Albedo
JF-Expert Member
- Feb 24, 2008
- 5,559
- 1,452
Siasa za Makundi zilizonogeshwa na Kile kilichoitwa "Kujivua Gamba Ili Kukinusuru Chama" sasa zimepelekea kutokea Makundi Makubwa ndani ya CCM yanayohatarisha Ustawi wa Chama hicho ( Tuendelee kuomba Mungu Kife Kabisa). Kwa Mtu anayefuatilia kwa Karibu Kabisa Mienendo na Minyukano ndani ya Chama Kicho Chenye Fikra zinazofanana Uzee wake ataona kwamba CCM sasa imegwanyika katika Makundi yafuatayo
1. CCM -Sitta: Hili ni lile kundi ambalo baada ya Kushindwa kanzisha CCJ sasa linaonekana kwamba linataka kuanzisha Chama ndani ya Chama. Hili ni kundi ambalo linajitahidi sana kutaka kuaminika kwa Watanzania kwamba ni Watakatifu ndani ya CCM. Nyuma ya kundi hili wamo akina Nape, Ole Sendeka, Kilango, Mwakyembe. Kundi hili linapambana kuhakikisha kwamba mwaka 2015 linafanikiwa kumpenyeza Mgombea wao wa Urais. Ni kundi ambalo limejaa wanafiki tukianzia na Samwel Sitta ambaye leo anaiita Kampuni ya Dowans aliyozima Mjadala wake Bungeni kuwa ni ya Kihuni. Huyu Babu ni Mnafiki anayeongozwa na Visasi vya Kuukosa Uwaziri Mkuu 2010. Ni kundi ambalo linaonekana kutumia Kujivua Gamba kama turufu ya kuwamaliza wabaya wao wa Kisiasa.
2. CCM-Lowasa: Hili ni lile kundi linaloamini kwamba Lowasa hakuwa na kosa katika kashfa ya Ricmond na kwamba Lowasa aliamua Kujitoa Sadaka ili kukiokoa Chama. Kundi hili linaona kwamba yule aliyejitoa Sadaka ili kukiokoa Chama dhidi ya Hasira ya wananchi sasa amekuwa Kafara. Ni kundi lenye Nguvu sana na Nguvu ya hili kundi ilidhihirika pale Lilipowazuia wale "Mitume" katika kundi la kwanza kukanyaga Igunga katika kipindi cha Kampeni za Uchaguzi mdogo wa Igunga. Ni Kundi ambalo linaamini kwamba Katika CCM hakuna aliye Msafi wa Kumyooshea Kidole Mwezake kwamba ni Fisadi. Ikumbukwe kwamba Lowasa anashutumiwa kwa Ishu ya Richmond pekee. Wachambuzi wa Mambo wanauliza kwamba Iweje IPTL iwe haramu lakini Richmond iwe Nongwa? Wanauliza vipi Kagoda, Deep Green , Meremeta, Tangold mbona Haziguswi? Kundi hili limeapa kufa na CCM
3. CCM-Membe. Hii ni CCM ambayo inategemea kudra na Huruma za Mwenyekiti, Wachambuzi wa Mambo wanasema kwamba Kundi hili liko kwenye Kundi la Kukosa maana kwa Sasa Mwenyekiti hana nguvu za kuamua nani awe Mgombea Uraisi. Ni Kundi ambalo linajaribu kujipendekeza zaidi katika Kundi la CCM-Sitta kama Fisi likingoja Mfupa Uanguke.
Wachambuzi wa Mambo wanasema kwamba Kwa Hali ilivyofikia ndani ya CCM ni Kudra za Mwenyezi Mungu zitakiwezesha chama hicho kikongwe kabisa Kupita salama katika Uchaguzi wa 2015
4-CCM-JF. Katika mtandao wa hapa jamii forums pia Makada wa CCM wametofautiana Kimtizamo na Kitu pekee kinachowaweka pamoja ni pale inapokuwa CCM against CDM.
4.1-CCM-Rostama: Hii ni CCM ambayo haitaki kusikia kwamba Rostam ni Gamba ni CCM ambayo kwao Rostam ni Role Model. Ni CCM inayoongozwa na Mwanamama FaizaFoxy na Malaria Sugu. Ni CCM ambayo imeapa kufa na Rostam