democrats; Lakini OBAMA na campaign yake pamoja na HILLARY na BILL CLINTON's kumshambulia kwa Maneno ya AJABU... Lakini yeye alijijenga from GRASSROOT LEVEL... kwahiyo akamshinda HILLARY CLINTON the established one...

Lakini, Hillary hakuhama CHAMA sio Rahisi kuwa INDEPENDENT sababu nilizokueleza lazima uwe affiliated na chama kingine

Sasa kama HUKO BONGO Wamefanya hivyo kumsitiri LOWASSA hayo ni yao lakini ni SIO DEMOCRASIA ni UPENDELEO kama Walivyo hao VIONGOZI waliochaguliwa kutengeneza HIYO KATIBA...

Katiba ya KENYA watu Mashuhuri Hawakuchaguliwa kuitengeneza; Wanasiasa hawakuhusishwa kuitengeneza hawakuwa na MUVUTO toka kwa CHAMA TAWALA... Hii inaonyesha kulikuwa na hulka za hapa na pale kila sehemu

Ndio nakupa HABARI hii INDEPENDENT CANDIDATE USA wanakuwa affiliated na vyama vingine... Unaona NATIONAL ni INDEPENDENT lakini REGINAL kime-registered lakini ni INDEPENDENT kwasababu hakiko states zote...

NAKUAMBIA nimelifuatila hili suala nipo huku na kama unataka makabrasha yangu yote yatakuumiza kicha kuyasoma
 
What has that got to do with the price of pork in China?

Nani kasema wamefanya hivyo kumsitiri Lowassa?

Katiba ya KENYA watu Mashuhuri Hawakuchaguliwa kuitengeneza; Wanasiasa hawakuhusishwa kuitengeneza hawakuwa na MUVUTO toka kwa CHAMA TAWALA... Hii inaonyesha kulikuwa na hulka za hapa na pale kila sehemu

What has that got to do with private candidates? Unaelewa swali hapa?

Ndio nakupa HABARI hii INDEPENDENT CANDIDATE USA wanakuwa affiliated na vyama vingine... Unaona NATIONAL ni INDEPENDENT lakini REGINAL kime-registered lakini ni INDEPENDENT kwasababu hakiko states zote...

Kuna uchaguzi wa rais unaokuwa regional?

NAKUAMBIA nimelifuatila hili suala nipo huku na kama unataka makabrasha yangu yote yatakuumiza kicha kuyasoma

Bado unabisha kwamba Marekani hawaruhusu independent candidate hata baada ya webpages ulizotuletea wewe mwenyewe kuonesha kwamba Ralph Nader alikuwa independent candidate?

Umeona nchi zote hizi kwenye Wiki zinazoruhusu independent candidates?

Independent (politician) - Wikipedia, the free encyclopedia

Mbona mnataka kufanya hiki kitu cha ajabu sana hamna kwingine kokote duniani?
 
Kumbe ndio maana chadema walianza kelele za kudai ati wanapinga rasimu ya katiba. WANAOGOPA KIVULI CHAO WENYEWE SASA NAPATA PICHA HALISI WANACHOKIOGOPA SI KINGINE BALI ZITTO AKIJITOA AKAAMUA KUWA INDEPENDENT CANDIDATE.

Sijaona yenye mantiki wala mashiko kwenye kauli ya mtei. Huo ni utopian wenyewe tunaousema kila siku wa kuwa lazima ati uwe ndani ya chama ndio ugombee urais. Wanasahau kuwa vyama vinaundwa na wananchi na wananchi ndio wanaomchagua huyo rais. Rais hawajibiki kwa vyama anawajibika kwa wapiga kura waliomchagua kwani wao ndio wamempa kazi ya magogoni.
 
...nimefuatilia hoja za Kiranga na majibu ya Nngu007 najikuta naishia kucheka tu, ni burudani tosha...
 
Kumbe ndio maana chadema walianza kelele za kudai ati wanapinga rasimu ya katiba. WANAOGOPA KIVULI CHAO WENYEWE SASA NAPATA PICHA HALISI WANACHOKIOGOPA SI KINGINE BALI ZITTO AKIJITOA AKAAMUA KUWA INDEPENDENT CANDIDATE.

Sijaona yenye mantiki wala mashiko kwenye kauli ya mtei. Huo ni utopian wenyewe tunaousema kila siku wa kuwa lazima ati uwe ndani ya chama ndio ugombee urais. Wanasahau kuwa vyama vinaundwa na wananchi na wananchi ndio wanaomchagua huyo rais. Rais hawajibiki kwa vyama anawajibika kwa wapiga kura waliomchagua kwani wao ndio wamempa kazi ya magogoni.

Mgombea URAIS independent asiye na Chama.... Ndio anapotoa maoni yake siyo kwa nafasi zingine....Marais wote wenye vyama pia wanawajibika kwa wananchi... nchi zote zenye Demokrasia ya vyama ndivyo ilivyo... kuwa na Chama haimzuii raid kuwajibika kwa wananchi....isipokua kwa uchanga wa uanasiasa wa watanzania ... RAIS binafsi anaweza kuwa binafsi kweli....vyama vina saidia kujua km kweli yake...mfano anaweza akawepo RAIS aliyefadhiliwa na taifa lenye fedha nyingi la nje ili awatumikie na Watanzania tukipewa wali au pilau tunamchagua... "majuto hua ni mjukuu"
 
Mbona mnataka kufanya hiki kitu cha ajabu sana hamna kwingine kokote duniani?[/QUOTE]

Lamsingi ni je Independent candidacy is an answer to the leadership vacuum that is so evident? Mimi siamini kuwa Tanzania haikuwahi kuwa na right direction on leadership na pia utamaduni wa Taifa unaolenga maendeleo ya mtu, Mgombea binafsi hatakuwa na ushawishi wa lazima kuyarejea ... Ataanzisha msingi wake mwenyewe Jambo ambalo hakuna anayejua km kuna mafanikio au la....! na akija mwingine atafanya hayo hayo....party affiliation comes along with the national tradition on political issues which is healthy to the national development which has a lot of past experience as an important tool to succeed in setting up effective policies for national development
 
fugiken

Upande mwingine wa swali hili ni, je vyama vinaweza kukwamisha progress?

Vyama ni custodians tu wa political process. Sasa kwa nini uvipe vyama -custodians- haki ambazo wananchi wenyewe ambao ndio wenye nchi yao hawana?

Jibu ni ndiyo.

Unapokuwa na nchi ambayo watu makini wanashindwa kupata uongozi kwa sababu hawataki upuuzi wa vyama, inafaa kuwapa nafasi kama wagombea binafsi. Hususan kama vyama vinapitisha kina Kikwete, Lusinde na Profesa Majimarefu.

Kitu muhimu ni kuweka impeachment process kwa rais yeyote. Aliyepita kamamgombea binafsi au kwa chama.

It's not like Kikwete is not behaving like some Sultan already.

Tradition is what got us here. It is time for reexamination. Thats a big part of this whole exercise, isn't it?

Kunyima watu nafasi ya kugombea uongozi kwa sababu hawana/ hawataki uwakilishi wa vyama leo ni sawasawa na tulivyokataza watu wasigombee uongozi kwa sababu si wanachama wa CCM jana.

Tofauti pekee umebadilisha "CCM" na kuifanya "vyama vya siasa".

Mtei anajua hili. Na anajua nguvu za CHADEMA zitapungua kama Shibuda wa kesho ataweza kutoka CCM na kugombea ubunge Maswa au hata urais wa Tanzania bila ya kuhitaji kuwa sponsored na CHADEMA.

This is more about the guild maintaining control than about democracy. Angetaka democrasia ya kweli angeshangilia hili.
 
Last edited by a moderator:
Mgombea URAIS independent asiye na Chama.... Ndio anapotoa maoni yake siyo kwa nafasi zingine....Marais wote wenye vyama pia wanawajibika kwa wananchi... nchi zote zenye Demokrasia ya vyama ndivyo ilivyo... kuwa na Chama haimzuii raid kuwajibika kwa wananchi....isipokua kwa uchanga wa uanasiasa wa watanzania ... RAIS binafsi anaweza kuwa binafsi kweli....vyama vina saidia kujua km kweli yake...mfano anaweza akawepo RAIS aliyefadhiliwa na taifa lenye fedha nyingi la nje ili awatumikie na Watanzania tukipewa wali au pilau tunamchagua... "majuto hua ni mjukuu"

Bottom line ni kwamba, leo hii Watanzania wanaweza kuchaguliwa rais na mtu mmoja. Kwa sababu vyama vina nguvu sana kiasi kwamba huwezi kuwa rais bila ya kupitishwa na chama, hata kama 90% ya watu hawana chama na hawataki longolongo za vyama.

Unaposema kuwa na chama hakumzuii rais kuwajibika kwa wananchi, ukumbuke pia kwamba kutokuwa na chama hakumzuii rais kuwajibika kwa wananchi vilebile. In fact kama rais anataka kuwajibika kwa wananchi kwelikweli, rais asiye na chama ana urahisi wa kuwajibika kwa wananchi moja kwa moja kuliko rais mwenye chama, hana Halmashauri za chama, hana loyalgy na chama. Of course this can swing both ways, which is your legitimate concern.

Tusiweke mtego wa panya unasao wahusika na wasiohusika. Kama tatizo ni kwamba rais anaweza kuwa na nguvu sana na kusababisha madhara mengi nila checks akiwa independent, ondoeni nguvu za kimungu za rais. Kwa sababu kama mnategemea chama ndicho kimuadabishe rais, ni lini chama kimemuadabisha rais Tanzania? Tanzania ni nchi ya top down, ukishakuwa rais ndiyo ushakuwa sultani,na hiviNyerere kashajifia ndiyo basi tena, maana angalauyeyealiweza kum shame rais informally. Sasa kama tatizo rais ana nguvu sana punguza nguvu za rais, regardless kama ameshinda kwa nguvu za chama au kama independent.

Tusitake kuwanyima watu nafasi ya kutimiza haki yao ya kikatiba kwa kuogopa kitu ambacho ufumbuzi wake upo pembeni kabisa.
 
Mzee anazeeka sasa, rais awajibike kwa nchi na wananchi na si chama au kikundi chochote. Tanzania ni zaidi ya vyama
 
kwa nini wenye vyama vyao wamwogope mgombea binafsi? Historia ya nchi yetu inaonesha kuwa CCM wamekuwa wapinzani wakubwa wa mgombea binafsi. Sasa naona hapa hata mzee Mtei akijiunga kule kule.

Wenye vyama wanaogopa wagombea binafsi kwa sababu wagombea hao watawanyima nafasi ya kuteka "process" ya kuteua wagombea wa urais. Wagombea wenye nguvu watakuwa hawana cha kupoteza kwa kuwa kwenye vyama au kutoka nje, hivyo vyama vina wasi wasi wa kupoteza "relevance" katika zoezi zima la kuamua nani awe rais. Hii ni hatari kwa vyama.

Vyama vya siasa katika nchi yetu vimekuwa vikitegemea sana nguvu ya mtu mmoja mmoja kujijenga. Hili nalo ni baya. Yaani chama hakina mvuto wala mwelekeo, lakini akija fulani chamani, ghafla chama kinakuwa na nguvu ambazo hakikuwa nazo. Hapa imekuwa vyama kuwategemea watu, badala ya watu kuvitegemea vyama, sababu vyama vyetu havina mfumo imara unaoeleweka wa kidemokrasia ambamo watu wanalelewa na kukua. Unaweza kuona CCM pamoja na ukongwe wake leo hii kinaogopa watu - yaani mtu mmoja mmoja anaweza akawa tishio kwa Machinery ya chama kizima. Hapa maana yake ni kuwa vyama ni dhaifu, visivyo na demokrasia, fuata upepo, visivyojengwa juu ya msingi imara wa sera, n.k.

Matokeo ya hii imekuwa ni vyama kuwatumia watu kujinufaisha badala ya kuwajenga watu na kuwaweka juu. Mtu aliyejengwa na kuimarishwa na chama anajua kuwa bila chama yeye peke yake si kitu. Wawili si mmoja.

Sasa badala ya vyama kulalamikia na kuwaogopa wagombea binafsi, vinatakiwa vijiandae kwa kuunda mfumo imara wa kidemokrasia ndani yake utakaofanya wagombea binafsi wakose "relevance". Marekani hali iko hivyo. Mtu mmoja mmoja anaogopa kusimama peke yake dhidi ya "machinery" ya Democrats au Republican na hivyo independents mara nyingi wamekuwa ni wasindikizaji tu.

CHADEMA na CCM wajenge machinery kama zile za Democrats na Republican (GOP), hawana haja ya kulia lia na kupambana na mgombea binafsi. Huku kupinga pinga na kutaka kuzuia wagombea binafsi ni ushahidi tosha kuwa vyama hivyo vinawaogopa wagombea binafsi. Vinawaogopa sababu havijajipanga. Wagombea binafsi watavipa changamoto vyama hivyo vijipange, hivyo hawana budi kuwepo.

Visingizio vya kuwa mgombea binafsi anaweza kununuliwa havina mashiko, kwani vyama havinunuliwi? Kauli hiyo tumeshaona haina nguvu ukizingatia historia ya nchi yetu na jinsi ambavyo kwa muda mrefu tulivyoshuhudia watu fulani fulani wakivitia mifukoni mwao na kuviburuza kama wapendavyo. Kwenye swala la kununuliwa na watu, magenge ya mafia au Mataifa ya nje - vyama vya siasa haviko "imune". Kwa hiyo hiki si kigezo cha kuzuia wagombea binafsi.

Vyama vijiandae kwa kujenga mifumo bora ya demokrasia ndani yake. Ni mifumo hiyo itakayoviwezesha vyama kuwashinda wagombea binafsi na visijaribu kutumia nguvu ya sheria kuvilinda. Vyama inatakiwa vijengwe na watu kwa nia ya kusema "umoja ni nguvu". Ikiwa umoja ni nguvu, vyama vinaogopa nini? Hapa ni wazi vyama vinajua kuwa hakuna umoja ndani yake. Wagombea binafsi watasaidia kuleta umoja ndani ya vyama. Udikteta ndani ya vyama ni mbaya zaidi.
 
Baada ya rasimi ya katiba kuruhusu mgombea binafsi inaonekana wazi kuwa jamaa wa chukua chako mapema wapo matumbo joto....nilipita kijiw kimoja kuna hawa wazee makada walikuwa wanapiga story..wanasema hii ikipita tumekwisha...
 
Tanzania kwasasa inahitaji viongozi wa kisiasa wenye watu wa nyuma yao, kuwauliza na kuwahoji pale wanapotenda kinyume. Watu ni kupitia taasisi za vyama vya siasa hasa kile ambacho viongozi wanaotawala wanatoka. Rais kwa mfano ni vema atokane na chama ambacho kitamtuma kutekeleza matakwa ya wengi ili akivuruga, sauti ya wengi imwajibishe. Kwa nchi maskini yenye rasilimali nyingi hivi, kuweka 'rais binafsi' ni kuuza nchi. Omba Mungu rais huyo aongozwe na busara, akigeuka kuwa chizi anauza nchi then anaishia. Kwa neema hii ya gesi na madini tutarajie wagombea binafsi kununuliwa na kuwezeshwa na mataifa makubwa ili washinde na baadae kuhujumu nchi. Kwa kifupi, niwaombe watanzania tukatae kuruhusiwa mgombea binafsi kwenye katiba yetu kwani hasara na risk ni kubwa kuliko faida.
 
Kama mgombea binafsi atapata kura za Watanzania zaidi ya asilimia 50% basi atakua ameakisi na kubeba mawazo sawa na Watanzania walio wengi na hiyo ndiyo inayoitwa demokrasia (siafikiani na demokrasia).

Kama wewe ni mshabiki wa demokrasia basi inabidi ukubaliane tu na Ugombea binafsi.
 
Back
Top Bottom