Mtazamo: Dreamliner inataka kuwekwa rehani

Mtazamo: Dreamliner inataka kuwekwa rehani

Huyu Lisu sio mzalendo kabisa, ona sasa kawasaidia hawa Wajapani kutupiga B133, yaani halafu anataka wakamate Boeing yetu. Manina akili zitawakaa vema tu maana si kwa vibano hivi.
 
walipwe tu pesa zao maana bwana yule alisema tuna utajiri wa kutosha mpaka kuweza kukopesha pesa nchi nyingine
 
Siwezi kuweka hapa hadharani kwa misingi na maadili ya kazi yangu, lakini siwezi kuonyesha kufurahishwa na majanga ya aina hii yanayoikumba nchi.
Hata Mimi sifurahii matatizo yanayotukumba ila nawaponda waliofanya uzembe wa kujirudia mara kwa mara na kulisababishia taifa hasara ya mabillion

Sent from my SM-N910C using JamiiForums mobile app
 
Watu wanashangilia kwamba JPM anakomolewa na ndiye aliyetuingiza huko wakati kiukweli wakati hayo yanatokea JPM nakuwa wizara ya ujenzi

..kwani mkataba ulivunjwa mwaka gani?

..Waziri na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi alikuwa nani.

..Deni lililosababisha bombadier ikakamatwa lilitokana na mkataba uliovunjwa wakati Baba J akiwa waziri.

..Tunataka kuwajua wahusika waliosababisha hasara hii.
 
Mleta mada kaanza na heading MTAZAMO..,ina maana huo ni mtazamo wake,hivi kila mtu akileta mtazamo wake kuhusu siasa za TZ si itakuwa balaa?,kuna mtu hajui msimamo wa SALARY SLIP kwenye lolote linalohusiana na mabepari au wazungu?,na watu wanakomenti as if kaongea swala lililopo kumbe ni mtizamo na hisia zake na mahaba aliyonayo kwa mabepari.Ila uzuri maoni yake na mitazamo yake vinaishiaga JF tu.
 
Ujue hata huo uchaguzi unaweza kusogezwa mbele kisa PESA imetumika kukombolea ndege. Kwenye siasa kila tatizo linatumika kisiasa.
Uwache usogezwe tunyooke mwisho wa siku huyo Magu hapati hata shida yeye na mwanaye Bashite was wataendelea ku enjoy.
 
Wenye akili hawatoi cash Kununua midege ya aina hiyo. Tz inanunua cash. Very poor business thinking.
Ethiopia hawanunui cash. Wako mbali sana. Wanalipa kadri wanavyo operate
Hata British airways
 
Tukio haliumizi taifa,linamuumiza magu na kina bashite,sisi tushaumia vya kutosha tumeshakata tamaa maana tumeshanyanyaswa vya kutosha na hii serikali ya kidikteta...

Tumemuachia mungu mana magu anatumia madaraka yake kutunyanyasa anavyotaka...

Ila nimuambie tu magu cku zote mungu ndo anajua kutoa hukumu ya haki,atunyanyase tu anavyoweza but kuna siku itafika na mungu cku hiyo ndo atatoa hukumu dhidi ya wale wote wanaotumia madaraka yao kunyanyasa wengine
Hivi Zimbabwe wanavyopata shida unafikiri Mugabe na timu yake wanashida? Ndiyo kwanza wanajimwaga na ma shopping kwenye ma nchi tofauti
 
That's very perfect Mkuu..

Hiyo ndio namna pekee ya kuilazimisha serikali hii ilipe madeni yake hasa kwa hawa wakandarasi wa nje..

Konoike wapate usajili wa hiyo hukumu yao waende Paris wakazuie Boeing Dreamliner..

Mindege imenunuliwa bila kufata utaratibu, kibabe-babe tu wakati Nchi ina matatizo chungu tele yanayohitaji kutatuliwa kuliko kununua hizo ndege.
Huna akili hata robo. Ingekuwa una akili hata kidogo ungetetea vilivyo vyako. Ndege ya Tanzania ikishikiliwa means ni mali yako wewe imeshikiliwa. Kweli JF siku hizi haina watu.
 
ivi mnadhani kipindi cha JK madeni hayakuwepo? mikataba ilikuwa asitishwi? the problem with this mkulu ni jeuri hana chembe ya diplomacy katika akili yake na project kubwa kama hizi haziendeshwi kama tender za matikiti ni diplomacy ya hali ya juu inatumikaga na round table za watu wanaojua diplomacy sasa uyu anajiona too perfect lazima tufundishwe adabu tu na c kwamba wanaofurahia c wazalendo no.
ni impact ya uyu jeuri hataki ushauri wala kukosolewa
 
Mimi sio mwanasheria na wala sina ufahamu/utalaamu wa mambo haya ya mahakama za kimataifa.

Hata hivyo,kwa uelewa wangu,nadhani lengo la kampuni ya ujenzi ya Konoike ya Japani ni kutaka hukumu ya Mahakama ya Usuluhishi ya London isajiliwe na mahakama ya shirikisho nchi Marekani lengo hasa la wadeni wetu likiwa ni kupata idhini ya mahakama hiyo ya Marekani ya kuweza kukamata mali za Tanzania endapo deni wanalotudai halitalipwa na hapa bila shaka watakuwa wana-target ile dreamliner inayotarajiwa kuwasili nchi mwakani.

Tukumbuke kampuni ya Boeing inayotengeneza ndege za aina ya Boeing iko nchini Marekani.

Ni mtazamo tu.
hili ukiangalia kwa jicho lisilo na itikadi yoyote kuna ka ukweli fulani ndani yake.
 
Huna akili hata robo. Ingekuwa una akili hata kidogo ungetetea vilivyo vyako. Ndege ya Tanzania ikishikiliwa means ni mali yako wewe imeshikiliwa. Kweli JF siku hizi haina watu.
Mapengo weee..
I don't have dirty time to respond.
 
Back
Top Bottom