Mtatiro unapoteza muda CUF...karibu CHADEMA!

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
Mimi ni mmoja wa Watanzania ninayeamini kwamba Naibu katibu mkuu wa CUF ndugu Julius Mtatiro ana influence kubwa kisiasa tatizo hana jukwaa la kusimamia ndani ya chama dhaifu cha CUF japo simjui kiundani(wadau mtamchambua). Naamini Bwana Mtatiro anapoteza tu muda kwa kuwepo kwenye chama kinachopoteza umaarufu kila uchao kwa kitendo chao cha kufunga ndoa na CCM.Mfumo wa vyama vingi sio tu mwanzo wa mabadiliko ya kweli, bali vyama makini ndio mwanzo cha mabadiliko ya kweli yenye tija kwa taifa.Viko wapi NCCR,UDP,TLP n.k., yale matusi ya vyama vya msimu toka CCM hayajawagusa kwa sababu tu wao ni matawi ya CCM. Tanzania kuna chama kimoja tu cha upinzani. Ndugu Mtatiro, CHADEMA:A S 103: ndio chama sahihi kwa ndoto zako za kisiasa. Tafakari..Usipoteze muda..Fanya Maamuzi!
 
hata mimi nilikuwa nakiwaza sana hicho kitu kuwa ni kwa nini mtatiro yuko ccm B anafanya nini wakati vijana wenzake tuko chadema mtatiro mura si uje chadema alafu huyu jamaa ni mkurya au ni kabila gani kwa sababu haya majina ya mtatiro ni ya kwetu pare tarime mura thoka uko mura njoo chadema na ungekuwa uku wetu ungekuwa mubhunge haya kaka hizo ni changa moto unaweza zifanyia kazi
 
Binafsi namheshimu huyu jamaa kwani alikuwa mpiganaji mzuri wa haki wakati tuko udsm. Nakusihi angalia tz inakoelekea ndugu yangu ndo hiyo uliyokuwa ukiiota ktk maisha yako? Mbona watu wa mara si wanafiki, hawapendi wanakuambia, uking'ang'ania kama nyambali wanaku-displini, iweje kaka upoteze muda wako huko ccm b? Hao cuf wamekuweka ili kujisafisha na udini tu.
 
Hivi Mtatiro ndiye yule jamaa anayeongea kwa kuigizaji mapozi na sauti ya Lipumba? Kama ni yeye basi hana maana kabisa.
 
kjana mtatiro anajaziba sana apunguze jazba kidogo ila nimmoja kati ya vijana wapiganaji mimi sithan swala la kuhamia chama fulani ndio suluhisho ingekua watanzania sisi niwatu wakupima,kusikiliza na kuelewa vizuri hoja za hawa wanasiasa tungeweza kupata viongoz wazuri bila kujali vyama..TATIZO TUNAANGALIA VYAMA HATUANGALII WATU TUWAPIME WATU WENYEWE NA SIKUWAPIMA KUPITIA KWA VYAMA VYAO VYA SIASA WANAVYO VIWAKILISHA
 
"jana mtatiro anajaziba sana apunguze jazba kidogo ila nimmoja kati ya vijana wapiganaji mimi sithan swala la kuhamia chama fulani ndio suluhisho ingekua watanzania sisi niwatu wakupima,kusikiliza na kuelewa vizuri hoja za hawa wanasiasa tungeweza kupata viongoz wazuri bila kujali vyama..TATIZO TUNAANGALIA VYAMA HATUANGALII WATU TUWAPIME WATU WENYEWE NA SIKUWAPIMA KUPITIA KWA VYAMA VYAO VYA SIASA WANAVYO VIWAKILISHA"

>>>Mfumo wa vyama vingi sio tu mwanzo wa mabadiliko ya kweli, bali vyama makini ndio mwanzo cha mabadiliko ya kweli yenye tija kwa taifa<<<
 
Binafsi namheshimu huyu jamaa kwani alikuwa mpiganaji mzuri wa haki wakati tuko udsm. Nakusihi angalia tz inakoelekea ndugu yangu ndo hiyo uliyokuwa ukiiota ktk maisha yako? Mbona watu wa mara si wanafiki, hawapendi wanakuambia, uking'ang'ania kama nyambali wanaku-displini, iweje kaka upoteze muda wako huko ccm b? Hao cuf wamekuweka ili kujisafisha na udini tu.

Unamainisha ni kama vile alivyoekwa pro.Safari na Chadema ili kujisafisha na udini?
 
Siasa za CDM Mtatiro haziwezi kwanza anatumia nguvu nyingi kuongea kuliko kufikiri, Jazba, hashauriki huwa analoliamini yeye anapenda lifanyike tena kwa jazba muda si mrefu mtasikia mgogoro wa kichama utakao sababishwa na yeye sioni atafit wapi CDM labda ajiunge abaki kuwa mwanachama wa kawaida kitu ambacho i dont think ataweza
 
Hapana jamaa namfahamu,nakumbuka alikuwa mpiganaji namba moja pale udsm 2007,2008 hadi anamaliza,alichangia sana kuibadilisha sera ya 40% kwa mikopo ya wanafunzi ila mlango aliongilia sasa nw ndo tatizo.namkubali sana mtatiro ana deserve kuwepo chama cha mabadiliko katika nchi hii, CHADEMA.
 
hata mimi nilikuwa nakiwaza sana hicho kitu kuwa ni kwa nini mtatiro yuko ccm B anafanya nini wakati vijana wenzake tuko chadema mtatiro mura si uje chadema alafu huyu jamaa ni mkurya au ni kabila gani kwa sababu haya majina ya mtatiro ni ya kwetu pare tarime mura thoka uko mura njoo chadema na ungekuwa uku wetu ungekuwa mubhunge haya kaka hizo ni changa moto unaweza zifanyia kazi

unaisi yeye shida yake ubunge?
 
Ukisoma gazeti la Mtanzania ya leo limeelezea mambo mengi kuhusu Itatiro. Lakini kubwa zaidi ni hili la kutaka kuiendesha CUF kichadema zaidi. Mfano wanasema alishauri Lipumba asiende siku ya kuapishwa kikwete na hata alishauri CUF watoke nje siku ya kupitishwa mswada wa katiba.

Hata mapendekezo ya kubadili mswada ambao umeshangiliwa sana na CUF yametoka kwake.

Mnakumbuka msimamo wake hapa JF kuhusu mswada ulikuwa tofauti sana na msimamo waliouchukua CUF. Kwa hali hiyo namshauri ajiunge tu chadema. Na gazeti limeeleza kuwa alimwandikia Lipumba msg kusema kuwa CUF hakiwezi kumfikisha mahali anapotaka na Lipumba akampa Unaibu ili asiondoke.

Namshauri asiendelee kukaa kwenye chama ambacho yeye mwenyewe hashabihiani na malengo na itikadi yake. Viongozi wa CUF wanamlalamikia kama pandikizi la chadema ndani ya CUF , si maneno yangu ila gazeti hilo
 
Back
Top Bottom