Pole kwa sasa unamaumivu makali na hasira moyoni. Tulia omba Mungu vuta subira. Jipe moyo jitie nguvu usimtafute tena huyo mpenzi wako. Kama una mtoto lea mwanao bila msaada wake kama hujazaa na hii utaweza iwapo utafanya kazi kwa bidii. Kasi yotote ile mradi si kujiuza au haramu ili ulee mwanao bila kumtegemea. Jipe muda walau wa mwaka mmoja au miwili kabla hujaingia mahusiano mengine. Waweza kuwa na marafiki wa kiume kwa kipindi hicho ila uwe makini wasiwe wapenzi la huwezi kuwa na rafiki wa kiume bila kuwa wapenzi basi uwe na marafiki wa kike tuu au uwe kimwenyewe mwenyewe hadi utakapokuwa tayari kuingia kwenye mahusiano mapya.
Muhimu ujipende jitunze jithamini usikubali mtu akirudishe nyuma au kukuumiza kwa mawazo hasi.
Pole sana na kila la kheri, kwa asili yetu sisi wanawake lia weeeh tena kwa nguvu hadi hasira yako iishe kisha mtoe akilini mwako na songa mbele.
Ukifanya hivi nakwambia utang'aa na kupendeza upyaa hata kama unaogea mbuni na kupata rays moyo wako uwe meupeee na mwepesi usishikilie mtu hukoo.
Kila la kheri mama.