Mtazamo Ufaao Kuhusu Makosa

Mtazamo Ufaao Kuhusu Makosa

Mtayarishaji

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
291
Reaction score
198
Don na Margaret walifurahia kutembelewa na binti yao na familia yake. Katika sherehe ya kuwaaga, Margaret, ambaye zamani alifanya kazi ya upishi, aliandaa tambi na jibini, chakula kinachopendwa zaidi na wajukuu wake wawili.

Wote walipokuwa wameketi, Margaret alileta chakula na kukiweka mezani. Alinyanyua kifuniko, na kushangaa kuona mchuzi tu wa jibini ndani ya chombo!

Alikuwa amesahau kuweka tambi kwenye mchuzi huo!

Sisi sote hufanya makosa, haidhuru umri au uzoefu tulio nao. Huenda tulisema bila kufikiri, au tulifanya jambo fulani wakati usiofaa licha ya kwamba huenda ni zuri, au labda tulisahau kitu fulani.



Maswali ya kutafakari:


Kwa nini makosa hutokea?

Tunaweza kuyashughulikiaje?

Je, tunaweza kuyaepuka?



Mtazamo unaofaa kuhusu makosa utatusaidia kujibu maswali hayo.
 
Ila kuna baadhi ya maeneo na wakati ambao hutakiwi kufanya kosa na ukikosea unaharibu kila kitu, hivyo ili kuepuka kufanya kosa ni kuwa makini muda wote na ukiona kuna dalili ya kufanya kosa omba msaada wa haraka au kapumzike kwanza, japokuwa hata kupumzika huenda ikawa kosa jingine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom