Mtatiro atangaza maandamano ya CUF kupinga DOWANS

WanaJF na wapenzi wa CHADEMA,

Hii issue ya malipo kwa Dowans ni issue ambayo tumeipigia kelele sana humu JF,
Leo ametokea mtu, Chama na kinataka kutuonesha njia...wengine tumeanza kuwahukumu na kuwabeza na kuwaita majina..hivi tuko serious?
Au leo uchungu wetu juu ya malipo ya Dowans umekwisha?
Yaani threads zote tulizoanzisha kuhusu Dowans ni bure tu? Kwa vile CUF ndio wanaanzisha move hii?

Mimi nilitegemea hii ni issue ya wananchi wote na tungekuwa tayari kuyaunga mkono maandamano ya kupinga malipo kwa Dowans au tulitegemea chama fulani tu ndio kiitishe maandamano hayo?
Ushabiki wa chama mwanzo kuliko jambo la kitaifa linalowahusu wote?
Tuanche huu ushabiki..tuwaambie viongozi wa vyama tunavyovishabikia kuwa waunge mkono maandamano haya na wajitokeze kuandamana pamoja na CUF na sisi wenyewe pia.

Kuna mtoa mada mmoja alituchallenge kuwa sisi hapa JF kazi yetu domo tu,hatutaki kuchukua hatua ,sasa ametokea mtu,chama cha kukuza kilio chetu,kelele zetu, tusirudi nyuma tuwaunge mkono na tujitokeze kuandamana.

Tuwapelekee ujumbe vyama vyetu viwasiliane na CUF ili kufanikisha maandamano haya..huenda ukawa mwanzo wa vyama kushirikiana katika issues za kitaifa... na pengine watawala watanza kutia akili.
Haya Shime wanaJF.
 
Mi nadhani cuf walitakiwa wafanye utafiti kwanza kabla yakukurupuka kufanya hayo maandamano coz nachohisi ni kwamba vyama vingi vitataka kufanya Maandamano kupata credit kwa Umma na kila chama kitajitahidi kiwe cha kwanza kukiwahi kingine Matokeo yake yatakuwa ni Maandamano ya kisiasa na Hoja nzima ya Dowans itakosa mantiki.
Wote tumesikia kwamba TUCTA inaandaa maandamano yakupinga ongezeko la gharama ya umeme na wote tunajua Shirikisho hili linahusisha wafanyakazi wote kwa pamoja bila kujali ni ccm,cuf au cdm jiulize Wafanyakazi wote hawa wakiungwa mkono na wanafunzi wote,wafanyabiashara,wajasiria mali,watu wasio na kazi.Je ni kwanini vyama vyote visisikilizie hayo Maandamano ya TUCTA na kumobilize wanachama wao kuyaunga mkono nakushiriki rather than kuwagawa watu kwenye vijikundi vidogovidogo.
 
nice move CUF - mimi si mwanachama wa huko ila kwa vile maandamano yanahusu maslahi ya taifa basi naunga mkono MOVE iliyotangazwa na CUF. Wana JF tushirikiana bila kuangalia itikadi zetu wala dini zetu. Mungu ibariki Tanzania.
 
Bila kusahau kwa taarifa za kiitelijensia nilizopata,leo tar.1.2.2011 jiji la mwanza litawaka moto kati ya machinga na polisi ambao wanahamisha machinga kwa nguvu,tahadhar kwa wakazi wajiji lamwanza bagosha na bankima kuanzia asbuh jumatatu muwe makin kukatisha katikati ya mitaa yajiji lamwanza,hasa nyerere road na kenyata na pambaroad,hii ni kwa taarifa za kiitelijensia.
 
Sorry nimekusudia jumatatu 31.01.2011 mwanza ni machinga vs polis, tuombe amani na machinga watii sheria wasitake kupambana na dola wataumia.
 
Mie siamini iwapo viongozi wakuu wa kitaifa -- na hasa Jussa na Maalim Seif watakuwapo kuhutubia.

Jussa ni dam dam na Rostam -- kamwe hawezi kuwapo pale, achilia mbali kutoa hotuba ya kupinga Dowans kulipwa.

Na kwa Maalim Seif haitamkalia vizuri kupinga kile ambacho serikali ya CCM, ambayo yeye ni mshirika mkuu kwa upande wa Visiwani, imedhamiria kufanya, yaani kuilipa Dowans.

Lakini mimi nampenda sana Mtatiro, bila shaka anafanya hivyo kimakusudi tu kuwakomoa wawili hao. Namfananisha Mtatiro na Zitto katika Chadema, ingawa huyu Mtatiro anafanya mambo ambayo yana masilahi zaidi ya kitaifa kuliko huyo kijana mwenzake anayeonekana kutekwa na mafisadi.

Anyway, huu ni muono wangu to which I'm entitled.

kaka mbona UVCCM ilipinga kuhusu malipo ya Dowans? itakuwa CUF? Mie nadhani kunapokuwa na jambo la maslahi ya taifa basi wapinzani wawe kitu kimoja maana kama hamuaminiani itakuwa ngumu sana kushirikiana na hatimaye kushika madaraka ya Nchi.
 
wanaandamana kupinga nini ili hali wenyewe wapo serikalini huko zanzibar, wapo kimya kama dowans si swala la kitaifa, je wamewauliza wenzao
wa Zenj kuhusu Dowans? kule zenj CUF wapo serikalini, je mbona kimya? hawa ni CCM live wanatuzingua
 
Wazee,
Ni dhahiri sasa imebainika kuwa Rostam Azizi ndiye Dowans. Kama ndivyo, kwa nini wapinzani mnachelea kuratibu maandamano makubwa nchi nzima kupinga malipo kwa Rostam Aziz?
 
Safari hii iwe dar maandamano,mbona mnatubania wananchi wa dar! Kova atatupa kibali na ulinzi kwani hata wao wana uchungu wa salary yao kukatwa kupewa dowans..
 
Je kwa kufanya maadamano si mtakuwa mko nyuma ya makasisi, au mmetambua maana ya makasisi. Au mmeamua kusaliti mwisilamu mwezenu!!!. Lakini bila shaka ni mnataka kuonesha kuwa hamko na CCM inagwa mnapokea hongo yao kwa ajili ya kufanikisha ufisadi wao.
 
CUF kama bado wangekuwa kama Zamani wangeunganisha nguvu na Vyama vingine, lakini nadhani kuna umuhimu kama CUF wakifanya Dar basi siku hiyhiyo Chadema wafanye Mwanza ama Mbeya ama KIlimanjaro, au kote ili Serikali ijue nguvu ya wananchi ikoje
Kuna muda huwa sielewi matatizo tuliyo nayo vichwani sisi watanzania no wonder ccm wanatuchezea kila kukicha, ni kwa sababu hatuna akili, tumejaa ushabiki usio na tija. yaani kila siku hapa watu wanapiga mayowe ooh, dowans, dowans, umeme hakuna, ngeleja ajiuzulu and so on. sasa CUF wameandaa maandamano badala ya kuwatia moyo na kuungana sisi kama wananchi wa kawaida ili kulifanikisha hilo na kilio chetu kisikike kitaifa na kimataifa, here we go again na ushabiki wa vyama while we have a common problem. Ni wakati wa vyama vyote, dini zote, watu wa kada zote kuungana na kufanya maandamano ya ukweli bila kujali itikadi zetu maana hii ni ishu ya kila mtanzania awe cuf, chadema au ccm, au tlp, acheni huu ushabiki, maana haya haya si mashindano ya nani atascore higher marks, its about the wellbeing ya watanzania wote people. habari ya chadema nao waanzishe sijui ili kufanya counter attack ni upuuzi, tunashindania nini? mashindano ya aina hiyo subirini wakati wa uchaguzi, kwa sasa tuikomboe nchi hii kwa paomoja. nani aliyetuloga?
 
Je kwa kufanya maadamano si mtakuwa mko nyuma ya makasisi, au mmetambua maana ya makasisi. Au mmeamua kusaliti mwisilamu mwezenu!!!. Lakini bila shaka ni mnataka kuonesha kuwa hamko na CCM inagwa mnapokea hongo yao kwa ajili ya kufanikisha ufisadi wao.

crap, haijengi chochote zaidi ya kubomoa, what do you achieve kwa kueneza propaganda za aina hii. simameni pamoja mfanye kilicho bora kwa ajili ya taifa, mmbo ya aina hii hayamsaidii yoyote kati yetu. sanasana mnazidi kugawanyika na ccm wanapeta.
 
wanaandamana kupinga nini ili hali wenyewe wapo serikalini huko zanzibar, wapo kimya kama dowans si swala la kitaifa, je wamewauliza wenzao
wa Zenj kuhusu Dowans? kule zenj CUF wapo serikalini, je mbona kimya? hawa ni CCM live wanatuzingua

kwa hiyo you would prefer wakae kimya kama kila mtu alivyo kimya, at least wana courage ya kutoka mbele na kusema no, mbona wengine wote mnaowaamini wako kimya? acheni mawazo ya kitoto no wonder dowans italipwa maana watu wenyewe kama mawazo yenu ndo haya, who is going to stop ccm and dowans.
 
kaka mbona UVCCM ilipinga kuhusu malipo ya Dowans? itakuwa CUF? Mie nadhani kunapokuwa na jambo la maslahi ya taifa basi wapinzani wawe kitu kimoja maana kama hamuaminiani itakuwa ngumu sana kushirikiana na hatimaye kushika madaraka ya Nchi.

At least you understand and thanks. Ifikie mahali watu tupanuke akili na kujua kwamba si watu wote hata ndani ya ccm pia wanafurahia kinachoendelea, na cuf vilevile kuwa ndani ya serikali hiko zanzibar hakumaanishi wamefungwa midomo, especially bara maana kodi ni yetu na si ya wazanzibar itakayolipa dowans. msiwazuie watu wenye nia njema na nchi kuongea au kutake action kuhusu sereilkali eti tu kwa sababu wana some sort of ushirikiano na serikali, msiwazuie kwa vijineno vyenu vya kukatisha tamaa. acha wafanye kwa nafasi yao, na nyie mnaoongea sana bila kufanya action kaeni kimya kama hamtaki kuwaunga mkono.
 
WanaJF na wapenzi wa CHADEMA,

Hii issue ya malipo kwa Dowans ni issue ambayo tumeipigia kelele sana humu JF,
Leo ametokea mtu, Chama na kinataka kutuonesha njia...wengine tumeanza kuwahukumu na kuwabeza na kuwaita majina..hivi tuko serious?
Au leo uchungu wetu juu ya malipo ya Dowans umekwisha?
Yaani threads zote tulizoanzisha kuhusu Dowans ni bure tu? Kwa vile CUF ndio wanaanzisha move hii?

Mimi nilitegemea hii ni issue ya wananchi wote na tungekuwa tayari kuyaunga mkono maandamano ya kupinga malipo kwa Dowans au tulitegemea chama fulani tu ndio kiitishe maandamano hayo?
Ushabiki wa chama mwanzo kuliko jambo la kitaifa linalowahusu wote?
Tuanche huu ushabiki..tuwaambie viongozi wa vyama tunavyovishabikia kuwa waunge mkono maandamano haya na wajitokeze kuandamana pamoja na CUF na sisi wenyewe pia.

Kuna mtoa mada mmoja alituchallenge kuwa sisi hapa JF kazi yetu domo tu,hatutaki kuchukua hatua ,sasa ametokea mtu,chama cha kukuza kilio chetu,kelele zetu, tusirudi nyuma tuwaunge mkono na tujitokeze kuandamana.

Tuwapelekee ujumbe vyama vyetu viwasiliane na CUF ili kufanikisha maandamano haya..huenda ukawa mwanzo wa vyama kushirikiana katika issues za kitaifa... na pengine watawala watanza kutia akili.
Haya Shime wanaJF.
Very useful words. THANKS.
 
Mtatiro anatumiwa tu na CUF kuimarisha chama lakini kazi yake ikiisha atatimuliwa kama walivyotimuliwa akina James Mapalala, Rwakatarwe, Tambwe Hiza na wengineo. CUF walikuwa wanaitaka serekali ya SMZ na wameshaipata, na kazi yao imeshaisha. Nataka nimwone Maalimu Seif kwenye maandamano. Kama hayupo, then ni porojo tu. in fact CUF sio chama cha upinzani kwa sasa.
 
mi sioni tatizo kama mtatiro anatumiwa, na amekubali kutumiwa yeye mwenyewe na kwa utashi na akili yake timamu, we unaumia nini? na kama una akili timamu utajua hatumiwi na mtu bali anawatumikia wananchi kwa nafasi yake, hiyo ndiyo kitu cha muhimu ambacho kila mtu anayejiita mzalendo anatakiwa kuwa nacho, uwezo wa kuwatumikia wananchi bila kujali malipo. sasa hata akitimuliwa takuwa amefanya kazi yake vizuri, kama katiba mpya kwa ajili ya watanzania kaidai, kama kupinga dowans kaonyentya njia, and thats enough. maslahi ya wananchi ni zaidi ya cuf au maalim seif ndugu yangu, kama unamsubiri maalim seif ndo uone dowans imepingwa utasubiri sana, nguvu ya wananchi ni zaidi ya maalimu seif na lipumba na slaa so acha kukaa na kuongea pumba, play your part.
 
Back
Top Bottom