Mtatiro amkubali Slaa

Mtatiro amkubali Slaa

mbinguni

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2013
Posts
2,767
Reaction score
1,068
NAIBU Katibu Mkuu (Bara) wa Chama cha Wananchi (CUF), Mtatiro Julius, amesema kuwa chama hicho kikifanikiwa kushika dola kitahakikisha kinashirikiana na watu safi akiwemo Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.

Akizungumza katika kipindi cha ‘Tuongee Asubuhi' kinachorushwa na televisheni ya Star tv, Mtatiro alisema chama hicho kipo tayari kuhakikisha wanakuwa na lengo moja la kuijenga nchi kwa kushirikiana na viongozi waadilifu.

Mtatiro, alisema chama hicho kimejiwekea malengo na kipo tayari kuongoza dola pamoja na kushirikisha watu safi ambao watakuwa wakisimamia vema utekelezaji na kuwaletea Watanzania maendeleo.

Alisema ni muhimu Watanzania wakapata dira ya taifa itakayowaongoza na kuonesha wanapotaka kuelekea.Kuhusu vyama vya upinzani kuwa chanzo cha kuvuruga amani, Mtatiro, alisema vyama hivyo havifanyi kazi ya kushawishi Watanzania waharibu amani ya nchi na kama wapo wanaofanya hivyo wanapaswa kuchukuliwa hatua.

Alisema kuwa amani iliyopo inalindwa na Watanzania wenyewe, hasa kupitia viongozi ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhubiri suala hilo.

"Sio kweli CCM inalinda amani ya nchi…amani iliyopo inalindwa na Watanzania na kila kiongozi anayesimama kuhubiri jambo hilo," alisema.

Alisema kuwa iwapo vyombo vya dola vinashindwa kuwachukulia hatua wale wanaoonekana kuvuruga amani basi vyombo hivyo vitakuwa vimeshindwa kufanya kazi.

Mtatiro alisema kuwa uzalendo umepotea miongoni mwa Watanzania kutokana na ufisadi unaofanywa na wale walioshika dola.
"Hivi kweli unaweza kuwahubiria Watanzania wawe wazalendo wakati wanaona matendo yanayofanywa na viongozi wao…waziri anakuwa na nyumba ya sh bilioni sita unafikiri watakuelewa kukizungumza uzalendo?" alihoji.

Alisema kuwa uzalendo unaenda na vitendo, hivyo ili kuurudisha ni muhimu viongozi waliopo madarakani wakaanza kujitafakari upya.

Kuhusu makundi, Mtatiro alisema kuwa yapo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sio katika vyama vya upinzani kwa kuwa wamekuwa wakijitahidi kuyaondoa.

[TD="bgcolor: #ffffff"]

[/TD]
 
Hata Vuvuzela Nape akiwa nyumbani kwake anamkubali Dr. wa Ukwee, a.k.a Rais wa Mioyo ya Watanzania. Lakini akija majukwaani, ili apate "Ujira wake wa Mwiha", anamwita Jeetu Patel "Baba"! Siku ingetokea Marehemu angefufuka! Sijui Jamaa angejificha wapi!
 
Kwa hiyo wachumia tumbo lazima waew wanafiki ili wapate ujira wao!
 
chadema iungeni mkono cuf ishike dola,wakati ni huu..
 
Nilimsikia,na mh Mwigulu akamwambia asiwasemehe wengine,akisemee cuf,namshauri dr Slaa nae atamke kuwakubali cuf au baadhi ya viongozi wa cuf
 
NAIBU Katibu Mkuu (Bara) wa Chama cha Wananchi (CUF), Mtatiro Julius, amesema kuwa chama hicho kikifanikiwa kushika dola kitahakikisha kinashirikiana na watu safi akiwemo Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.

Akizungumza katika kipindi cha ‘Tuongee Asubuhi' kinachorushwa na televisheni ya Star tv, Mtatiro alisema chama hicho kipo tayari kuhakikisha wanakuwa na lengo moja la kuijenga nchi kwa kushirikiana na viongozi waadilifu.

Mtatiro, alisema chama hicho kimejiwekea malengo na kipo tayari kuongoza dola pamoja na kushirikisha watu safi ambao watakuwa wakisimamia vema utekelezaji na kuwaletea Watanzania maendeleo.

Alisema ni muhimu Watanzania wakapata dira ya taifa itakayowaongoza na kuonesha wanapotaka kuelekea.Kuhusu vyama vya upinzani kuwa chanzo cha kuvuruga amani, Mtatiro, alisema vyama hivyo havifanyi kazi ya kushawishi Watanzania waharibu amani ya nchi na kama wapo wanaofanya hivyo wanapaswa kuchukuliwa hatua.

Alisema kuwa amani iliyopo inalindwa na Watanzania wenyewe, hasa kupitia viongozi ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhubiri suala hilo.

"Sio kweli CCM inalinda amani ya nchi…amani iliyopo inalindwa na Watanzania na kila kiongozi anayesimama kuhubiri jambo hilo," alisema.

Alisema kuwa iwapo vyombo vya dola vinashindwa kuwachukulia hatua wale wanaoonekana kuvuruga amani basi vyombo hivyo vitakuwa vimeshindwa kufanya kazi.

Mtatiro alisema kuwa uzalendo umepotea miongoni mwa Watanzania kutokana na ufisadi unaofanywa na wale walioshika dola.
"Hivi kweli unaweza kuwahubiria Watanzania wawe wazalendo wakati wanaona matendo yanayofanywa na viongozi wao…waziri anakuwa na nyumba ya sh bilioni sita unafikiri watakuelewa kukizungumza uzalendo?" alihoji.

Alisema kuwa uzalendo unaenda na vitendo, hivyo ili kuurudisha ni muhimu viongozi waliopo madarakani wakaanza kujitafakari upya.

Kuhusu makundi, Mtatiro alisema kuwa yapo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sio katika vyama vya upinzani kwa kuwa wamekuwa wakijitahidi kuyaondoa.

[TD="bgcolor: #ffffff"]
[/TD]

Kwanza kabisa Karibu sana JF. Pili Acha upotoshaji mkuu,wengi tulifuatilia mdahalo ule, alichokisema Mtatiro ni kuwa watakuwa tayari kushirikiana na watu potential bila kujali vyama vyao kumtaja Dr Slaa ilikuwa ni mfano tu lakini hakusema watahakikisha wanamshirikisha Dr Slaa kwenye serikali ya CUF.
 
Kafu ina viongozi kama watano cdm naomba tuwasajiri wajiunge na m4c maana chama chao hakiko mioyon mwa watu na kilisha kufa siku nyingi
 
ZAnzibar ni nchi kamili kabisa tatizo tu bado hawajiamini na hawajitambui.
 
Tunamkubali,tunamwamini,tunampenda Dr Slaa,nlifurahi kumsikia Mtatiro akizungumzia hilo jana
 
naibu katibu mkuu (bara) wa chama cha wananchi (cuf), mtatiro julius, amesema kuwa chama hicho kikifanikiwa kushika dola kitahakikisha kinashirikiana na watu safi akiwemo katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema), dk. Willibrod slaa.

Akizungumza katika kipindi cha ‘tuongee asubuhi' kinachorushwa na televisheni ya star tv, mtatiro alisema chama hicho kipo tayari kuhakikisha wanakuwa na lengo moja la kuijenga nchi kwa kushirikiana na viongozi waadilifu.

Mtatiro, alisema chama hicho kimejiwekea malengo na kipo tayari kuongoza dola pamoja na kushirikisha watu safi ambao watakuwa wakisimamia vema utekelezaji na kuwaletea watanzania maendeleo.

Alisema ni muhimu watanzania wakapata dira ya taifa itakayowaongoza na kuonesha wanapotaka kuelekea.kuhusu vyama vya upinzani kuwa chanzo cha kuvuruga amani, mtatiro, alisema vyama hivyo havifanyi kazi ya kushawishi watanzania waharibu amani ya nchi na kama wapo wanaofanya hivyo wanapaswa kuchukuliwa hatua.

Alisema kuwa amani iliyopo inalindwa na watanzania wenyewe, hasa kupitia viongozi ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhubiri suala hilo.

"sio kweli ccm inalinda amani ya nchi…amani iliyopo inalindwa na watanzania na kila kiongozi anayesimama kuhubiri jambo hilo," alisema.

Alisema kuwa iwapo vyombo vya dola vinashindwa kuwachukulia hatua wale wanaoonekana kuvuruga amani basi vyombo hivyo vitakuwa vimeshindwa kufanya kazi.

Mtatiro alisema kuwa uzalendo umepotea miongoni mwa watanzania kutokana na ufisadi unaofanywa na wale walioshika dola.
"hivi kweli unaweza kuwahubiria watanzania wawe wazalendo wakati wanaona matendo yanayofanywa na viongozi wao…waziri anakuwa na nyumba ya sh bilioni sita unafikiri watakuelewa kukizungumza uzalendo?" alihoji.

Alisema kuwa uzalendo unaenda na vitendo, hivyo ili kuurudisha ni muhimu viongozi waliopo madarakani wakaanza kujitafakari upya.

Kuhusu makundi, mtatiro alisema kuwa yapo ndani ya chama cha mapinduzi (ccm) na sio katika vyama vya upinzani kwa kuwa wamekuwa wakijitahidi kuyaondoa.

[td="bgcolor: #ffffff"]
[/td]

- kwani cuf ni wapinzani au tawi la ccm?

Le mutuz
 
Safi sana Mtatiro Dr. Slaa ni jembe hata Jk anajua hilo
 
Kwenye vyama kuna watu ambao wanakubalika na watu wote. Mfano asiyemkubali prof lipumba ni mtu ambaye anatakiwa apimwe akili yake. Ukija kwa dakt slaa asiyemkubali atakuwa na matatizo kama ya wale wenye magamba orijino. Sishangai mtatiro kumvulia kofia yake dakt kama vile zitto alipomvulia kofia prof siku ya j mos kwenye kpindi hichohicho
 
Kwanza kabisa Karibu sana JF. Pili Acha upotoshaji mkuu,wengi tulifuatilia mdahalo ule, alichokisema Mtatiro ni kuwa watakuwa tayari kushirikiana na watu potential bila kujali vyama vyao kumtaja Dr Slaa ilikuwa ni mfano tu lakini hakusema watahakikisha wanamshirikisha Dr Slaa kwenye serikali ya CUF.

Nakuunga mkono kwa sababu niliangalia kipindi, jamaa kakuza hili suala kama habari za kwenye magazeti ya udaku.
 
Kwanza kabisa Karibu sana JF. Pili Acha upotoshaji mkuu,wengi tulifuatilia mdahalo ule, alichokisema Mtatiro ni kuwa watakuwa tayari kushirikiana na watu potential bila kujali vyama vyao kumtaja Dr Slaa ilikuwa ni mfano tu lakini hakusema watahakikisha wanamshirikisha Dr Slaa kwenye serikali ya CUF.

Sasa unasema nini na unakataa nini............. Mbona hakumtaja Nape kama mfano!!
 
- kwani cuf ni wapinzani au tawi la ccm?

Le mutuz

Hivi wewe hao waliokuchagua huko kwenye jumuiya ya wazazi wanajisikiaje kwa maandishi kama haya ? Hukustahili , bali ulistahili uwe Dj wa Vigodolo kule Buguruni kwa Mnyamani ! Aibu sana !
 
Sasa unasema nini na unakataa nini............. Mbona hakumtaja Nape kama mfano!!

Mkuu ninachokikataa ni matumizi ya neno "Watahakikisha Dr Slaa anakuwa ni miongoni mwa watu watakaokuwa katika serikali ya CUF"
 
Hivi haya Majoho ya graduation yatachezewa mpaka lini?Kama watu wanaopewa majoho ndiyo wa aina hii naomba kupata mwongozo "Inawezekana kurudisha cheti Chuo Kikuu cha Umma nilichosoma hapa nchini ili dhambi hii ya kuandika ----- isi nijumishe na huyu na huyu W.J.M?"Naomba mwongozo tafadhali
 
Back
Top Bottom