MTAZAMO: Mungu bado hajalitupa taifa lake la Tanzania

FUTURE HUNTER

JF-Expert Member
Apr 30, 2018
2,022
2,591
Nakumbuka mwaka 2012 nikiwa mkoa mmoja nyanda za juu kusini nilikuwa mwana maombi upande wa UKWATA.Kipindi Fulani wana maombi walikubaliana kufanya mfungo wa takribani siku 30 huku wakiomba Mungu awajibu mambo kadhaa.

Mambo hayo ilijumuisha kubainisha harakati za kichawi kwenye ile shule, Mungu kuipatia nchi Rais atakaye kidhi mahitaji ya Tanzania kwa wakati huo (Kuna kitu watanzania waliki miss kutokana na mwenendo wa kipindi hicho) Uhalali wa babu wa loliondo.Maombi haya ya kufunga yalifanyika kwa kupokezana kwa wana maombi wote. Ukifunga leo wewe kesho ni Mwingine. Siku moja tukiwa kwenye maombi saa mbili usiku,mwenzetu mmoja akodondoka chini na akaanza kunena kwa lugha isiyoeleweka eleweka.Wana maombi wakaendelea kushusha maombi zaidi basi akatulia kasha sauti ikatoka kinywani mwake ikisema “ Vijana wote sogeeni hapa”!

Basi tukasogea na kumzunguka yule mwenzetu kIsha tukaanza kuambiwa mambo tuliyoomba kipindi cha maombi, Babu wa loliondo ni wakala wa shetani na akalaumu sana kwa nini tunakuwa na imani haba, Pili tukaambiwa kuliombea kanisa moja kubwa kuliko yote hapa nchini kutokana na utitiri wa washirikina kwenye kanisa hilo na tatu hakika tukaambiwa 2015 tutapata rais mzuri atakaye kata kiu ya yale watanzania walikuwa wakiyalilia. Tangu siku zile niliishi kwa imani kubwa sana nikisubiri 2015 nione ni nani atakuwa rais. Ile sauti toka kwa Yule mwenzetu ilivyomaliza basi ikatuaga na ghafla jamaa akazinduka na kuwa mtu wa kawaida kabisa na yeye asijue hata alichokiongea

Baada ya uchaguzi nikiri kuwa nilifurahi kumwona raisi aliyeapishwa na kimoyo moyo nikakumbuka na yale maonesho ya Mungu basi nikasema ukurasa mpya hakika umefunguliwa kwa taifa teule. Mwanzo wa mheshimiwa nilifurahi na kuona mwelekeo mpya kwa nchi yetu kila uchwao.Lakini ndani ya miaka miwili kuna mda nilianza kujiuliza hivi huyu mtu ndio Yule halisi Mungu alituahidi siku zile? Nilipata wasi wasi mkubwa baada ya kuona uhasama,chuki, mauaji uporaji na matendo mengi mengi yasiyo ya kibanadamu yakifanyika ndani ya utawala ule.Ikanipa wasi wasi kiasi kwamba moyoni nikawa nahoji kuwa kwa nini Mungu karuhusu haya yanatokea wakati aliahidi kuleta mfuta machozi.

Kila siku hali ilizidi kuwa mbaya kwa ujumla kiasi kwamba wengi wakawa wamekata tama huku na mtawala akijenga choko choko pengine za kutaka kabisa kung`ang`ania kabisa kubaki madarakani.Uhasama chuki na uonevu na matabaka vilitapakaa mno kiasi kwamba upendo baina yetu ulififia sana na uhasama ukajaa.

Je, Mungu ameamua kumuita mtumishi wake kwake ili kulilinda Taifa lake dhidi ya chuki mbaya iliyokuwa inajengwa na kukuzwa siku hadi siku? Sina majibu kiukweli lakini inanifikirisha sana hii ama kweli huenda Mungu ametumia kura ya VETO kuokoa waja wake toka mtumishi wake ambaye ni kama aligeuza kinyume mambo yote alioyoagizwa awatendee kondoo alio pewa na Mungu au la ni wito wa kawaida ambao kila binadamu amepangiwa siku ikifika lazima aende.

Nahitimisha.Tutende haki na tuishi kwa utu na kujaliana kila mmoja kwa nafasi yake.Mungu huinua haki.
Hakika tutaenzi siku zote yale mema uliyolitendea Taifa la bwana.Kwa uthubutu ule ulihitajika mno ili kulijenga taifa letu ni bahati mbaya upande wa pili wa mzani ukawa unachafua yote mema unayofanya upande A

Asanteni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom