Wanabodi,
Kama kawaida yangu, nipatapo fursa, hupita huku na kule na kubadilishana mawazo na watu mbalimbali wa kada tofauti. Kwa takriban siku 3 zilizopita, nimepata fursa ya kutembelea mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ambayo ndiyo inayo dorminate Kanda ya Kaskazini, kiukweli CCM Imechokwa mpaka basi!.
Siku zote nimekuwa nikisema humu, CCM imekuwa ikichaguliwa na wengi sio kwa sababu ya kupendwa au kukubalika sana, bali kwa mazoea tuu wengi wakiwa ndicho chama pekee walichokifahamu tangu wamezaliwa, na wengine wakikichagua CCM kama asante ya kutuletea uhuru kupitia TANU, na idadi kubwa ya walio vijijini, wamekuwa wakiichagua CCM kwa ignorance tuu ya elimu ya uraia!. Sasa wale wanaichagua CCM kama asante ya kutupatia uhuru, ni oldguard, wanazidi kupungua na wachache waliobakia they days are numbered!. Wale wengi waliokuwa wakiichagua kwa ignorance, sasa wameamka!.
Kwa mujibu wa kada mbalimbali nilozungumza nao, wamethibitisha kuwa hakuna jinsi Ole Sendeka, Ole Medeye na Ole Nyaguro wataweza kusalimika, sehemu salama mpaka sasa ni Jimbo la Monduli tuu!.
Kama kasi ya upepo wa mwamko kama Kanda ya Kaskazini, utaingia kanda ya Ziwa kwa kasi hiyo hiyo, then hakuna jinsi yoyote ya kuiokoa CCM isipigwe mwereka uchaguzi wa 2015!.
Determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii, ni wapiga kura wa Kanda ya Ziwa ambayo ndiyo inayoongoza kwa idadi kubwa ya watu!. Kati ya watu milioni 40 wa sensa ya mwaka 2002 kwa Tanzania yenye makabila 120, Wasukuma peke yao wako milioni 6!. Sasa ukiwajumlisha na Kanda ya Kaskazini, hata kama mikoa yote iliyobakia wataipigia kura CCM, bado kwa kanda hizo mbili pekee, zinatosha kabisa kuipiga chini CCM!.
Mwelekeo huu ni uthibitisho kuwa ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania, sio ndoto tena, ni kitu ambacho kinawezekana!.
Natoa mwito kwa Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu, tusiendekeze hizi siasa za chuki za kukichukia chama fulani bila sababu za msingi ya chuki hiyo, au kukipenda na kikishabikia chama fulani kwa upenzi tuu, matokeo ya mwisho ya siasa hizi ni kujengeana chuki zisizo na sababu!. Tupingane bila kupigana, tutofautiane kisiasa bila kuchukiana bali tupingane huku tukipendana!.
Hata mimi uchaguzi wa Arumeru, nilisimama na Sioi, tumekutana na Nasari pale Dodoma, tumekumbatiana, na kiukweli kutoka moyoni mwangu, sina chuki na Nasari, namkubali kwa dhati japo namhurumia Sioi kwa sababu ni rafiki!.
Nyie watu wa Kanda ya Kaskazini, msiichukie hivyo CCM, kwani pamoja na mabaya yake, pia kuna mema mengi imelifanyia taifa hili!.
Namalizia kwa kusisitiza, huu ni mtazamo tuu!
Wasalaam.
Pasco
Arusha.