Mtanisamehe kwa hili

Mfano mmojawapo ni mimi nachukia gari binafsi japo uwezo wa kununua ninao.
Watanzania walio wengi elimu ya uchumi imewapitia kushoto mtu anaenda kukopa gari kwa manufaa ya kutia kishoka tu na aonekane matawi ya juu ila hasara anazopata ni nyingi ukilinganisha na faida.
Unakuta mtu ananunua gari halafu kimshahara chote kinaisha kwenye kununua mafuta ya gari.
Ndio maana wahindi kwa vile ni watu wa mahesabu wanapanga karibu na kariakoo ili kuepuka hizi gharama akiamka anatembea kwa miguu tu kwenda kazini kwake.
Na kuna wabongo wachache wenye mahesabu hata akinunua gari anatembea nayo umbali mfupi anaipaki kisha anadandia mwendokasi inamsogeza kazini kwake jioni akimaliza kazi anachukua mwendokasi anashuka anapanda gari yake inamsogeza nyumbani kwake kwa hiyo gari haiwezi kumfilisi maana anaitumia kimahesabu tofauti na mtu ambaye anaendesha gari yake kutokea Bunju au Chanika hadi Posta mtu huyu atakuwa anateketeza zaidi ya laki 6 kwa mwezi kwenye mafuta tu.
 
Badala ya kutusema sisi,iambie SIRIKALI yenu iboreshe usafiri wa umma ili kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa na mifoleni isiyo na kichwa wala miguu!
Ungesema serikali ipige marufuku hivi vigari vidogo (mkopo) kwenye barabara kubwa ili kuondoa follen ningekuunga mkono. Ujerumani taifa lililoendelea ila wananchi wengi wanatumia usafiri wa umma.
 
Sahihi,Kuna jamaa anamagari ila anaogopa kuendesha na Wala hajui!
 
de Gunner , kwanza una mingap?.

Okay najua itakuwa chini ya 25. Na ndio Maana unaona una haki ww kupanda daladala na wenye above hapo bas wawe wana magar yao na nyumba zao.

Ila Sio kwamba watu hawatak Maisha Mazuri. Ila wamepambana kwa namna zao na hapo walipo ndio wamefikia.

Najua Lengo sio kuwabeza. Ila Umewashangaa. Kwamba imekuwaje kuwaje. Ila jua tu. Maisha ni fumbo Kubwa.

Ww shemej ako anajimudu. Ila huwez jua kesho yake. Wala kesho yako.

Cha Muhimu ni kupambana.
Uwe na hela au usiwe na hela.

Be humbe Bro.
Life is a Mother Teacher.
 
Maneno Yako ni kichekesho,ila Yana ujumbe wa Kweli!
 
Daah! Hivyo Mkuu we ulipanda dalada for fun hapo hapo gari ya shem ilikuwa mbovu hapo hapo tena hukutaka kupanda uber hapo hapo mwanaume unakosaje M6. Lol

πŸ€”
Kwani what's wrong with that?
Yes, nikifanya for fun maana uber naimudu vizuri tuu si kutaka na sikuwa nawahi sana niendako
 
Do you think people like to be in public transports? Ulisha mwona mtu maarufu au tuseme mtumishi mkubwa wa serekali hata mbunge tu au mfanya biashara mkubwa anahangaika na usafiri wa umma?

Hebu wacheni kujifariji. Hata hao wazee wanaendeshwa bwana
 
Do you think people like to be in public transports? Ulisha mwona mtu maarufu au tuseme mtumishi mkubwa wa serekali hata mbunge tu au mfanya biashara mkubwa anahangaika na usafiri wa umma?

Hebu wacheni kujifariji. Hata hao wazee wanaendeshwa bwana
Kwani SGR na ndege siyo usafiri wa umma? Mbona sgr na ndege sikuizi wanagombea kabisa kupanda ....kilichokosekana kwenye daladala ni usasa tu ...tumia akili kujifunza kwa usafiri wa treni Tanzania...hadi mashirika ya ndege yana hofia kufirisika kwa sababu ya sgr ya kisasa ...pia kuhusu matajiri kuto kupanda usafiri ...wakati mwingine ni usalama wao mfano mawaziri wabunge wanaofia usalama wao kujichanganya sana na raia ni hatati kwao
 
Hii ndo sababu wengi hawatoki.

They live their lives comparing who did that, who came from a wealthy family. Who got a proper childhood.

Hili ni moja wapo ya fungo la kifikra.

Hauwezi kukaa unasema maisha yako yana kuwa controlled na mifumo, wazazi, mazingira au historic background yenu.

Maisha ni rahisi endapo utaukubali uhalisia na kupambana, wengi wamefungwa na dogma ya kudhani they're a product of their circumstances.
. Tuache huu ujinga ndugu zanguni. Kila mtu ana equal chance ya mafanikio.. It's all about making the probability so high that success feels irresistible.
 
kama mvua haijawahi kukunyeshea uwezi jua umuhimu wa mwavuli tunafanya kazi usiku na mchana siyo kwamba ni wavivu ila bahat bado
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…