Mtanzania apora Sh. bilioni 400 za Aga Khan

Ha! Ha! Ha!

Umenikumbusha wale jamaa wa security group waliokimbia na hela wakaishia kununua viwanja kisemvule na magari used

Mwisho wa siku wakakamatwa km kuku
Ndio nature ya wezi wa kibongo🤣🤣🤣
 
Nimesoma hapo kwa huyo jamaa wa Nairobi mwenye hiyo kampuni ambayo imethibitika haijasajiliwa Kenya (GR Construction Limited) nime- conclude hao Aga Khan nao wanastahili lawama, haiwezekani wafanye kazi na kampuni isiyosajiliwa, hapa nahisi baadhi ya maofisa wake watakuwa wanahusika na huo mchezo mchafu.

Lakini pia, kitendo cha FBI kutilia shaka nyendo za huyo jamaa mpaka waanze kumtafuta inaonesha jinsi taasisi zetu za kiuchunguzi hapa ndani zilivyolala, au inawezekana nao ni sehemu ya hilo dili kuna kitu walipewa wakafungwa midomo.

Nasema hivi kwasababu mabenki yetu mara nyingi yamekuwa yakitoa taarifa za wateja wao kwa serikali, na hao Baclays wana tawi Tz, sasa vipi kwa huyo muhusika ishindikane kumgundua mapema? hapa wafanyakazi wa hiyo benki wanatakiwa kujibu maswali.
Nimesoma maelezo yote, sijaona mahali popote vyombo vyetu vya dola kama Polisi ikihusika kuchunguza, kukamata au kutoa taarifa.
Sijui tunakwama wapi?
 
Nyaraka za akaunti zilizoko Benki ya Barclays zinazoonyesha mmiliki wake ni Mtanzania – kwa miaka mitatu mfululizo, zimetumika kutakatisha zaidi ya Sh. bilioni 400, fedha zilizokwapuliwa kutoka Taasisi ya Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), uchunguzi umethibitisha.

Kiasi hiki ambacho ni zaidi Dola za Marekani milioni 176, zinatosha kujenga vyumba vya madarasa ya kisasa 10,000 yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 450,000 wa shule za sekondari nchini – ikiwa kila darasa litabeba wanafunzi 45. Darasa la kisasa lenye samani zake linaweza kufikia Sh. milioni 40,000.

Pia fedha hizi ni sawa na mapato ya serikali kwenye mauzo ya makaa ya mawe Ruvuma kwa kipindi cha miaka mitatu (2017-2020) ambako zaidi ya vijana 700 wameajiriwa. Ni sawa na gharama za kujenga barabara ya kilomita 270 kwa kiwango cha lami, ikiwa kilometa moja itajengwa kwa Sh. bilioni 1.5.

Hapa maelezo haya yameirefusha makala wakati pesa hizi si za waTanzania bali jamaa ameitumia Tanzania na nchi kibao kutakatisha fedha.

Uhalifu unaovuka mipaka ya nchi yaani Mambo ya kimataifa, ndiyo maana Idara ya Upelelezi Marekani FBI wanataka kufahamu wanufaika wa fedha hizi ni kina nani na kwa manufaa gani . Je ni ya kufadhili au kuwezesha manunuzi ya silaha au ugaidi au kujitengenezea utajiri kupitia wizi wa kimataifa.
 
Kwa jinsi nilivo soma na kuelewa kumbe hizi pesa sio za agakhan .......hizi pesa ni za raia flani wapuuuzi ambao wameamua kumpa agakhan ili awe tajili huku yenyewe yakibaki masikini Kwa kigezo cha kusaidia wengine masikini uku yeye anakuwa tajili na familia yake............nasema hivi HEKO KWA MBONGO ULIYEJIZOLEA HUO UKWASI MAANA HATA WEWE UNA AKILI KAMA WAO...........
 
Pamoja na kwamba maelezo ya awali ya benki yanakanganya, lakini inawezekana siku alipokwenda kutoa fedha, dirishani, aliitwa na uongozi na akaahidi kurejea siku inayofuata.

Lakini hakutokea na hakuna traces. Akapotea. Kama unavyosema, ni mchezo unaohusisha idadi kubwa ya watu wakiwamo maofisa wa benki na hata taasisi
Kutoa fedha dirishani
 
Anakupa 0.15% ya hela aliyokwapua kama rushwa nadhan utafunga domo. Unafikiri hao waliochanganya hiyo habari mpaka haieleweki walipewa nini? Hahahahha

Mtu wamemhoji ati wakaagana atarudi tena mpaka leo et hawajui alipo.

Ila watu wana visa..ati u designer umemshinda
 
Agakhan gan Kwanza jaman,sijaelewa n hii hospital au?

Mambo n mengi muda mchache
 
Hapo ni crew ya masela wanaofanya au walifanya kazi Agakhan wametengeneza account nyingine halafu funds zinakua diverted kwenda kwenye account yao mpya badala ya account halisi. Kwahiyo Agakhan wao hawajakwapuliwa pesa kwenye accounts zao ila pesa zimepigwa juu kwa juu zikaelekezwa kwingine tena pesa nyingi inakua kutoka kwa wafadhili wapya ambao wanakua hawajui account ipi ni ipi maana zote zinakua na jina moja.
 
Back
Top Bottom