Baada ya Faustin Sungura kujikomba jana kwenye mdahalo akikandia hoja ya haki ya kuandamana kwa sababu anazozijua mwenyewe, aliinuka kamanda Julius Mtatiro na kusema kwa ujasiri mkubwa kile Sungura alichoshindwa kusema tena akiwa amepoteza ujasiri kabisa. Wachambuzi wa public speaking mtaona wazi kabisa kuwa Sungura alikuwa akisema kana kwamba ameambiwa ukisema tofauti na haya umekwisha. Hakusema toka nafsini mwake bali out of pressure. Mtatiro alitetea demokrasia akijua wazi kuwa kama leo mtu mmoja amefanyiwa vile, basi kesho kuna mwingine aweza kufanyiwa vibaya zaidi na kumkanushia moja kwa moja mjeshi aliyemwakilisha Mkuu wa majeshi.
Tangu siku nyingi niliwahi kuwaambia baadhi ya vijana kuwa Mtatiro ni mwanasiasa mzuri ila nahisi yuko choo cha kike. Mifano inayoonyesha ni cha kike ni kauli ya mwenyekiti wake kufanya kampeni za waziwazi msikitini hivi karibuni na picha zake kupostiwa UTube na yeye kushindwa kukanusha.
Nadhani Mtatiro hujachelewa, msimamo wako tunaufahamu, wewe bado ni kijana...unangoja nini huko CUF? Toka ndugu yangu toka ukaungane na wapambanaji wenzako mkomboe nchi hii toka kwenye mikono ya mabeberu.