Mtanzania mwenzetu yupo live ITV, tumsikilize!

TeamLowassa

JF-Expert Member
Nov 30, 2013
1,495
936
Mimi simjui jina lake but hope anaitwa michael

Anazaungumzia uchumi kipindi cha mwalimu

Anasema sasa hivi mtu ukiwa na miaka 35 huna hata kitanda, wakati wa mwalimu miaka 22 ni mtu anajitegemea

Viongozi wetu wamekosa maarifa hawana uweledi!

Kipindi cha mwalimu kulikuwa na mabasi ya maghorofa

Sasa hv wasomi ni wabaya kuliko wasiosoma, wasomi wanawaibia wasiosoma!

Kipindi cha mwalimu hakuna kubanana kwenye daladala

Mwalimu alikuwa anataka tujitegemee kwanza, kabla hatukuweza kufanya hilo tunaanza kuzalisha matajiri

Tumeacha misingi yetu ya kitaifa. Huwezi kuuza viwanda halafu ukawa salama

Mwalimu alikuwa na madkatari bingwa wanne tu mmoja kijana alifariki akabakiwa na watatu. Leo wapo maelfu kwa maelfu kwa maelfu lakini wagonjwa wanalala chini

Mwalimu alikuwa na mainjinia 12 hakuna mwanafunzi aliekaa chini, leo wapo mainjia maelfu lakini wanafunzi wanakaa chini

Leo viongozi wananunua gari moja milioni 250 ambayo inatosha hospitali ya mwananyamala, lakini wao wanatembelea

Mwalimu alifanya Tanzania kama chuo cha marais wote. Marais zaidi ya 12 walikimbilia tanzania. Leo rais gani anakimbilia hapa

Mwalimu alisema tusichimbe madini kwanza hadi watoto wetu wapate elimu. Leo wamesomeshwa wanaiba kila kitu

Nenda kapige kura kwa jazba kwa hasira kubwa, kwa morali kama ya kimasai..
 
Mimi simjui jina lake but hope anaitwa michael

Anazaungumzia uchumi kipindi cha elimu

Anasema sasa hivi mtu ukiwa na miaka 35 huna hata kitanda, wakati wa mwalimu miaka 22 ni mtu anajitegemea

Viongozi wetu wamekosa maarifa hawana uweledi!

Kipindi cha mwalimu kulikuwa na mabasi ya maghorofa

Endelea kutupa uptodates tafadhali
 
Huyo aliye na miaka 35 bila kitanda atakuwa na tatizo lake binafsi.

Naona unajisimanga mwenyewe..
Na hicho kitengo chenu cha LB7 mwisho oct. 24 sasa sina uhakika sana kama ulikuwa unatunza hata nauli za kurudia Sitimbi.
 
Kipindi cha mwalimu dawa.zilikuwa bure hakuna aliyenunua, tanzania ni nchi ya 3 kwa misitu africa, lakini wanafunzi hawana madawati, hospitali wanalala chini
 
Jamaa anaongea kwa jazba huyo, mara anaweza akamchapa gondwin gondwe kofi aisee, ana uchungu hasa na nchi hii
 
Yeah, ila ameongea facts sana aisee

Unajua ukishatoka nje ya tz ukaenda nchi za watu ndo utaona jinsi tz tilivyo nyuma, inauma sana unajua mkuu, mie mtazamo wangu naona wale wanaooshabikia kijani kwanza ni maslahi yao, kingine hawajabatika kutoka nje ya nchi, inauma sana mkuu na tuna kila kitu
 
-Bora Ujinga usio na Madhara kuliko Elimu isiyo na Faiza.
-Wasomi Wetu wa sasa Majanga afadhali mara 100 Chief Mangungo aliyekuwa hajui kusoma wala kuandika.
 
Mwalimu alikuwa na mainjinia 12 hakuna mwanafunzi aliekaa chini, leo wapo mainjia maelfu lakini wanafunzi wanakaa chini

mara nyingine mwalimu anapata sifa asizostahili, kwa tulioishi kipindi chake tumeyaishi mengi magumu, hususan kuanzia miaka ya 70+ sera za nje za huyu mzee zilikua kama za rasta kila mtu ndugu yake watoto wake wakisoma chini ya miembe, hospitali zikiwa wilayani, kwenda songea siku 10 njiani...
 
Anasema sasa hivi mtu ukiwa na miaka 35 huna hata kitanda, wakati wa mwalimu miaka 22 ni mtu anajitegemea

Hilo tu ndio kasema mkumbushe wakati wa muwalimu kila kitu kilikuwa shida kupata ili ukipate lazima upange foleni si chini ya ya masaa 56 ndio ukipate.
Kuanzia chakula hadi mafita ya petoli au disel.
Magari binafi marufuku kitembea jumamosi na j2.
 
Back
Top Bottom