Mtazamo: Mjadala wa utata wa 'Billion''

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,409
31,394
Takribani siku kadhaa mitandao ya jamii imegubikwa na hoja ya utata wa akiba ya Taifa (6,253B). Hoja kubwa si kiasi si thamani ya kiasi bali neno Bilioni katika dollar ya kimarekani badala ya Milioni. Kiasi ni kikubwa kikilinganishwa na Milioni za mikopo, watu wanahoji kwanini kukopa ikiwa pesa ipo

Zipo pande mbili za sakata hili, ya kwanza inashutumu upotoshaji na kuhoji kwanini umetokea. Upande wa pili ni unasema ni makosa ya kibaindamu yasiyo na madhara na halipaswi kukuzwa

Hoja zote zina mantiki kutegemeana na unaliangalia vipi na mtazamo gani suala zima. Aidha, ukubwa wa suala unaonyesha Taifa linavyogawanyika hata kutoafikiana !!

Kauli ya Mh Rais SSH haifanani na ya mtu mwingine, ni kauli ya Taasisi ya Urais inaweza kuwa Ombi, amri au Sheria. Kauli hiwezi kurahishwa kama 'slip of tongue') kughafilikiwa)

Taasisi ya Urais (Ikulu) ni nyeti inapata 'resources' zote , rasilimali watu na nyenzo na vitendea kazi kuliko taasisi nyingine ili kutekeleza majukumu kwa wepesi, haraka na usahihi

Ikulu ina watumishi wa kada zote wakiwemo watayarishaji na wapitia hotuba za Mh Rais. Makosa hayawezi kupewa uzito wa udogo kwavile yanaweza kuwa na athari na hatari

Mfano,kukiwa na mvutano wa nchi yetu na 'Jirani'na Rais wetu akasoma hotuba ''.... Tutakwenda vitani'' badala ya ''...hatutakwenda vitani'' kosa litakuwa na madhara na hatari kinyume na makusudio ya Mh Rais. Haiwezi kusemwa ni typo

Ikiwa Rais atashuhudia makubaliao ya dollar milioni 1.23,mkataba ukaandikwa milioni 12.3 hili ni tatizo kwa Rais, serikali na nchi kwa ujumla

Wasaidizi wa Rais ni lazima wawe makini, si kazi ya Mh Rais kusoma kila neno au tarakimu. Inakuwaje kosa la Bilioni 6.253 likatokea? Ikulu hakuna 'proofreading' ya kazi za Mh. Rais?

Kuna sababu ya kwanini watu wana 'react' kwa kosa hili; Kwanza kumekuwa na makosa mengi ya taarifa za Ikulu kila wakati.

Mfano, Rais amemteua Bw X katika nafasi Y na Bwana Z katika nafai Q.
Halafu taarifa inarudia tena kabla ya uteuzi bw. X alikuwa na Bwan Y alikuwa.....

Taarifa ya sentensi mbili inaandikwa kwa ukurasa mzima, achilia mbali makosa ya lugha.

Mfano mwingine, Ikulu inatumia muda mwingi sana kuwatambua washiriki wa hafla

Shughuli inaanza kwa kutambulisha waalikwa,kila anayefuata anaanza mlolongo ule ule wa kutambua walioshiriki kuanzia Mh Rais hadi mkurugenzi au mwenyekiti wa bodi

Mlolongo hauzingatia ujumla, akitajwa Waziri mkuu tayari anawakilisha Cabinet, kwanini mmoja mmoja atajwe tena?

Hivi kwanini wakuu wa vyombo watajwe kwa ujumla halafu mmoja mmoja kwa vyeo!

Rais ni mkuu popote alipo hivyo anawatambua wachache kiitifaki na si mlolongo hadi mwenyekiti wa bodi au mkurugenzi.

Rais akimtambua VP, PM na RC, Mabibi na Mabwana inatosha, hawa wanawakilisha taasisi na washiriki wengine, kwa namna moja au nyingine wanawajibika kwa serikali. Rais anaongea na wananchi ambao ni mabibi na mabwana!

Kwanini PM halafu waziri na naibu wake!!

Tulizoea kuwasikia marais kama Nyerere wakianza kuhutubia kwa kutambua wenye shughuli wachache kisha ' ndugu wananchi' kwa maana kila mmoja.

Kuna tatizo katika Itifaki, muda mwingi unapotea bila sababu kutambua washiriki

Mambo kama haya yaki ''accumulate' wananchi huonyesha kutoridhishwa na utendaji wa wasaidizi wa Rais. Hili la Bilioni lianeleza hisia kwa watendaji wa tasisi nyeti nchini.

Sababu ya pili ya 'reaction'. Taarifa ya Bilioni 6.253 ilihojiwa mapema kidogo
Kwanini Wafanyakazi wa Ikulu hawakusahihisha hadi ilipogeuka kuwa kichekesho?

Ikulu na vyombo vingine havikuweza kubaini tatizo hilo hadi kugeuka kibwagizo mitandaoni

Hili linamchafua Mh Rais, wasaidizi ima hawawajibiki au wana viwango vyenye mashaka.

Mh Rais hakuwa na kosa, hata hivyo, makosa ya wasaidizi hayawezi kutengwa naye. Rais ana mamlaka ya moja kwa moja au kupitia taratibu nyingine kwa wasaidizi wake.

Rais ni mteuzi wao na yakitokea haya '' the buck stops with her'' kama alivyosema Rais mmoja wa Marekani

Makosa ya Ikulu hayana udogo hata kidogo! yana impact kwa jamii kwa ujumla. Hakuna sababu ya kwanini Ikulu iwe sehemu ya 'makosa'. Je, tuna upungufu wa wataalam?

Kuna tatizo mahali, paangaliwe. Tusijadili ''wanaozomea'' tuangalie wanachozomea

Tusemezane
 
Bajeti yetu haijitoshelezi na huwa tunategemea misaada. Hawa wanaotupa misaada kwa data hizi wataridhia kuendelea kutusaidia au ndiyo tumeshakua donor country?
Ndio maana nimesisitiza kwamba wanaohalalisha hili kosa kwa udogo au 'slip of tongue' wanakosea
Ikulu ni kubwa sana haina kosa dogo kwasababu inababe maisha ya watu milioni55

Taarifa ya Mh Rais ikiandikwa '' Anyongwe' badala ya 'Asinyongwe' kuna madhara kwa maisha ya mtu. Wafanyakazi wa Ikulu wana nyenzo zote, iweje hali kama hii itokee?

Hotuba iliandikwaje bila proofreading na kwanini ilipobainika kuna tatizo imechukua masiku!
 
Back
Top Bottom