Mtatifikolo Isimani: Kuendeleza Miradi ya Lukuvi

Mtatifikolo Isimani: Kuendeleza Miradi ya Lukuvi

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
602
Reaction score
551
MTATIFIKOLO: NITAENDELEZA YOTE YALIYOACHWA NA HAYATI WILLIAM LUKUVI.

Mgombea Ubunge Jimbo la Isimani Ndg. Emmanuela Mtatifikolo ameendelea na kampeni kuelekea Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Isimani katika Kata ya Malengamakali na kuzungumza na wananchi wa Vijiji vya Iguruba, Makadupa, Mgodini, Isaka, Nyakavangala, Mkulula na Usolanga kuomba ridhaa ya kura za kishindo Kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) siku ya Uchaguzi Juni 1, 2026.

Aidha Mtatifikolo ameahidi kuwahudumia Wananchi hao Kwa moyo wote na kuendeleza yale yote yaliyoachwa na mtangulizi wake Hayati Mheshimiwa William Lukuvi.

Hata hivyo ameeleza kuwa Vipaumbele vyake ni Kushirikiana zaidi na Wananchi wa Jimbo la Isimani Kwa rika zote, huku akisisitiza kuendelea na moto ule ule katika kumalizia na kutekeleza miradi yote ya kimaendeleo katika Jimbo la Isimani ikiwemo Ujenzi wa Bwawa la Umwagiliaji Kwa ajili ya Kilimo na Ufugaji, Zahanati Kwa Kata ambazo bado, Umaliziaji Barabara, Uwezeshaji wa vijana, wanamama pamoja na wazee Ili kuleta Maendeleo kwa wana Isimani wote.
IMG-20260515-WA0053.jpg
 
Back
Top Bottom