Mtatiro amkubali Slaa

Mtatiro amkubali Slaa

Safi sana Mtatiro Dr. Slaa ni jembe hata Jk anajua hilo
yes na kumhakikishia hilo tangu JK aingie madarakani hayawahi -- narudia tena hajawahi kutoa kebehi / dharau ya aina yoyote kwa DR. Slaa - he knows!!! -- our next president. najua nape na rafiki yake mwigilu wananuna sana ila ni sisi watanzania ndiyo tumeamua kumpa nchi 2015.
 
Kwanza kabisa Karibu sana JF. Pili Acha upotoshaji mkuu,wengi tulifuatilia mdahalo ule, alichokisema Mtatiro ni kuwa watakuwa tayari kushirikiana na watu potential bila kujali vyama vyao kumtaja Dr Slaa ilikuwa ni mfano tu lakini hakusema watahakikisha wanamshirikisha Dr Slaa kwenye serikali ya CUF.

Sasa umeongea nini na mwenye mada kasena nini?
Ni saw 1+2=3-0.
 
We gamba KIM DARDASH, muwahi Nepi lumumba akupe posho yako kwa kuchangia hii post
 
Inafurahisha mtu unapokiri kufurahishwa au kukubali kitu, kama kweli Mtatiro alikubali kuwa Dr ni mtu safi nampongeza, maana najua hata CCM wapo wanaokubali kuwa Slaa ndio hasa anafaa kuongoza hii Nchi kwa sasa ila kwa kuogopa kuvuliwa uanachama na AC zao kutoingia tena hela za kifisadi basi inabidi wajikamue hivyo hivyo kumtukana Dr Slaa, unafiki ni mbaya sana hasa unapochanganyika na njaa (mfano Nape), huyu kijana ilibidi ajiunge na vijana wenzake kulilia mali za Nchi hii na kutetea Watanzania wanyonge lkn yeye anakwenda tofauti na kutetea uharibifu wa Nchi yetu unaofanywa na CCM.

Ila tusishangae kwani akili za kipambe ndivyo zinavyofanya kazi hasa ukikumbuka kule South Africa weusi walivyokuwa wanawabadilikia weusi wenzao ili tu kushibisha matumbo yao.
 
tusishangilie hili, tujadili kwa mapana na marefu, au tumlishe maneno  ANAMKUBALI SLAA au ANAIKUBALI CDM, je? mh SLAA ana nguvu kuliko CDM au CDM ina nguvu kuliko MH SLAA, ? maana kwetu neno usaliti liko karibu saana kulitamka kuliko kulifanyia uchunguzi tukio lililotokea. leo hii CUF na CDM vyote ni vyama vya upinzani kwa sasa kikojawapo kikifanikiwa kuchukua nchi.kingine bado kitakuwa chama cha upinzani. yule kiongozi atakayeteuliwa ili ashiriki kwenye serikali hataitwa MSALITI ? vinginevyo chama chote kiungane na chama tawala kuunda serikali mnakumbuka lugha yetu tutawaita.........B .hivyo tusifie sera za chama .kuliko kusifia mtu.
 
Mtatiro kama unasoma hapa utauona unafiki wa hawa watu, walikuwa wanakuponda kila leo humu, vile umemtaja babu wamekuona wa maana. Ntakukumbusha siku ukiwapa ukweli watakapokushambulia.
 
Kwanza kabisa Karibu sana JF. Pili Acha upotoshaji mkuu,wengi tulifuatilia mdahalo ule, alichokisema Mtatiro ni kuwa watakuwa tayari kushirikiana na watu potential bila kujali vyama vyao kumtaja Dr Slaa ilikuwa ni mfano tu lakini hakusema watahakikisha wanamshirikisha Dr Slaa kwenye serikali ya CUF.

mkuu ningependa ulikanushe gazeti nijuavyo mimi ni kwamba mleta mada amekopi kutoka kwenye gazeti moja la leo mwenyewe pia nimesikia limelipoti hicho kitu
 
tusishangilie hili, tujadili kwa mapana na marefu, au tumlishe maneno  ANAMKUBALI SLAA au ANAIKUBALI CDM, je? mh SLAA ana nguvu kuliko CDM au CDM ina nguvu kuliko MH SLAA, ? maana kwetu neno usaliti liko karibu saana kulitamka kuliko kulifanyia uchunguzi tukio lililotokea. leo hii CUF na CDM vyote ni vyama vya upinzani kwa sasa kikojawapo kikifanikiwa kuchukua nchi.kingine bado kitakuwa chama cha upinzani. yule kiongozi atakayeteuliwa ili ashiriki kwenye serikali hataitwa MSALITI ? vinginevyo chama chote kiungane na chama tawala kuunda serikali mnakumbuka lugha yetu tutawaita.........B .hivyo tusifie sera za chama .kuliko kusifia mtu.

rejea hapo nyekundu....chama ni imara na ni maarufu lakini kinajengwa kutokana na uadilifu wa viongozi wake waadilifu(Dr. Slaa, mbowe, mnyika, lisu, n.k ) so kuna sifa binafsi zinazobeba mantiki ya ubora wa chama husika ila sifa hiyo sharti iende na sifa ya chama na ndicho ninachokiona kwa mh. rais dr. slaa na si vinginevyo
 
Mtatiro kama unasoma hapa utauona unafiki wa hawa watu, walikuwa wanakuponda kila leo humu, vile umemtaja babu wamekuona wa maana. Ntakukumbusha siku ukiwapa ukweli watakapokushambulia.

wewe kijana acha unafiki wako...acha kutumikia tumbo wanao watakuja kukulaani milele....mtu anasifiwa kwa jema lake, ustaraabu wake,uzalendo wake,ustahimilivu wake kama mtatiro though atakuwa na mapungufu yake na anasimamia ukweli nimemkubali, sio wewe unayeingia hapa kwa lengo moja tu lisilobadilika kuishambulia CDM tu...........
 
rejea hapo nyekundu....chama ni imara na ni maarufu lakini kinajengwa kutokana na uadilifu wa viongozi wake waadilifu(Dr. Slaa, mbowe, mnyika, lisu, n.k ) so kuna sifa binafsi zinazobeba mantiki ya ubora wa chama husika ila sifa hiyo sharti iende na sifa ya chama na ndicho ninachokiona kwa mh. rais dr. slaa na si vinginevyo
una maana viongozi wa CDM kwa umoja wao wanajenga chama chenye nguvu. ambacho nacho kina mtoa mtu mmoja ambaye ana nguvu umempa urais ,dr slaa una maanisha hivyo.
 
mkuu ningependa ulikanushe gazeti nijuavyo mimi ni kwamba mleta mada amekopi kutoka kwenye gazeti moja la leo mwenyewe pia nimesikia limelipoti hicho kitu

Mkuu mimi sijaliona hilo gazeti na pia sijui nitumie utaratibu gani kulikanusha gazeti hilo!Nadhani nipo sahihi kumkanusha mleta mada maana yeye kaileta kama vile yeye ndiyo chanzo cha upotoshaji huu, hajalinukuu gazeti ulisemalo mkuu wangu.
 
Huyu dogo tangu alipokua chuo, alipendeza sana angeingia kwenye harakati za CDM. HAPO CUF YUPO KAMA AJIRA TU.
 
ua viongozi na maanwa CDM kwa umoja wao wanajenga chama chenye nguvu. ambacho nacho kina mtoa mtu mmoja ambaye ana nguvu umempa urais ,dr slaa una maanisha hivyo.

rejea nyekundu= jibu-ni jibu ni ndio maana umoja ni nguvu kwa wao kufanya kazi kama timu wanajenga chma chenye nguvu na imara .bluu=jibu ni ndio chama chenye nguvu kinamtoa kiongozi imara wa kupeperusha bendera ya urais ambaye ni dr. slaa amaye kiukweli mi kama mimi nampenda na ktk hali ya kawaida ukiangalia bila malice utaona walio wengi wanampa sifa na nafasi japo chama kinaweza kuamua vinginevyo........sabababu za mimi kumpam urais moja ndiye mgombea pekee aliyepata kunivutia na mpaka leo napenda pia apeperushe bendera,pili ni mtu pekee inayesemekekana ni mpinzani wa kwanza kushinda urais tangu nchi ipate uhuru na kufanyiwa hila na hakudai kwa nguvu(busara) ,tatu hakurupuki na mtu mwenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu........n.k
 
Mtatiro.JPG
NAIBU Katibu Mkuu (Bara) wa Chama cha Wananchi (CUF), Mtatiro Julius, amesema kuwa chama hicho kikifanikiwa kushika dola kitahakikisha kinashirikiana na watu safi akiwemo Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.
Akizungumza katika kipindi cha ‘Tuongee Asubuhi’ kinachorushwa na televisheni ya Star tv, Mtatiro alisema chama hicho kipo tayari kuhakikisha wanakuwa na lengo moja la kuijenga nchi kwa kushirikiana na viongozi waadilifu.
Mtatiro, alisema chama hicho kimejiwekea malengo na kipo tayari kuongoza dola pamoja na kushirikisha watu safi ambao watakuwa wakisimamia vema utekelezaji na kuwaletea Watanzania maendeleo.
Alisema ni muhimu Watanzania wakapata dira ya taifa itakayowaongoza na kuonesha wanapotaka kuelekea.
Kuhusu vyama vya upinzani kuwa chanzo cha kuvuruga amani, Mtatiro, alisema vyama hivyo havifanyi kazi ya kushawishi Watanzania waharibu amani ya nchi na kama wapo wanaofanya hivyo wanapaswa kuchukuliwa hatua.
Alisema kuwa amani iliyopo inalindwa na Watanzania wenyewe, hasa kupitia viongozi ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhubiri suala hilo.
“Sio kweli CCM inalinda amani ya nchi…amani iliyopo inalindwa na Watanzania na kila kiongozi anayesimama kuhubiri jambo hilo,” alisema.
Alisema kuwa iwapo vyombo vya dola vinashindwa kuwachukulia hatua wale wanaoonekana kuvuruga amani basi vyombo hivyo vitakuwa vimeshindwa kufanya kazi.
Mtatiro alisema kuwa uzalendo umepotea miongoni mwa Watanzania kutokana na ufisadi unaofanywa na wale walioshika dola.
“Hivi kweli unaweza kuwahubiria Watanzania wawe wazalendo wakati wanaona matendo yanayofanywa na viongozi wao…waziri anakuwa na nyumba ya sh bilioni sita unafikiri watakuelewa kukizungumza uzalendo?” alihoji.
Alisema kuwa uzalendo unaenda na vitendo, hivyo ili kuurudisha ni muhimu viongozi waliopo madarakani wakaanza kujitafakari upya.
Kuhusu makundi, Mtatiro alisema kuwa yapo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sio katika vyama vya upinzani kwa kuwa wamekuwa wakijitahidi kuyaondoa.

[TD="bgcolor: #ffffff"]
NAIBU Katibu Mkuu wa Cuf Mtatiro Julius

na Betty Kangonga

[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"] [/TD]
 
Ameanza kudandia migongo ya watu ili ajikweze kisiasa. Angeongelea wale waadilifu waliopo CCM tungemuelewa, maana CUF na CCM havitengamani.
 
so far, CCM wote wanamlilia Slaa arudi CCM ndio maana wanamlipia kadi yake ya uanachama huko. Wanajua Dr Slaa ndio jembe pekee linaloifaa nchi kwenye kile kiti kikubwa cha magogoni. Lakini wasemeje sasa zaidi ya kuunyaunya?
 
Back
Top Bottom