Mtego aliotegewa Abdul Nondo na "watekaji" wake,hauna tofauti na ule wa Odwang Odwaa mwanafunzi Mganda UDSM

Ngaliba Dume

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,710
3,669
Yaliyomkuta Abdul Nondo ndiyo yaleyale yaliyowahi kumkuta mwanafunzi mmoja raia wa Uganda aliyekuwa chuo kikuu cha Dsm akifahamika kama Odwang Kefas Odwong(?).Miaka karibu 12 iliyopita,Odwang alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dsm akisomea sheria.

Hakuna kijana aliyesoma UDSM kati ya mwaka 2004-2009 asiyemjua Odwang,huyu alikuwa ni mwanafunzi toka nchini Uganda,mwanaharakati na mkosoaji mkubwa wa uongozi wa seeikali ya wanafunzi(DARUSO),na kuna wakati harakati zake zilipelekea mpaka kuwa mkosoaji wa serikali ya CCM.

Odwang alikuwa jasiri sana,yeye hakuwa anategemea mkopo wa Serikali ya Tanzania,lakini mara zote alikuwa anasimama mstari wa mbele kutetea haki za wanafunzi wenzake,mwaka 2006/2007 aliitisha maandamano makubwa sana toka mataa ya Ubungo mpaka viwanja vya Jangwani.

Maandamano haya yalikuwa nyuma ya kina Julius Mtatiro,Owawa,Bush mtoto wa Mama Leah(kwa sasa kibaraka mkubwa wa Serikali) na wengineo,dhima kubwa ilikuwa ni kupinga 40% ya mkopo,wakati huo serikali ilikuja na sera kuwa wanafunzi wote watapata 60% ya mkopo na 40% watajilipia wenyewe kwa njia ya wazazi wao.

Baada ya tamko hili,UDSM ililipuka,kukawa na maandamano na mgomo mkubwa sana,Odwang alikuwa kinara,akisimama Mabibo Hostel pale "Car Parking" akitoa sauti kwa nguvu "Odwaaaaa" kule blocks za wanawake za A,B na C zinaitikia "Odwaaaaang",huku za wanaume zikirindima kwa miruzi na kelele.

Serikali ilitishika,Mabibo Hostel mpaka Main Campus pale Rev Square ilikuwa ukisikia sauti ya Odwang,basi lazima kule Utawala kina Prof Mkandara watikisike.Odwang Kefas Odwang akawa anapata interview kwenye vyombo vya habari na anaelezea "uonevu" wa serikali kwa wanafunzi.

Kila walipomtafuta Odwang walishindwa kumpata,maana kama kuongoza maandamano ya wanafunzi,yeye alikuwa ana haki kama mwanafunzi na member wa DARUSO anayekatwa pesa kila mwaka kuichangia DARUSO.Na dalili zilionyesha watu walitaka Odwang agombee urais au awe Waziri Mkuu.Hii iliwatisha sana watu wa Lumumba.

Wanafunzi UDSM walipata ujasiri ziaidi sababu ya Odwang Kefas Odwang,na serikali ikaanza kumtafutia "dawa" Odwang ili "kumpoteza".Iliutumia ubalozi wa Uganda nchini Tz,lakini walishindwa sababu hata nyumbani kwao Uganda,famili ya Odwang ilikuwa na "ugomvi" na serikali ya Mseven sababu ya aina ya utawala wake.

Odwang alikuwa akiishi maeneo ya Mikocheni,huko ndiko ambapo maisha yake baada ya shule alikuwa akikaa na kuishi,baada ya njia zote kushindikana kumpata Odwang,wenye nchi yao wakampandikizia Odwang mwanamke,alikuwa dada mrembo haswaa.

Alikuwa "mwanafunzi bandia" wa kitivo cha sheria,akiishi Block F,eneo ambalo kwa wakati ule waliokuwa wanaishi wengi ni "Postgraduate Students" hata kama akiwa ni "Undergraduate" basi anatoka katika familia njema.

Kama ilivyokuwa mbinu ya "Honeypot trap",naye Odwang akaingia mkenge,na baadae akawa anamkaribisha yule dada "mwanafunzi" nyumbani kwake.

Wakati huo BAVICHA haikuwa moto kama leo,hawa kina Mnyika walikuwa wakionekana Nkurumah hall kwenye "Public Talk" lakini si kwa nguvu za BAVICHA ya leo.

Odwang alipoingia kwenye mtego,yule mwanamke akatengenezwa na akamuwekea Odwang kadi ya Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) kwenye moja ya begi lake,na baadhi ya machapisho kama katiba ya UVCCM na ilani ya Chama 2005/2010.Ndani ya kabati lake ukakutwa muhutasari wa UVCCM kuelekea sherehe za miaka 30 ya CCM mwaka 2007.

Huu ulikuwa ni mtego mkubwa sana kwa Odwang,maana katika ile form ya "Foreign Students" ya kujiunga chuo Kikuu (UDSM)miaka hiyo,kulikuwa na kipengere cha "Applicant Pledge".

Sehemu ya "Pledge" ya "Foreign Student" ilikuwa inasema "I as a foreign student,I will not participate in any form of political activities such as organizing or joining a political party,attending political meetings,publishing articles and declarations,or participating in political demonstrations".

Kwa kukutwa na nyaraka za chama,muhutasari wa kikao cha UVCCM na kadi ya UVCCM yenye jina lake,kulimfanya Odwang apoteze sifa ya kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu Dsm,na siku ya tukio,akiwa hajui alipo "mpenzi" wake wa Mabibo Hostel na simu yake ikiwa haipatikani hata hewani,Odwang alichukuliwa moja kwa moja mpaka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere,na kusafirishwa kwenda kwao Uganda kupitia shirikia la ndege la Kenya(Kenya Airways).

Huu ndio ukawa mwisho wa Odwang Kefas Odwaa,mwanaharakati na kijana jasiri aliyehamasisha wenzake kugomea 40% na kuitisha maandamano na kuhutubia Revo Square" kwa hamasa kubwa.Michezo hii haiwezi kuwa ya kwanza kwa Nondo,wakati haya yanatokea,Bashite alikuwa chuo cha Uvuvi Nyegezi na part-time kondakta wa daladala za Sahara to Nyegezi huku akitafuta sifa za kujiunga chuo cha Uvuvi Mbegani kwa level ya diploma.

Anayefanya picha hii iungue na isikamilike vizuri,ni yule jamaa wa kada wa CCM wa Bagamoyo aliyemuokota Abdul Nondo msitu wa Sao-Hill akiwa hajitambui,akampa nauli ya tax ili afike Mafinga mjini,na huyu "mpenzi" wa Nondo,anaweza kuwa kama yule "Mpenzi" wa Odwang aliyeandaa safari ya Odwang kurudi Uganda kwa mafanikio makubwa.Mambo haya yanafikirisha sana.
 
umenikumbusha mbali kidogo kipindi hicho Udsm ilikuwa na wanaume kweli kina Deo Daud Mbasa.sasa hivi hamna kitu ile ndiyoooooo ya kanda ya kati ndio imehamia hapo.
 
Back
Top Bottom