Mtanzania aliyeuawa Los Angeles-Caroline Mmari kuzikwa kesho Dar. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtanzania aliyeuawa Los Angeles-Caroline Mmari kuzikwa kesho Dar.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tusker Bariiiidi, Jul 15, 2010.

 1. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,753
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mwili wa Mtanzania Caroline Tom Mmari ambaye aliripotiwa kupotea May 20.2010,na kupatikana akiwa amekufa huku mwili wake ukiwa umefichwa/zikwa nyuma ya nyumba aliyokuwa akiishi Jijini Los Angeles,unatarajiwa kuzikwa kesho July 16.2010.

  Taarifa nilizozipata kutoka kwa ndugu wa karibu na Marehemu zinasema kutakuwa na Ibada takatifu ya kumwombea marehemu itafanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Usharika wa Azania Front kuanzia saa 3 na nusu asubuhi (Saa za Tanzania) na Maziko kufanyika katika makaburi ya Kinondoni saa 6 na nusu Mchana (Saa za Tanzania).

  Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe.
   
 2. JS

  JS JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  RIP Caroline
   
 3. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  rip dear sister,

  utakumbukuwa daima kwa ucharming wako!
   
 4. P

  Penguine JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2010
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Ipo haja ya kutafakari, kwa nini vijana wenzetu waliowengi ( hapa natafakari juu ya maisha ya ndugu zetu, baada ya kusikia na kuona unyama wa aina hii ukitokea. Kwa mfano, kuna mwanafunzi wetu aliuawa huko india, Mwingine alirushwa ghorofani huko YUKEI mwingine alipondwa kichwa huko RASHIA, e.t.c) mauti yao wakiwa ugaibuni ni kwa njia ya ku- uawa?

  1. Je, tuseme ni unyama tu dhidi ya watu hao?
  2. Je, kuna agenda wanazojiingiza kuzitekeleza nazo zinapelekea hayo yanayowapata/ au,
  3. Ni Bwana tu aliyetoa huamua kutwaa?

  Nafikiri tukitafakari kidogo juu mambo haya matatu, twaweza kuokoa maisha ya waliosalia endapo watatilia maani mantiki ya mijadala yetu na endapo mijadala yenyewe italetwa kwa namna ya kuokoa maisha ya walosalia
   
 5. P

  Penguine JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2010
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Carloline,
  may your soul rest in eternal peace, amen
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Una uhakika kwamba waliowengi wanaokufa ughaibuni wanakufa kwa ku uawa? Una takwimu za kuthibitisha hivyo? Au unasikia sana habari za wanaouawa kuliko nyingine kwa sababu zinakuwa kwenye news sana ?
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  Nini haswa zababu ya kifo chake, je wauaji wamesha kamatwa?
   
 8. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,753
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mkulu Pasco tunaomba msaada najua upo karibu zaidi...
   
 9. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #9
  Jul 15, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Wakati tukimwombea Marehemu Mungu ailaze mahala pema peponi, mimi kwa hakika nina uchungu sana na ndugu zangu walio-stowaway Uuko majuu. Wakati nikiunga mkono harakati za maisha kutafuta, lakini kwa hakika nawaonea huruma sana hawa vijana wanao-hang tu huko majuu. Nimebahatika kuwatembelea baadhi yao, Asia, Ulaya, USA na Austalia, na hakika nikiwaangalia, sioni hata sababu ya kuendelea kuning'nia huko waliko. Wengi wao wanaishi maisha wakiamini wako sahihi kabisa na kwamba bongo ni kama jehanamu, wakati si kweli! Nakubalia kwamba wengi wao ni vijana ambao wako under qualified, std 7 au drop-outs za primary school, forms na six, lakini wako ambao wana brain ambayo wakiirudisha bongo wanaweza excel sana. Kuna ambao walinishangaza sana kwa kusema ati bongo ujambazo mwingi na hawawezi kuishi maisha hayo!

  Ingawaje siyo mahala pa kuongelea hii lakini message lazima iwe delivered kwa watu hawa. Hakuna haja ya kuwa mtumwa wako mwenyewe! Kuna waliopoteza wazazi wao wanashindwa kurudi kwenye misiba; kisa ati visa itapotea au hawatapata visa tena....!!! Hivi kweli inaingia kwenye akili hii?! Kuna wanaobadilisha namba za simu na majina kila wakati kuweza ku-evade system ya huko.

  Jamani, ni utumwa uliopitiza kuning'inia kwenye nchi ambazo si zenu na tena kwa wasi wasi kama panya. hata kama hauko priviledged kusoma, isiwe sababu ya kujitesa na kudhulumu nafsi yako kwa kuendelea kukaa majuu ambako, kwanza hata hiyo sababu ya kuwa huko hatuioni.

  Is good that some have started to come back. Wengine; achana na kuzungukazunguka vichochoroni huko kwa kisingizio cha kazi ambayo tukikuuliza imekufanyia nini, huna jibu mpaka leo. Mbaya ni hii mtu kufa na kutokomea siku kadhaa bila kujulikana na kugundilika baadaye. Si ajabu huyu ndugu zake wamemwona mara ya mwisho miaka kadhaa iliyopita na sasa wanaletewa mauti. Inaweza pia kuwa si hivyo, lakini ujumbe naupeleka kwa wahusika wa hivyo. Poleni sana wafiwa.

  Ukweli ni huo huo, ingawaje unauma sana. Hakuna maneno mbadala hapo.
   
 10. S

  SuperNgekewa Member

  #10
  Jul 15, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhe Kiranga,
  Nchi nyingine akiuawa raia wao mmoja nchi nzima inasisimka - ikiongozwa na Serikali yao. Wewe unataka Watanzania wauawe wangapi ndiyo iwe issue. Kwa kuwa kuna wanaokufa bila kuuawa, unataka wanaouawa kwanza wazidi wanaokufa bila kuuawa ndiyo iwe issue?
   
 11. P

  Penguine JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2010
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180

  Thank you Kanyaafu Nkanwa kwa mtazamo na maoni yako mazuri, though
  am sorry for Kiranga,

  Nashukuru kwa mawazo yako Ndg. Kiranga hata hivyo ningekushauri ulete mijadala ya namna ya kuokoa maisha ya ndugu zetu walosalia huko majuu ama wanao taraji kwenda huko. Ninao uhakika wa ndugu yetu aliyezikwa huko kilimanjaro baada ya kuuawa huko India, ninao uhakika kabisa juu ya ndugu Siza wa Kyela- mbeya aliyepatwa na masahibu kama hayo huko Urusi, na sasa tumeletewa habari ya ndugu Carloline sasa unahitaji nini zaidi? my reserah methodology? my literature review? au?

  Kiranga, achana na ubishi usiojenga pafanye JF mahala pa wanatafakuri na wachangia suluhu kwa matatizo yanayoisibu jamii.


   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Jul 15, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Sikusem kwamba kusiwe na outrage kuuawa Mtanzania, nilichofanya ni kuuliza hizi takwimu za kwamba Watanzania wengi wanaokufa wanauawa .

  No dis kwa wafiwa, kufiwa kunauma.Mimi mwenyewe niko viwanja na naweza kuuawa. Lakini...

  Ni upumbavu kufikiri kwamba utaweza kuzuia kuuawa kwa Watanzania watatu kwa mwaka nje ya nchi. Let's be real. Unataka watu wafanye nini sasa? Watanzania wote warudi bongo? Bongo ndiko hamna kuuana? Unaweza kukimbiia kuuawa viwanja ukauawa na tumbo la kuharisha kwa sababu umekunywa maji machafu ya kisima. Naelewa idea nzima ya precaution, lakini ukiangalia idadi ya Watanzania wote wanaoishi nje, watanzania wote wanaokufa kwa kuuawa kwa mwaka wakiwa watau (so far as presented here) hii ni statistical inevitability.It is bound to happen.What next mnataka kuzuia kufa kabisa?

  Na hizi habari za nchi nzima kusisimka kwa sababu raia wao mmoja kauawa ndiyo zinazoenda kuleta vita za majuha zinazoua mamilioni bila sababu.
   
 13. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Ukitaka kuwanusuru na kifo warudishe wote, halafu wafungie kila mtu chumbani kwake. Uwapatie chakula na huduma nyingine zote. Na hata hapo kuna siku watakufa tu.

  Kuna vitu vingine haviepukiki, watu kuuawa, hususan kama ni watu watatu kwa mwaka, ni moja ya vitu hivi.

  Labda mngekuwa mnajali kweli mngeanza na ku concentrate kuboresha maisha hapo nchini ili watu wanaokwenda nje wawe wamejitakia wenyewe.Currently watu wanalazimika kutoka nje ya nchi na ukishatoka nje hata Polisi wa Masha hawapo huku kusema watakujua na kukita "ndugu".

  Hivi kwa nini tunajitia umajinuni wa kutaka kuzuia statistical inevitabilities wakati tunashindwa hata kupiga kura sensibly hapo nyumbani?
   
 14. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #14
  Jul 15, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  We Kiranga, nani amekwambia analazimika kwenda nje kukimbia hali mbaya Tanzania? Sisi tuko humu humu ndani na tuko happy sana. Wewe kama umelazimika ni kwa sababu yako, la labda hujui hali nzuri ni kitu gani. Na si kweli uko nje kuna life better kuliko bongo kwa Mtanzania. Kw amfano, tukikuuliza wewe hali nzuri uliyonayo baada ya kukimbia unaweza ielezea? Kuna mabwana niliwakuta central Europe, wamekaa pale ten years. Life very misreable. Ukiwauliza, nyie mnafanya nini huku majibu; hali ya maisha bongo ni ngumu bora huku! Niliporudi bongo kuwapelekea zawadi ndugu zao (wazazi) I was shocked and still confused. The essence of good life majuu!
   
 15. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,778
  Likes Received: 20,711
  Trophy Points: 280
  umeona watu wote wanaishi nje ya tz au unatumia image uliyoona kwa hao uliowaona central europe ku-generalize maisha ya watz nje???post yako inaonyesha majungu na kufuatilia maisha ya watu.mind ur business achana na maisha ya watu.
   
 16. Fab

  Fab JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2010
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 763
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bora umempa yake,hata mie alishaanza kunibore....
   
 17. P

  Penguine JF-Expert Member

  #17
  Jul 15, 2010
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Dear Kiranga,
  Sitachoka kukuelimisha katika hili
  Hapo nilipo highlight in red ndipo tunapopataka, hapo umechangia namna ya kunusuru maisha ya wabongo wenzio kwa maelezo kwamba poor social service delivery at the point of origin (if you are materially evidenced that the delivery is really poor because the essence of poor is also relative in perceiving it) ) ni miongoni mwa sababu zinazo wafanya baadhi ya watu kukimbia mahali walipo kwenda mahali pengine (however this might also be a mere expectation for good life at the point of destination) . Hivyo tunapaswa kuboresha huduma hizo pale tunapokuwa. Ukirudi Bongo ama hapohapo ulipo jijali, chemsha maji ya kunywa (kama siyo salama) usijepoteza maisha kwa tumbo la kuhara unaloliogopa, usisubiri serikali kwa kila jambo! usisubiri sana misaada kutoka kwa hao vijana wa Masha unaowasema, ndiyo maan ya kujitegemea.

  Kwa mwanajamii mzuri mtu mmoja kuondoka katika jamii yake kama alivyoondoka dada Carloline ni jambo la kuhuzunisha sana.
  Nasikitika kuona kwamba kwako Ndugu Kiranga lazima yatokee mauaji ya halaiki ndipo unasikitika. Ungependa kusikia watanzania wote waliokuwapo Los Angeles wameuawa ndipo uchangie suluhu kwa tatizo hili, Kiranga ndugu yangu kiranga mbona utu umekutoka sana!

  Jamii zenye kujali maisha ya watu wake huchunguza chanzo cha madhara ya aina yoyote ile yanayotokea kuanzia kwa mtu wao mmoja. Hebu tujadili hoja hii kwa kuanzia na kupotea kwa mwenzetu mmoja tu bila kujali nature ya kifo chake.

  Be careful, maana Utawatiisha hata Ndugu zako wa damu wakisoma mawazo yako na kuona kwamba mmojawao akiuawa it makes neither sorrow nor regret to you kwa sababu statistic ya vifo vinavyokushangaza na kukuhuzunisha haitoshelezwi na kifo cha mtu mmoja ama watatu.

  Labda ili tusije tukakukwaza siku nyingine ebu tujulishe unahitaji watanzania wangapi wafe ndipo ujisikie kutafakari sababu za vifo vyao?

  Nani kakuibia huruma yako Ndg. Kiranga
  Mengine yote uliyaandika (isipokuwa hapo kwenye red highlight) yaweza kuwa ni vielelezo vya namna yako ya kufikiri kuwa chini ya uwezo wa kutafuta suluhu ya challenges za maisha yako ndiyo maana unafikiri kukimbilia ughaibuni ndiyo suluhu ya maisha magumu. Pls never induce that to your siblings! sina mpango wa kutambiana idadi ya viwanja vya majuu ambavyo mimi au wewe tumetembelea kwa sababu mpaka sasa nimeomba Pasi ya nne hapa idara ya uhamiaji DSM kwa sababu pasi 3 za awali zimejaa kwa ajili ya kusafiri hivyo viwanja. maisha ya huko nayo nayafahamu ipasavyo.

  Nomba Mungu akuongoze vema katika kujadili hoja hii hata kama utakuja kwa mara nyingine ukiwa statistically obsessed ndipo uone haja ya kujadili suluhu ya kupunguza mauti zinazotokana na kuuawa kwa wenzio huko ng'ambo.

  karibu tena kama utapenda kwa hoja hii ama hoja zingine.

   
 18. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 521
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  mimi nafikiri suala hapa si kulumbana, nilichomuelewa mheshimiwa ni yeye kutaka kufahamishwa kwa nini hali hii inatokea? nini hasa sababu za msingi zinazofanya hawa watanzania tulioko nje tunapatwa na vifo ktk mazingira ya kutatanisha? we have to debate in a polite way such that however goes through our notions can gain something as JF is looking to be a home of knowledge, kikubwa nafikiri basi hata serikali yetu ingekuwa inajitahidi kutoa feedback zinazoeleweka juu ya hivi vifo ili watu waelewe sababu, hakuna anayeweza kuzuia maamuzi ya mungu na kila nafsi itaonja mauti, tatizo la hawa wenzetu hawakukutwa wamekufa KANISANI wala MSIKITINI, ni vifo vinavyoashiria kuwepo na vitendo vya kikatili, basi watu wafahamishwe ili sisi tulioko huku nje tuwe na amani.
   
 19. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #19
  Jul 15, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mnh hata bongo watu wanauwawa...

  infact majambazi yamekuwa tishio sasa...

  haya mambo ya kujaribu kupaint picture hapa kuwa 'nje' tu ndiko kunakotokea hivi vifo vye 'utatanishi' tu...will lead us to nowhere!:mad:
   
 20. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #20
  Jul 15, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Vifo vya kutatanisha ndo sehemu ya maisha ya ughaibuni...unapokuwa kwenye nchi ambayo jeshi la polisi limetulia kwenye kazi na upelelezi wao unaendeshwa kisasa zaidi basi unakuwa na wahalifu ambao nao wanakuwa na njia zao za kutatanisha!

  Sidhani kama kuna muhalifu ambaye angependa kufanya kosa na kukamatwa tu...yaani it's like every other mhalifu out there will want to get a way with whatever crime s/he commits kwa hiyo hata njia zao ni za kuhakikisha kuwa hawaachi vidhibiti vyovyote vitakavyosababisha wao kutiwa hatiani kirahisi!

  Mauaji haya ya Caroline ni ya kawaida tu huku Marekani...akili za watu huku mmh...kazi kweli kweli!
   
Loading...