Mtanzania mahakamani uingereza

Injinia

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
849
26
Mtanzania mwenye asili ya Asia, Safina Khan, amefikishwa mahakamani hii leo huku Uingereza kwa mashtaka ya 'human trafficking' - alimleta mama wa miaka 47 kuja kumsaidia kazi za nyumbani lakini mama huyo anafanyishwa kazi kwa masaa mengi bila mapumziko.

Hii ni kwa mujibu wa Sky News Radio jioni hii.

Hivi, hizi kesi za waTanzania wanaoleta wafanyakazi wa ndani chanzo ni kipi kati ya hivi:
1. Waajiri wanawarubuni kuwa wakifika huku watalipwa mshahara kwa viwango vya Uingereza
2. Hao wafanyakazi hawajali mradi wameambiwa ni Ulaya/ Uingereza
3. Hao wafanyakazi wakifika huku wanakuwa wajanja na kufungua mashtaka hata kama si kweli
4. Ni kweli waajiri wanawaonea wafanyakazi wa ndani na kuwatumia kama watumwa?
 
Back
Top Bottom