Mtego wa Rais kwa CAG


Hiyo ni kawaida sana kwenye masuala ya kiuchumi.

Ndiyo maana kuna kitu kinaitwa intelligence.

Nnafurahi sana kusikia Rais kuyasema hayo.

Hilo ni dongo kwa wale wanaosema "anakurupuka".

Hongera Magufuli, hivyo ndiyo sahihi, lazima upate information kutoka sehemu tofauti kwa miono tofauti ili ufanye maamuzi sahihi.

Ndiyo maana ulipomtunbua Anne Kilango nikasema yule mwanamke ni bogus kabisa kutokuelewa kuwa Rais anapokutuma kazi ana njia nyingi nyingine za kupata taarifa.

Mleta mada usiwe kama Anne Kilango. Tumia kichwa chako kufikiri japo kiduchu na usikiwache kuwa ni mzigo tu juu ya mabega yako.
 
Binafsi, naona ni sawa kabisa, nchi zote zilizoendelea hakuna siku hata moja utafanya kazi pekee ni lazima kuna taasisi nyingi sana zinakufatilia kuona unachofanya kama kipo sahihi/ repoti zinakuwa sahihi.

Na pia , Rais amefanya vizuri sana kumwambia wazi kuwa kuna timu za watu wengine pia wanaofanya utafiti juu ya hicho kitu.

Na hii itasaidia sana watu kuwa waadilifu.

Labda, ushauri sasa Rais, wakati mwingine na kazi zitakazofuatia usiseme kuwa anawafatilia .
Alifanye kwa siri kisha alinganishe na majibu yanayoletwa na tume au wataalamu au hao invisibles.

Na hili litaipatia akili hata bunge ili lisiwe kundi la vibwagizo vya ndiyoooooooo na kiitikio cha siyoo.

Lazima, tufike mahala pazuri kama watu watamuelewa JPM.
 
Si kwamba hamwan CAG la hasha!! Bali kiuahalisia nikutaka report yenye uhakika kwa kua ktk nyanja zinazo ipa taifa fedha ni madin na uwezekano upo wa kufanywa figisu figisu ikatengenezwa report isiyo sahihi na ndyo maana amempa mkwara huo.
 
mtu analalamika pesa haitoshi kukagua hesabu zote za serekali utamwamini vipi wakati anaweza hongwa raisi yuko sahihi kimtizamo wahasibu walikagua mahesabu miaka kumi hawakuwahi kuleta hasara iliotokana na wafanyakazi hewa leo tuwaamini vipi jpm hadanganyiki
 
Hatuwezi kuota. Magufuli kaweka kodi mpaka ya ndoto tunabana matumizi.


Si kweli.

Magufuli hawezi kuweka sheria mpya bila kuipitisha hiyo sheria bungeni. Sijaona kodi yoyote mpya.

Sema upinzani hamna hoja ya siasa mlichobaki nacho ni hoja za kurukia, mnataza wapi kuna uoenyo ndiyo mnabwabwaja.

Nnashangaa sana pale nnapoona upinzani unakosa mawazo mapya (ideas), unakosa hata kuongolea matukio (events) unabaki kuongelea watu.

Hoi.
 
mkuu upo sahihi inaonyesha dhahiri kuwa mwenye nchi hana mahusiano mazuri na mkaguzi mkuu wa serikali (hana imani nae).
 
Hivi sheria inasemaje? CAG ana haki ya kufanya auditing kwenye taasisi/kampuni binafsi? Au ni pale tu kunapokuwa na maelekezo maalum?
 
Magufuli yeye ni bunge, mahakama, serikali ya mitaa na mpaka kanisa.

Sijui unaongelea bunge gani wakati kashaliamrisha bunge litunie fedha za tafrija yake kwenye habari za hospitali.

Utaongelea mahakama gani wakati Magufuli kahutubia Mahakama na kuipangia kazi.

Utaongelea serikali za mitaa gani wakati Magufuli kaenda kwa Mzee wa Upako na kuaguza barabara itengenezwe.

Anaenda kanisani na kutoa hotuba ya kisiasa mbele ya kanisa.

Na juzi kaingikia mpaka wasanii anaaanza kuwapangia mistari ya kuandika kwenye nyimbo zao.

Sasa hivi ataomba atoe single na Ney wa Mitego.
 
Only in God we trust...
 

Bahati mbaya tuliyonayo ni hao ambao ndiyo wenye access kwenye key boards...Watanzania average wana akili zao ila kwasababu tu ya hawa waovu wachache walinyimwa haki ya kupata elimu na nafasi zenye kuwawezesha kutoa maoni yao kama hawa waliokosa uzakendo kwakua tu mkate wao sasa umepunguzwa ukubwa kwakugawia wenzao...
 


Naam, wakati watu wanalia vitanda hamna mahospitalini wewe unafanya sherehe ya mamilioni? Inaingia akilini hiyo?

Kuhusu mzee wa upako, ni safi sana. Hebu soma hiki kipande "...wenye mahitaji ya kuabudu waabudu...".

Ukitaka "context" ya hicho kipande, pitia hapa: Siasa, Uchumi, Dhahabu, Neema na Laana zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…