Mtangazaji wa Sibuka Radio aliyesoma Vichwa vya Habari leo arudi tena Darasani anatia 'Kichefuchefu' Kumsikiliza

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,694
109,133
Tafadhali Mzee wangu na Mmiliki wa Sibuka Media Dk. Nangale na Mkeo Doreen Nyange ( Boss Mwandamizi Sibuka Media ) mmekumbwa na nini Siku hizi hadi mnaajiri Watangazi wa hovyo hovyo na wanaotia Kichefuchefu kuwasikiliza kama huyu wa leo?

Nawaombeni hebu rejeeni Kukagua Academic Credentials za huyo Dada ( Mtangazaji ) wenu wa zamu na aliyesoma Vichwa vya Habari leo Ijumaa tarehe 30 Desemba 2022 kuanzia Saa 2 na Robo hadi Saa 2 na Nusu ili Mjiridhishe nae kama anastahili kuwa Mtangazaji.

Hivi Qualified and Professional Radio Presenter anaweza akawa kweli na Madhaifu haya yafuatayo kama aliyokuwa nayo Yeye leo akiwa anatusomea Vichwa vya Habari vya Magazeti?.

1. Ajari ya Preshisheni Hea
2. Kipa wa Simba SC Benyo Kakolanya
3. Kiungo wa Brazil Pele hafariki Dunia
4. Tanzania Prisons wahaidiwa Haadi wakiifunga Simba SC leo

GENTAMYCINE ningemsamehe ila alipokuja Kunikera zaidi ni pale alipoanza Kuinanga Kiaina Simba SC huku akisema Kimafumbo huku akicheka kuwa Wao ( akimaanisha Yanga SC yake ambayo hata Wewe Boss wake Dk. Nangale nakujua Unaishabikia ) wako ( mko ) juu Kileleni.

Tafadhali Mzee wangu Dk. Nangale na Mmiliki wa Sibuka Media na Mkeo Doreen Nyange hebu tafuteni Watangazi mahiri na siyo hawa Vichefuchefu na wasiojua hata kuficha Mahaba yao ya Kimpira kwa Vilabu vyao wanavyovishabikia.

Mwisho nimalizie kwa kutoa Wito kwa Vyuo vya Uandishi wa Habari Tanzania hebu jitahidini Kutuzalishia Watu ( Waandishi wa Habari ) walio Competent na siyo Vichefuchefu kama huyu ( huyo ) Dada kwani Wanaiabisha Tasnia yangu Mama, Pendwa na inayoheshimika sana hapa Duniani.

GENTAMYCINE ni kama Bahari huwa sikai na Uchafu hivyo lifanyieni Kazi hili kwa manufaa ya Redio yenu na Sisi Wasikilizaji ( Audiences ) wenu vinginevyo mtatupoteza na mtakosa hata Wadhamini ( Advertisers ) na mtaanza kumtafuta Mchawi na kukimbilia kusema Mmerogwa wakati kumbe Mmejiroga wenyewe kutokana na Mapungufu yenu ya Kimsingi.
 
1. Ajari ya Preshisheni Hea
2. Kipa wa Simba SC Benyo Kakolanya
3. Kiungo wa Brazil Pele hafariki Dunia
4. Tanzania Prisons wahaidiwa Haadi wakiifunga Simba SC leo
Huwa ninachefukwa sana ninaposoma habari nikakuta panapotakiwa kutumia "a" pameanza na "Ha" kwa mfano badala ya ahadi pameandikwa hahadi au haadi ....au maneno kama sio badala ya siyo, ndio badala ya ndiyo, baati badala ya bahati...

Kundi lingine ambao wanatakiwa warudishwe darasani wakafunzwe upya usomaji ni polisi hasa RPCs, wengi wao ukiwasikiliza wanaposoma taarifa zao kwa wanahabari kwa kweli ni aibu. Ni kama wanajifunza kusoma
 
Unatibua ugali wa mtu hapoπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Na bahati mbaya Kwake hii Mass Communication and Journalism ndiyo Profession yangu Tukuka 100% na huwa nachukia kuona Mapungufu kama hayo ( haya ) hivyo hapa nataka Tasnia yangu hii pendwa Kupigwa iheshimiwe.
 
Na bahati mbaya Kwake hii Mass Communication and Journalism ndiyo Profession yangu Tukuka 100% na huwa nachukia kuona Mapungufu kama hayo ( haya ) hivyo hapa nataka Tasnia yangu hii pendwa Kupigwa iheshimiwe.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Ndio maana unaweza kuwahandle watu humu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Chini ya uzi huu, JF imeniletea uzi mwingine.

Mtu kaandika kichwa cha uzi "Teknolojia hatari inayoogopwa na waharifu huko China".

Huyu ni mtu asiyejua tofauti ya "wahalifu" na "waharifu".

Zamani tulichekana kwa kutojua Kiingereza.

Tukaja kugundua ni vibaya kuchekana hivyo, kwa sababu Kiingereza si lugha yetu. Wote bado tunajifunza tu. Wengine kwa bado kwa sana, wengine tunajifunza bado hata kama tunakijua kuliko Waingereza wengi.

Rais Mwinyi alisema Kiingereza ni Kiswahili cha dunia.

Akimaanisha kwamba, kama Kiswahili kilivyo "lingua franca", lugha ya biashara, ya Tanzania na Afrika ya Mashariki, Kiingereza ni kugha ya biashara ya dunia.

Nchi yetu inaongeza watu kwa kasi kubwa kuliko inavyoongeza usomi.

Hivyo ni wazi kunaongezeka watu wengi sana wasiojua mambo ya msingi kabisa, hata matamshi, sarufi, herufi, nomino, nyambulisho, fasihi, hata kusima tu kwa ufasaha.

Hata hapa JF tu, napata tabu karibu kila siku, kwa sababu nakutana na watu wengi ambao inaonekana wazi kwamba hawajui kusoma kwa ufasaha na kufuatilia matiki ya lugha.

Hawajui. Ama hawafundishwi au hawafuatilii wao ni suala tofauti, lakini, inainekana tunazidisha idadi ya wajunga nchini. Sikusudii kuwatusi, lakini nakusudia kueleza ujunga kama ukisefu wa ujuzi wa jambo.

Hao waajiri oengine wanaoenda hao wasiojua mambo sana, kwa sababu hao ndio wasiojua kudai haki na mishahara, wanaojua mengi wanadai mengi.

Kwa hivyo, licha ya kwamba kuna wengi wenye kujua mengi, inawezekana wasiojua mengi wakachagukiwa jwa sababu ndio wanaokwenda na bajeti ya kubana matumizi.

Tunapenda zaidi kubana matumizi kuliko kufanya kitu vizuri hqlafu kikaleta ufanisi zaidi na kujenga biashara zaidi.

Mwishowe tunabana matumizi kijinga.

Unaajiri mtu asiyejua lugha, makampuni ya kutangaza biashara yanaona hufai kuoata matangazo. Unakosa biashara kwa kuonekana unabangaiza.

Wakati tofauti ya hela kidogo tu ya kumuajiri mtu anayejua kazi, ingekupeleka ufanye biashara za matangazo mpaka ya kimataifa.

Tunajifunga wenyewe kwa kukisa vision.

Halafu tunatafuta mchawi aliyeturoga na kutuweka kwenye umasikini.
 
Unamshangaa huyo mtangazaji? Shangaa kwa gwiji la soka duniani Pele kuna watangazaji wananakili makosa kwenye jina lake pale palipoandikwa do badala ya dos. Kituko kingine kilikuwa msimu wa kombe la dunia kuna watangazaji na wachambuzi walikuwa wanatamka majina ya wachezaji isivyo hasa yale ya kifaransa, kihispania na kijerumani. Hizi ajira zinatolewa kwa kujuana na undugu bila kujali umahiri wa mtangazaji katika fani hiyo
 
Simiyu ila kwa hapa Dar es Salaam wapo Mwenge Bamaga nyuma ya Hotel Maarufu ya aliyekuwa Hawara Mwandamizi ( Mpango wa Kando ) wa Aliyelala mazima Ziwa Victoria Mkoani Geita.
ila we jamaa!!

Vp na wale wa..

AC Monaco

AC VITA

AC ROMA

Hii ndio bongo nyoso
 
Back
Top Bottom