Mtangazaji wa Kike akabwa kiajabu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtangazaji wa Kike akabwa kiajabu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by HP1, Jul 19, 2012.

 1. HP1

  HP1 JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 3,353
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mtangazaji mmoja wa kike alikabwa kiajabu usiku wa kuamkia leo huko Mbeya. Kwa mujibu wa kipindi cha Morning Talk kinachorushwa na Radio Ebony FM ya mkoani Iringa, Mwanadada huyo alikumbwa na maswahibu akiwa ameenda kufatilia habari juu ya malalamiko ya kiwanja. Akiongea kwa tabu alisema "... ilikuwa majira ya saa nane usiku ambapo nilikutwa na kitu ambacho hakijawahi kunitokea maishani kwangu. Nilikuwa nimelala ghafla nikaanza kusikia kama watu wanatembea juu ya paa. Nilidhani kuwa ninaota, nikashtuka na kukaa kitandani. Niliendelea kusikia hao watu, na nywele zikanisisimka sana. Baadae kukawa kama mtu ananigusa nyuma yangu. Giza lilikuwa nene na mahali nilipofikia hakuna umeme, wanakijiji wapo mbali. Nikaanza kutuma meseji kwa watu ninaowajua, cha kushangaza meseji zikawa zinanirudia. Nikaanza kupiga kelele kuomba msaada. Kwa bahati nzuri ndugu mmoja akapata meseji yangu. Nilianza kukabwa mpaka shingo ikawa inabonyea ila kinachonikaba nashindwa kukishika. Alikuja huyo ndugu aliyepata meseji na kunipeleka kwake. Jamani kweli uchawi upo..."

  Ama kweli ukishangaa ya Musa uayaona ya Firauni!
   
 2. P

  Penguine JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2012
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Watakuwa CHADEMA hao. Ngoja aje Kova atatueleza vizuri. Hata hivyo, pole msana ndg. piga goti ukiomba na kusujudu. Amina.
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  yamekuwa hayo tena, lol.

   
 4. wilbald

  wilbald JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 1,247
  Likes Received: 631
  Trophy Points: 280
  waefeso 6:11 inasema 'Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
   
 5. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  pole ungekemea tu kwa maombi vitu vya disign hii vipo sana
   
 6. Blessed

  Blessed JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 2,488
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  serikal imeamua kujikita ktk tasnia ya maigizo na filamu ikishirikiana na vyombo vya dola ngoja tuone mwisho wake
   
 7. HP1

  HP1 JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 3,353
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kweli maombi yanatakiwa
   
 8. HP1

  HP1 JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 3,353
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Ni tukio la ukweli
   
 9. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkuu let us be serious!
   
 10. Biohazard

  Biohazard JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 2,002
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  Kweli hata mie nimeona hiyo kitu sababu kulikua na watu wamevaa magwanda walikua wanazunguka kwenye nyumba alikuwepo yule mtangazaji.
   
 11. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,325
  Likes Received: 2,624
  Trophy Points: 280
  duh wakati uchawi wa kizungu unatumika kutengeneza simu, intaneti na mitandao, magari......
  uchawi wa kiafrika hutumika kuchezea watu usiku, kunyonga albino na kuchunana ngozi...
   
 12. Biohazard

  Biohazard JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 2,002
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  Ni katika JINA LA YESU BWANA ALIYE MWOKOZI WA MAISHA YETU
   
 13. Mwananzuoni

  Mwananzuoni JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 288
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Ulikuwa Hujui!
   
 14. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Si angekemea tu mapepo yote yangekula kona.
   
 15. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2012
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  pole kwa huyo dada.
   
 16. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #16
  Jul 21, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  She needs to see a psychiatrist.
   
Loading...