Nilichokiona na Kukisikia Kijijini Nyololo, Siku 4 Baada ya Mauaji ya Mwandishi Daud Mwangosi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nilichokiona na Kukisikia Kijijini Nyololo, Siku 4 Baada ya Mauaji ya Mwandishi Daud Mwangosi...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Sep 9, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  IJUMAA alfajiri ya Septemba 7 niliondoka nyumbani Iringa kuelekea Njombe kikazi. Jana yake, alhamisi usiku, Mwandishi Gershom Malegesi wa Redio Ebony FM alinipigia simu kuniomba nishiriki kwa simu kwenye kipindi chake maarufu cha ' Morning Talk'.

  Nikamjibu, kuwa kwa vile nina safari ya Njombe, basi, nikifika kijijini Nyololo, Mufindi, nitasimama na kuongea na wakazi wawili watatu waniambie wanachofikiri juu ya kilichotokea. Kisha Maregesi aniunganishe kwa simu nikiwa hapo Nyololo tuongee redioni. Tukakubaliana.

  Baada ya kutoka Mafinga na kuumaliza msitu wa Sao Hill, nilianza kuiona Nyololo kutoka mlimani. Nilipaki gari yangu takribani nusu kilomita kabla ya kuingia kijijini Nyololo. Nikaanza kutembea kwa miguu kuelekea kijijini bila kushika kamera wala mkoba.

  Sweta nililovaa siku hiyo ra rangi ya zambarau huenda lilinifanya nionekane kama ' wapasua mbao' wengine! Ilinisaidia, maana, kwenye meza ya kwanza ya biashara pale kijijini, niliwakuta akina mama watatu wakisikiliza kwa makini ' Morning Talk' ya Ebony FM. Kulikuwa na watu waliokuwa Nyololo siku ya tukio wakitoa ushuhuda wao studioni.

  Nilimwandikia meseji mtangazaji Malegesi kuwa angeweza kuniunganisha hewani kwa wakati huo. " Kaka, nimeshafika Nyololo!" Nilimwandikia. Naye akanijibu; " Kuna jamaa wanatoa ushuhuda wao studioni, nitakuunganisha baada ya dakika 15".

  Taratibu nami nikajivuta karibu zaidi kwenye meza ile ya biashara ya mboga mboga iliyozungukwa na akina mama waliokuwa wakifuatilia kinachosemwa kuhusu kilichotokea mahali ambapo wao ndipo walipo kwa wakati huo.

  " Kamwene!"- Niliwasalimia kwa Kihehe. Kisha nikajiunga kwenye kusikiliza ' Morning Talk'.

  Niliwasikiliza akina mama wale wakijadiliana pia katika baadhi ya waliyokuwa wakiyasikia. Niliwaona wakitingisha vichwa kukubali baadhi ya yaliyokuwa yakisemwa na mashuhuda. Niliwaona pia wakitingisha vichwa kuyakataa baadhi ya yaliyokuwa yakisemwa na mashuhuda.

  Nikavuta pumzi, kisha nikawauliza; " Mwenzenu napita njia tu, hivi siku ile ya Jumapili ilikuwaje na mlijisikiaje?"

  Nikawaona walivyo na hamu ya kumsimulia ambaye hakuwepo. Nikawasikiliza. Mmoja anasema; hakuwahi hata siku moja kusikia mlio wa bomu. Ilkuwa ni mara yake ya kwanza. Mwingine akaniambia; " Yaani , mimi , niloposikia mabomu tu, nikajifungia ndani na kulala!". Naam, huyu aliugeuza mchana kuwa usiku.

  Akina mama wale wanasema, kuwa usiku ule wa Jumapili walikosa hata hamu ya kula chakula. Hawakula chakula. Walilala kwa mashaka pia.

  Kando ya meza ile nikawaona watoto wakisogelea na kusikiliza mazungumzo. Nilizioona sura za watoto wenye hofu. Msichana wa miaka 13 akasimulia jinsi alivyokimbilia porini kuhofia maisha yake.

  Ndio, kuna watoto wengi wa Nyololo leo ambao wangehitaji msaada wa kisaikolojia kuelewa kilichotokea na kuwapunguzia hofu yao.

  Nikiwa nimesimama pale kwenye meza ya biashara nikaisikia simu yangu ikiita. Ni Mtangazaji Gershom Malegesi wa Ebony FM aliyekuwa tayari kuniunganisha na studio. Lakini, kwa nilichokuwa nikikiona na kukisikia pale kutoka kwa wakazi wenyewe wa Nyololo, nikashindwa kuijibu simu ya Malegesi. Sikutaka tena kuunganishwa hewani. Nilihitaji muda wa kutafakari.

  Hakika, niliyoyaona kutoka kwa wakazi wa Kijijini Nyololo ni pamoja na hofu, mashaka, hasira na zaidi maswali ya ' Kwa nini?". Kuna wanaojisikia vibaya sana kuona tukio lile baya limetokea kijijini kwao. Kuna wanaojisikia kukatishwa tamaa na mambo ya siasa na hawaipendi siasa kwa sasa. Kuna wanaojisikia aibu kuwa Kijiji chao kimejulikana sasa kwa sifa mbaya ya mauaji. Kuna wanajisikia kuwa watu wa kutoka nje wamekuja na kufanya mambo mabaya kijijini kwao.

  Nilizunguka kwa miguu kwenye mitaa ya kijiji cha Nyololo. Niliziona teksi mbili tatu kuu kuu ambazo hufanya safari za kutoka barabara kuu hadi vijiji vya ndani. Kuna ambao siku ya tukio gari zao zilikodishwa kuwakimbiza majeruhi au waliotaka kuikimbia Nyololo kwa haraka.

  Ndio, niliwaona vijana wale wa Nyololo, wa kike na wa kiume, ambao kwa kawaida ukipita Nyololo huonekana kuchangamka sana, lakini, Ijumaa ile niliyopita Nyololo niliwaona wakiwa kama ' Kuku waliomwagiwa' maji. Wengi hawakuchangamka. Hata kwenye sura z baadhi yao unaweza kuona, kuwa kuna jambo kubwa limewatokea na wako kwenye kutafakari na labda hofu pia. Maana, redio, runinga na magazeti bado yanazungumzia kilichowatokea.

  Na kikubwa nilichokiona ni kuwa; wakazi wa kijijini Nyololo wana ukweli ambao huenda wengine hawaufahamu. Ni wajibu wa wote wenye jukumu la kuusaka ukweli mzima wa kilichotokea kuwasikiliza wakazi wa Nyololo pia.

  Na bila shaka, kama Taifa, Nyololo inaweza kutusaidia kufungua ukurasa mpya wa namna iliyo bora na salama ya kwenda mbele kama ndugu wa Taifa moja. Kwamba kilichotokea Nyololo kisitokee tena.

  Maggid,
  Iringa.
   
 2. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Unanikumbusha machungu
   
 3. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,813
  Likes Received: 1,057
  Trophy Points: 280
  Funguka zaidi mate.
   
 4. Neiwa

  Neiwa JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 730
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Mkuu hicho kifo kimesikitisha ndio, ila personally naona sasa umezidi na ni wakati wakusonga mbele na kupumzisha hili swala tuangalie mambo mengine kama vile kukazana na mjane kama ulivyofanya.
   
 5. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Kwa hali hiyo, hawatakaa wakipende CDM kamwe. Chadema ndio wamesababisha yote haya. Na hii inatokana na uchu wa madaraka wa viongozi wachache wa CDM. Poleni sana wananchi wa Nyololo
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kama amba tuliishia kuona kwenye luninga na magazeti tu imetuumiza hivyo sijui hao walioshuhudia itakuwa je?
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  Exactly the CCM strategy, kuwatia hofu wananchi kuwa ikishika madaraka Chadema kutakuwa na matukio mabaya. So much for a democratic country, huh!
   
 8. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  A thinker?
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  umezunguka zunguka tu....
   
 10. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,581
  Likes Received: 848
  Trophy Points: 280
  wewe ndio umesema!
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Viva CCM endelea kuuwa kwa kutumia PolisiCCM
   
 12. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
 13. Mu-Israeli

  Mu-Israeli JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 2,456
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Hapana, watawachukia sana polisi, maana ndio walioua mwandishi asiye na hatia hata kidogo. Mwandishi hakuwa na kosa lolote, hakuwa mwana Chadema, hakuwa anaadamana, wala pale kijijini hapakuwa na maandamano wala mkutano wa hadhara.

  Picha zote zipo zinaonyesha polisi wakipiga mabomu ya machozi kwenye ofisi ya Chadema ambayo ilikuwa imefungwa !!

  Polisi wakabomoa mlango na kupiga mabomu ya machozi ndani ya ofisi ambayo ilikuwa imefungwa !!!

  • Rai kwa wana-JF wote wataotetea na kusherehekea mauaji haya kwa kushirikiana na CCM:-
  • Kumbukeni kuwa damu ya watanzania wasio na hatia inawalilia kwa uchungu mkubwa sana, na hakika, itawafuata ninyi wote akina Rejao na vizazi vyenu vyote mpaka mwisho wa maisha yenu.
  • Atawalaye kwa upanga, hakika, atakufa kwa upanga.
   
 14. G

  GODY MAGESSA New Member

  #14
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mjengwa hongera sana kwa habari zako....kikubwa zaidi ni namna ulivyohamasisha jamii kuichangia familia ya Marehemu. Mungu awe nawe daima.
   
 15. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  A great thinker!

  Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Sep 9, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Nadhani hata polisi pia hawatapendwa pia katika kijiji, hiki sipati picha wanamuonaje mtu alie katika sare za polisi.
   
 17. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #17
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  maggid

  For the sake of curiosity,kwa nini ulikataa kuwekwa hewani wakati tayari ulukuwa na watu ambao wangetoa first hand information?.Je walizungumza jamboambalo lilikuwa kinyume na ulivyoa mini kiasi ambacho ulijisikia vibaya?

  Hapa ni lazima utufafanulie kwani niliamini ungeingia hewani na ukawaweka mashuhuda hewani pia,kipi kilikuogopesha,tuambie.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #18
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Aisee, kumbe afande Kamuhanga alikuewa anatekeleza amri toka kwa viongozi wa CDM. Wabaya sana hawa CDM na polisi yao.
   
 19. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #19
  Sep 9, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,418
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  haya ndio mawazo na mategemeo ya wana ccm wengi ila kwetu sisi tunamawazo tofauti REJEO,CCM wanatumia polisi kuua ili mpate uhalali huo.subiri siku ya kura ndio utajua
   
 20. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #20
  Sep 9, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Maggid, no offense lakini mbona sioni habari katika ulichoandika?

  Kwamba watu wana hofu ni kitu kinachofahamika na sidhani kama kinastahili kuanzishiwa thread.

  Kwamba ukweli utafutwe, ndio lilikuwa linazungumziwa toka siku ya kwanza.

  Kwamba watu wana majonzi sidhani kama linahitaji kulifungia safari mpaka Nyololo.

  What exactly is the output of your visit to Nyololo?
   
Loading...