Mtazamo wangu; Viongozi wenye ushawishi zaidi kwa mwaka 2023

ndo vile

Member
Mar 11, 2023
25
12
1. Samia Suluhu Hassan
Huyu ndiye Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,pia mwenyekiti wa chama cha mapinduzi,chama kikongwe na cheye heshima kubwa sana barani Afrika,taarifa zisizo rasmi zinasema chama hiki kina wafuasi zaidi ya millioni 35 ndani na nje ya mipaka ya Tanzania,kwa mtazamo wangu huyu ndiye kiumbe mwenye ushawishi zaidi kwa mwaka 2023 nchini Tanzania.

2. Engineer Hersi Saidi
Kutokana na mabadiliko ya kikatiba yaliyofanyika katika timu ya Yanga kwa sasa huyu ndiye rais wa timu hii,tangu achaguliwe kwenye nafasi hii timu yake imeweza kupata mafanikio makubwa katika ligi za ndani hata katika michuano ya kimataifa,hivyo kupelekea wafuasi wa timu hii kumpenda huyu kiumbe,taarifa zisizo rasmi zinasema taasisi inayoiongoza ina wafuasi zaidi ya milioni 30 ndani na nje ya mipaka ya nchi,kutokana na kupendwa na wafuasi wake kiongozi huyu amekuwa akiwataka wafuasi wake wafanye vitu fulani na wafuasi huwa wanatii mfano wote vaeni vipensi,nyoeni vipara n.k kwa mtazamo wangu huyu nampa namba mbili kwa kuwa na ushawishi.

3. Mohamed Dewji
Huyu ni raisi wa heshima wa klabu ya Simba sports,bilionea huyu amekuwa chachu ya mafanikio ya klabu hii kubwa na yenye mafanikio yaliyotukuka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania,taarifa zisizo rasmi zinasema kuwa klabu hii inawafuasi zaidi ya millioni 30 ndani na nje ya mipaka ya Tanzania ,kwa mtazamo wangu nampa nafasi ya tatu kwenye watu wenye ushawishi kwa mwaka 2023.

4. Bonifase Mwamposa
Mtume huyu mwenye huduma ya inuka uangaze,amekuwa akivunja rekodi zake mwenyewe za kujaza idadi kubwa ya watu kila anapokuwa anafanya huduma,sina takwimu zozote kuhusu makadirio ya idadi ya wafuasi wake ila Mwamposa kwa 2023 ametisha sana pia ni mtume mwenye wafuasi watiifu sana,maelfu kwa maelfu ya wafuasi wake hujitokeza kila anapoenda kufanya huduma,kwa mtazamo wangu mtume huyu nampa namba 4 kwa 2023

5. Diamond Platnumz
Msanii bora wa kipindi chote wa muziki wa bongo fleva haswa kwa waimbaji,msanii mwenye mafanikio zaidi kwa Afrika mashariki na kati,mshindi wa tuzo mbalimbali ndani na nje ya mipaka ya Tanzania,mkurugenzi wa wasafi media,kijana huyu ni moja ya vijana wenye ushawishi mkubwa sana hapa nchini haswa kwenye mitandao ya kijamii,miziki yake imekuwa ikipendwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania haswa na kundi la vijana,kwa mwaka 2023 kwa mtazamo wangu kijana huyu ameshika no 5 kwa ushawishi.
 
Back
Top Bottom