Mtawala anayegombea hatapata - Askofu Lazaro

Mtawala anayegombea hatapata - Askofu Lazaro

Chromium

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2008
Posts
589
Reaction score
187
Habari hii si propaganda kama za CCM. Pengine ni mwendelezo wa uthubutu wa viongozi wa dini (hasa Wakristo) wanaoamua kusema ukweli kwamba hali ya mambo si shwari serikalini.

na serikali hii ambayo haivumilii kusemwa tofauti na inavyotaka, inawakemea utadhani hawapendi kabisa kusikia udini wakati wakitokea viongozi wengine wa dini wakiwasifia (kama Kulola) wananyamza na kuomba waheshimiwe. Hii ni kawaida kabisa ya serikali dhalimu.

Sasa habari hii si njema kwa CCM lakini habari ndiyo hiyo.

Jumapili iliyopita nilikuwa kanisani kwa Askofu Lazaro na kwa masikio yangu nilimsikia mzee huyu akiwaonya wakristo kutokupoteza muda kuomba mambo ambayo Mungu hatayasikia. Akisoma kitabu cha Amos 4:6 na kuendelea, Askofu Lazaro alisema wazi kwamba Mungu amemwambia ataitikisa serikali kwa namna ambayo haikupa kutokea!

Mtawala anayegombea sasa hivi, hatapata. Na kwamba Mungu amempa jina la mtu ambaye atakuwa Rais wa nchi hii (japo hakuwa tayari kumtaja kuepuka itakavyopokelewa na watu)!

Na dalili ziko wazi. Kila mwenye macho naona namna CCM kilivyoishiwa na kubaki kutengeneza propaganda zisizona miguu. Naanza kuamini kwamba ni kweli mtawala anayegombea hatapata.

Tungoje tarehe 31 Oktoba!
 
MUNGU NDIYE MWENYEKUAMUA ITAKAVYOKUWA LK KAMA ATATUPA PhD SLAA TUTAMSHUKURU SN,
KILA JAMBO LINAMUDA WAKE.
 
Kweli yawezekana, ila kama ulivyosema kuwa utawala dhalimu, huu utahakikisha kuwa hawatoki madarakani lazima wataibua mbinu chafu ya kuvuruga matokeo...
 
Mungu tayari amekwishatoa viashiria kwa watanzania kuwa nani ni Rais na nani asiyesikia sauti ya Mungu. Tunamshauri JK asikilize sauti ya Mungu na kuanza kujiandaa kutoka Ikulu, na asijaribu kushindana na Mungu kwani habari haitakuwa njema kwake. Ndugu zangu watanzania Mungu amesikia kilio cha waja wake na sasa anawaletea ukombozi, ole wake atakaye jaribu kuzuia matakwa ya Mungu maafa yatamkuta.

Kumbuka wana wa Israel walipokuwa wanakombolewa kutoka utumwani, Mungu alimtuma Musa kwa Faraoh amwambie kuwa waache watu waende wakanitumikie jangwani, Faraoh akakaidi mapigo yakamwandama. Hatimaye akaruhusu, lakini bado akawa kichwa ngumu akawafuata wana wa Israel na wote tunajua jinsi majeshi yalivyo angamia ndani ya bahari nyekundu. Huyo ndiyo Mungu. Sasa ameyaona mateso ya watanzania.

Ole wako JK usipokuwa na busara na kukaidi sauti ya MUngu, sio siri maafa yatakuijia.
 
Yatosha kusema unampenda nani awe Rais lakini msimsingizie Mungu katika matamanio yenu.
 
Huyo askofu ameamua kuungana na Shekh Yahaya kufanya kazi ya kupiga ramli?
 
Tusubiri baada ya 31 Oktoba tutajua nani ni nani!
 
hakuna mwanzo usiokuwa na mwisho,utawala uliopo ndo unafika mwisho.
 
Mungu anasikia kilio cha watu wake. wameumia mno ila wanaangamia kwa kukosa maarifa ya kuchagua maisha bora si bora maisha.
 
Habari hii si propaganda kama za CCM. Pengine ni mwendelezo wa uthubutu wa viongozi wa dini (hasa Wakristo) wanaoamua kusema ukweli kwamba hali ya mambo si shwari serikalini.

na serikali hii ambayo haivumilii kusemwa tofauti na inavyotaka, inawakemea utadhani hawapendi kabisa kusikia udini wakati wakitokea viongozi wengine wa dini wakiwasifia (kama Kulola) wananyamza na kuomba waheshimiwe. Hii ni kawaida kabisa ya serikali dhalimu.

Sasa habari hii si njema kwa CCM lakini habari ndiyo hiyo.

Jumapili iliyopita nilikuwa kanisani kwa Askofu Lazaro na kwa masikio yangu nilimsikia mzee huyu akiwaonya wakristo kutokupoteza muda kuomba mambo ambayo Mungu hatayasikia. Akisoma kitabu cha Amos 4:6 na kuendelea, Askofu Lazaro alisema wazi kwamba Mungu amemwambia ataitikisa serikali kwa namna ambayo haikupa kutokea!

Mtawala anayegombea sasa hivi, hatapata. Na kwamba Mungu amempa jina la mtu ambaye atakuwa Rais wa nchi hii (japo hakuwa tayari kumtaja kuepuka itakavyopokelewa na watu)!

Na dalili ziko wazi. Kila mwenye macho naona namna CCM kilivyoishiwa na kubaki kutengeneza propaganda zisizona miguu. Naanza kuamini kwamba ni kweli mtawala anayegombea hatapata.

Tungoje tarehe 31 Oktoba!
Better words than Kulola's....Uzuri wa Lazaro ana hekima.Hajipendekezi kwa serikali ana msimamo lakini pia busara na ndiyo maana kwenye mgogoro wao wa uaskofu,Kulola alitumia wahuni kufanya fujo na serikali ilikuwa upande wake,hata hivyo kwa busara Lazaro akaachia ngazi...Mwenzake Kulola hana busara na ndio maana alisema JK ni chaguo la Mungu....Tofauti yake na Kulola ni kwamba yeye anawasikiliza waumini wake zaidi na ndio maana akaja na conclusion hiyo together with the fact kuwa ana kipaji cha unabii, whereas Kulola yeye anataka asikilizwe kwasababu ya maslahi yake kupitia serikali na ana ishara ya unabii wa uongo coz nasikia alishawaaga watu huko mwanza kuwa 2000 ni mwisho wa dunia!

Na Mungu kuitikisa serikali ina maana ni majaribu serikali itakayokutana nayo haswa ukizingatia wanataka kurudi madarakani kwa kila njia ikiwemo kupitia vibaraka wa udini kama Kulola na wengineo,na kwa mtu makini mwenye kupima upepo na kuwasoma watanzania,anajua kuwa this time wananchi wako makini zaidi.
 
]MUNGU NDIYE MWENYEKUAMUA[/COLOR] ITAKAVYOKUWA LK KAMA ATATUPA PhD SLAA TUTAMSHUKURU SN,
KILA JAMBO LINAMUDA WAKE.

Mkuu sisi ndio tunaamua nani tunamtaka, wewe kapige kura yako hiyo tarehe 31 na mchague slaa tunamuomba mungu atuwezeshe na kutupa afya njema na akili timamu za kufanya maamuzi sahihi..
 
Bwana, wewe wajua yote, uliytujua kabla hata ya kuzaliwa kwetu, tupe chaguo lako kupitia kura zetu.
 
Yatosha kusema unampenda nani awe Rais lakini msimsingizie Mungu katika matamanio yenu.
Haa haa haa!! Hee hee! Mkuki kwa nguruwe ehe? 2005 waliposema Kikwete chaguo la Mungu hamkusema wanamsingizia Mungu!! Bwaa!!! Hayoooo!!!!
 
Back
Top Bottom