Mtanzania Raia wa Marekani anaweza kurithi mali zilizopo Tanzania?

Hapa bongo hatuna uraia pacha kwa hiyo ukichukua uraia wa Marekani au nchi yoyote ile, automatically unakuwa umeukana uraia wa Tanzania.

Hivyo kama wewe si raia wa Tanzania utakuwa huna uwezo wa kumiliki ardhi (nyumba, mashamba, kiwanja n.k) ISIPOKUWA utaweza miliki kama muwekezaji tu. Yaani hiyo ardhi itakuwa inamilikiwa na TIC na wewe unakuwa kama mpangaji tu.

Kwa kumalizia huyo ndugu yako unayemuita Mtanzania raia wa Marekani hata weza kurithi hati miliki za mirathi yenye uhusiano na ardhi. Ila atapata mkwanja utokanao na kuuzwa kwa mali za mirathi ihusuyo ardhi. Period.
 
Kwa sheria za uraia na sheria za ardhi ni ngumu sana.Ila kama ni mali ambazo ni substancial inawezekana ila kwa kuuzunguka mkono wa sheria.
 
Hatuna uraia pacha... Labda umiliki kama muekezaji. ILA KWA UBOVU WA CCM WEWE NJOO NA JINA LA UKOO NA VIPESA KIDUCHU UTARITHI MALI ZA BABU YAKO.
 
Mtoa mada anawaza Mali za wazazi tu
Juma1967 imebidi nicheke kidogo umenifurahisha
Mimi niko fit sana pia natoka lile kabila ambalo huwa hatushobokei kutegemea urithi wa baba yako sisi kwetu hata kama baba yako ana mali kiasi gani na wewe umuonyeshe ni mwanamme kama yeye unatafuta chako vya kwake ni yeye na mkewe ambaye ni mama yangu.Endapo ikitokea akakurithisha inakuwa kama nyongeza tu hapo heshima inakuwepo toka kwa mzazi wako kama bado yuko hai.Mimi sitokei lile kabila ambalo watu wanaanza kugombea baba akiwa bado kitandani anaugua redio hata na TV achilia mbali kinyumba cha udogo kisicho hata na choo cha maana nje.
 
Anataka kudhurumu mali za ndugu yake aliyekuwa Marekani!!
Mimi niko fit sana sisi tunajua kutafuta bro ni kweli alinituma niulizie maana ukweli tayari ana viwanja vyake huku sasa yuko kule kakaa miaka30 anataka kurudi bongo.home is best.
 
Kuna Stori ya mteja wangu inaumiza Sana.
Ndugu zake wa kuzaliwa pamoja wanataka kumdhukumu Mali zake Kisa kaenda kuishi Ulaya mwaka wa 20 huu.

Yaani kuna Ndugu Wana roho mbaya Sana.

Mtu Kama mmezaliwa wote akaachiwa Urithi au anamali zake huku Naye anaishi Ulaya au nje ya nchi ataendelea kubaki kuwa Ndugu yako.

Uroho wa Mali usikufanye umdhulumu mwenzako, Kule kaenda kutafuta.
Wakati mwingine kuna Mazingira ya kuukana Uraia wa nchi yako ili update Baadhi ya fursa za nchi mpya
 
Hapa bongo hatuna uraia pacha kwa hiyo ukichukua uraia wa Marekani au nchi yoyote ile, automatically unakuwa umeukana uraia wa Tanzania.

Hivyo kama wewe si raia wa Tanzania utakuwa huna uwezo wa kumiliki ardhi (nyumba, mashamba, kiwanja n.k) ISIPOKUWA utaweza miliki kama muwekezaji tu. Yaani hiyo ardhi itakuwa inamilikiwa na TIC na wewe unakuwa kama mpangaji tu.

Kwa kumalizia huyo ndugu yako unayemuita Mtanzania raia wa Marekani hata weza kurithi hati miliki za mirathi yenye uhusiano na ardhi. Ila atapata mkwanja utokanao na kuuzwa kwa mali za mirathi ihusuyo ardhi. Period.
Sio tanzania wageni kibao wanamiliki ardhi bila shida...nliuza shamba langu arusha mateves kwa mzungu mkataba aliandika jina lake....mkewe ni mtanzania ila hakumuweka
 
Back
Top Bottom