Baada ya taarifa za Prof. Lipumba Kwenda Zanzibar, ulinzi waimarishwa ofisi za CUF

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
UONGOZI wa juu wa Chama cha Wananchi (CUF) umeimarisha mfumo wake wa ulinzi kwenye Makao Makuu yake yaliopo mtaa wa Mtendeni, mjini Zanzibar wakati huu wa kuendelea kwa mgogoro wa uongozi.

Uimarishaji wa ulinzi unatekelezwa kwa makusudi hasa baada ya kupatikana taarifa ambazo hazijathibitishwa mpaka sasa, kwamba Profesa Ibrahim Lipumba, aliyefukuzwa uanachama wiki mbili zilizopita, amepanga kutinga kwenye ofisi hizo.

Mbali na ushuhuda kwamba ‘askari’ wa chama waitwao Blue Guards wameongezwa, mitaa yote na vichochoro vinavyoingilia mtaa wa Mtendeni, ina walinzi wengi wakiwemo waliowekwa kwa siri.

“Si uongo, mfumo mzima wa ulinzi hapa makao makuu Mtendeni umeimarishwa. Unajua zilienea taarifa za kiitelijensia kuwa Profesa Lipumba anatarajiwa kuja na kutaka kuingia ofisini,” amekaririwa mlinzi mmoja wa CUF.

Mlinzi huyo alipoulizwa kwa alivyosikia Profesa Lipumba aende Mtendeni kufanya nini wakati anajua hatua hiyo huenda ikamsababishia matatizo, mlinzi huyo alisema, “Tunasikia ametangaza kuwa anataka kuja makao makuu eti kukutana na watendaji wa chama waliopo huku Zanzibar.”

Hakuna kiongozi aliyekuwa tayari kuzungumzia suala hili upande wa Zanzibar kwani hata Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Salim Bimani alipoulizwa, ghafla simu yake ilikatika na haikupatikana tena.

Katika moja ya vikao vyake na waandishi wa habari akiwa Ofisi Kuu za CUF Buguruni ambako Profesa Lipumba amejichimbia na genge lake la watu wachache, amesikika akisema kuwa anakusudia kwenda Zanzibar kukutana na watendaji.

Profesa Lipumba alitangaza mwishoni mwa wiki kuwa anawataka watendaji wote ndani ya chama kufika ofisini ili kufanya kazi walizoteuliwa kuzifanya na kwamba kwa yule atakayekosa kufika na kukakosekana taarifa ya maandishi ya sababu yake, atahesabiwa kuwa amejiondoa katika nafasi.

“Nitateua wanachama wengine wa kufanya kazi walizopangiwa wale watendaji watakaokuwa wameshindwa kutokea,” alisema. Hata hivyo kwa taarifa zilizopatikana jana, hakuna mtendaji hata mmoja aliyemtii Profesa Lipumba.

Mtendaji mmoja kwenye ofisi hizo ameiambia MwanaHALISIonline kuwa hana moyo wa kufika ofisini kufanya kazi kwa kuwa mgogoro umesababisha kuwepo mazingira ya hofu Ofisi Kuu Buguruni.

“Hivi ukiangalia kwa mtu mwenye akili timamu, unakwenda ofisini pale kufanya kazi gani kama sio kutafuta kusakamwa,” alihoji mtendaji huyo wa ngazi ya juu.

Prof. Lipumba juzi alitangaza kutengua uteuzi wa watendaji uliofanywa wakati wa kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa (BKUT) wiki iliyopita mjini Zanzibar.

Mvutano unaendelea kugubika CUF ambayo Prof. Lipumba ameshika upande mmoja akiwa na viongozi wawili tu – Mgdalena Sakaya na Abdul Kambaya – ambao walisimamishwa uanachama pamoja naye 28 Agosti.

Sakaya alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama Bara wakati Kambaya alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma. Wote wanaendelea kujitambua kuwa ni viongozi halali.

Prof. Lipumba ambaye anadai kusimamia kutambuliwa na Msajili wa Vyama kama mwenyekiti halali kwa hatua yake ya kutengua kujiuzulu kwake, alifukuzwa uanachama 27 Septemba kufuatia kutotii wito wa kufika mbele ya Baraza Kuu kujitetea kwa tuhuma za kuvamia Ofisi Kuu Buguruni na kuvunja ofisi na kuharibu mali za chama.

Upande mwingine wa mgogoro unaongozwa na Katibu Mkuu Maalim Seif Shariff Hamad anayeungwa mkono na zaidi ya asilimia 90 ya Baraza Kuu la Uongozi.
 
CUF Mtendeni usipime

Posted by: Jabir Idrissa 11 hours ago 0 Comments 384 Views

Tweet

Share

ShareUONGOZI wa juu wa Chama cha Wananchi (CUF) umeimarisha mfumo wake wa ulinzi kwenye Makao Makuu yake yaliopo mtaa wa Mtendeni, mjini Zanzibar wakati huu wa kuendelea kwa mgogoro wa uongozi, anaandika Jabir Idrissa.

nachoweza kusema hapa BWANA HUYU hatoweza kupata ushirikiano anaoutaka kwa hao aliowateuwa kushika nyadhifa za juu... kwa maana wanaomuunga mkono BWANA HUYU wengi wao ni mbugila wasojua hili wala lile NO ELIMU.. ili BWANA HUYU apate watendaji ni lazima hao watendaji wawe wasomi. wengi ya wafuasi wake BWANA HUYU ni mizoga tu haina chochote inacho jua zaidi ya vibandiko na mikelele na baadhi yao ni kutoka upande uleee wa LUMUMBA wamechukua jukumu la kumsaidia BWANA HUYU ili afanikishe malengo yao ya kuivunja CUF kitu ambacho ni ndoto kulingana na michakato yao wanaLUMUMBA tangu walipo anza nao BWANA HUYU na BWANA YULEEEE akishiririkiana na kimada wake.
HATUSHIIIIIINDWIIIIIIIIII.... CUF ni ya wananchi na si ya BWANA HUYU.
 
Kutapa tapa kwende mbio sikupa kwenda mbio sikupata nakupa pole bwana yule nakuangulia kicheko
 
Huyo msela anaelala ofisini hana huo ujasiri wa kwenda mtendeni sanasana labda aende mtendeni ya kisutu dar
 
“Hivi ukiangalia kwa mtu mwenye akili timamu, unakwenda ofisini pale kufanya kazi gani kama sio kutafuta kusakamwa,” alihoji mtendaji huyo wa ngazi ya juu.
Mbona profesa yupo ofisini anachapa kazi, na maana hana akili timamu?
 
Umaskini mbaya kweli fainali uzeeni vijana tutafute pesa mapema kabla ya umri wa lipumba hivi ana watoto kweli au mke wangishamtoa humo ofisini kwa nguvu ,mwenyekiti haogi wiki nzima
 
Huyu Lipumba anazuiwa na wahuni wa blue guard angali yeye alimkaribisha Seif Buguruni akaona aibu kwenda....baasi huyu profesa Lipumba ni CUF na CUF ni Profesa Lipumba
 
Back
Top Bottom