Mtanzania aliyefungwa gerezani China, ampigia simu Millard Ayo akiwa ndani ya gereza...

Ombudsman

JF-Expert Member
Apr 18, 2012
3,565
3,730
Mtanzania aliyefungwa gerezani China, ampigia simu Millard Ayo akiwa ndani ya gereza na kuelezea namna alivyokamatwa kwa ishu za dawa za kulevya, maisha wanayoishi gerezani na Idadi ya Watanzania waliofungwa huko.

Katika exclusive interview Mtanzania huyu anasema ‘ Ilikuwa mambo ya madawa, mimi nilikuwa nimetoka Dubai kuja China, jamaa wakaingia katika hoteli na wakatukamata, jumla tulikuwa watu nane ‘

‘Ujue nchi hii mambo ya madawa wanapiga vita mno, kesi ya madawa zina adhabu ya miaka mingi kuliko kesi nyingine yoyote, kama mimi nimepewa miaka kumi na miezi sita ‘

‘Mimi nimefungwa nikiwa na miaka kama 26, nilianza kufanya biashara ya dawa za kulevya nikiwa na miaka kama 18, hawa jamaa wa China ni wabaguzi sana, hivyo unatakiwa uwe kauzu ili kuendana nao sawa‘
 
Kila mfungwa wa kitz aliyefungwa china anampigia cm millard ayo ina maana Ayo ni msemaji wa gov au ???
 
Magereza ya china huwezi fanya ivyo aache kutafuta umaarufu cheap....
 
Amempigia simu,

je amesema nini?
Je amewataja waliombebesha mzigo?
Kama amewataja ni kina nani?

Habari za kutueleza sijui amafungwa 10 years, sijui alianza kuuza unga akiwa na miaka 18, hizo hazitusaidii.

Tunachotaka kujua hao waliombebesha huo unga.
 
Clouds inatisha sana, majuzi magu kupiga simu clouds hatuja kaa vzr mfungwa wa Gerezani naye kampigia simu Millard ayo
 
Kila mfungwa wa kitz aliyefungwa china anampigia cm millard ayo ina maana Ayo ni msemaji wa gov au ???
Kuna tatizo gani kama wanaona huyo mtangazaji ni kijana mwenzao na ana moyo wa kufikisha habari bila kukaa nayo mezani?
 
Nimeisikiliza hiyo audio!! Duh inauma sana!! Miaka kumi bila kumuona mtoto,mke,baba na mama!! Nakumbuka sana namna nilivyotakwa kuigizwa kwenye hii biashara na jamaa mmoja Zanzibar. Nilileta uzi kuhusiana na huu mkasa. Nakumbuka namna jamaa nikiwa nae akipigiwa simu na viongozi wakubwa tu wa serikali kwamba wahi airport kuna mzigo!! Bahati nzuri jamaa alikuwa mlopokaji sana hadi akanitajia. Siku nikipata msaidizi wa karibu na Magufuri basi tamdokeza lkn huyo mtu hata Magufuri hawezi kumgusa isipokuwa atamgusa huyo jamaa yangu. Mungu ni mwema na malipo yapo hapahapa duniani kwani hadi natoka Zanzibar mtoto wa huyo kiongozi alikuwa ashakuwa teja.
 
JK aliwahi kukiri kuwa ana majina ya wauza unga but ten years down the road kamaliza muda wake. Yako wapi yale majina? Kuna nn hadi akaamua kukaa nayo kimya?
 
Back
Top Bottom