Mtangazaji wa E-FM kipindi cha Zilipendwa ana umri gani?

Padri Mcharo

JF-Expert Member
Feb 28, 2015
1,899
3,671
Wakuu,

Nimetulia getto namalizia ka weekend kangu nime tune 93.7 FM "namba ya bahati" nikiwa napata historia fupi ya Jabali la Muziki Marijani Rajabu.

Huyu mtangazaji nimekua nikimfatilia sana kila Jpili, the way anavoelezea huu muziki wa Enzi za baba yangu (Mungu akulaze mahali pema Amen) aisee jamaa ni kuwa alikuepo miaka hiyo ama anaingia google kupata story za wanamuziki.

Maana akianza kuchambua historia ya Ndala Kasheba, Maalim Ngurumo, Dar international, Tabora Jazz aisee atakuchambulia kuanzia mpiga gitaa wa bendi mpaka muimbaji alikua nani na sasa hivi yuko wapi....

Leo amechambua story ya Marijani na Fresh Jumbe aisee hata Baruan Muhuza (yule wa RFA kabla hajaenda TBC then Azam TV) haoni ndani....

Najiuliza jamaa atakua mzee sana eeh... Maana habari za wanamuziki wa zamani hapa bongo google hazipatikani kusema uingie upate kila kitu....

Kuna wimbo hapa wa "Makumbele nimevumilia mpenzi" umenikumbusha zile Cassette (kanda za radio) za Marehem Baba yangu... Alikua anaweka anaanza kucheza basi watoto tunacheka sana... Daaah

Dada Remmy dada sikilizaaa... Ndio bwana ndio bwana..
Nitakufa bure juu yako Remmy, Dada Remmy dada Remmy...
Tulia tuyajenge maisha Remmy, Bila wasiwasi Remmy...

"Tutu tutuu tututu tuuutuuuu" (hilo Gitaa sio sauti ya mtu)

E FM Bigup sana (Mawingu FM tupa kuleeee)
 
Si ni John Kitime naye alikuwa mwanamyziki mzuri tu enzi hizo ila siku hizi naona amekuwa mchambuzi wa muziki. Ni msanii wa siku hizo. Aliwahi kuwa mtahini wa mashindano ya BSS km sikosei amefundisha pia chuo Bagamoyo - hili sina uhakika nalo lkn
 
kwa hiyo askofu Gwajizo akichambua habari za YESU alikuwepo enzi hizo?au sheikh kiponzelo akimchambua mtume alikuwepo?
 
Kwanza hongera zake kwa uchambuzi mzuri.

Maoni yangu hawa wanamuziki nguli tungewatengenezea Documentary ambayo itadumu siku zote za maisha ya mwanadamu kizazi hadi kizazi
 
Saa kumi nam mibili jioni mpaka saa nne usiku. Sasa hivi bado kipo hewani....

Kwanza tunatoa shukurani, kwa serikali yetu ya Tanzaniaaaa...
Kutupatia nafasi, ya kwenda nje ya Tanzaniaaaaaa....
Kwenda kwenye maonyesho ya biashara Japaniiiii...

Noma sana.
Mpaka nimeingia YouTube
 
Ndio hapo clouds wanapopigwa bao!
Ile miziki ya zamani siku hizi ukisikiliza inafurahisha sana! hata kwasisi ambao hatukuwepo enzi hizo
Hakuna tv yenye kipindi cha miziki hiyo ya zamani

Tangu nigundue citizen tv wanakipindi kila jumamosi huwa sikosi!

E tv ikianza kufanya kazi hebu tupeni burudani hiyo ya muziki wa zamani
 
kwa hiyo askofu Gwajizo akichambua habari za YESU alikuwepo enzi hizo?au sheikh kiponzelo akimchambua mtume alikuwepo?

Mkuu,
Hahaha! Umeuliza swali zuri sana, kitu ambacho kwenye utamaduni wetu tunapaswa kujijengea udadisi kufahamu kwanini fulani amekuwa nguli ktk fani.
 
Nyimbo za zamani haziishi hamu, sio miziki ya kisasa kama big G dakika 10 tu huna hamu ya kusikiliza. Tanga wataanza kusikika lini? Najua wameruhusiwa kusikika mikoa kumi. Tunawasubiri kwa ham E fm, karibuni Tanga.
 
Baba alikuaga na sanduku limejaa radio cassette za Tabora Jazz na wale Marquise band aisee...

Dada Remmy dada sikilizaaa... Ndio bwana ndio bwana..
Nitakufa bure juu yako Remmy, Dada Remmy dada Remmy...
Tulia tuyajenge maisha Remmy, Bila wasiwasi Remmy...
Mzee home pia alikuwa na santuri nyingi sana za mbaraka Mwishehe wa Morogoro.

Ila Nakumbuka sana Tabora Jazz bwana....jamani kuna hakika havitasahaulika vichwani but tuandae documentary zao kila bend au mwanamziki
 
kwa hiyo askofu Gwajizo akichambua habari za YESU alikuwepo enzi hizo?au sheikh kiponzelo akimchambua mtume alikuwepo?
Kuna mambo mengine sio ya kuyalinganisha ujue...
Habari za Yesu na Mtume zipo kwenye maandiko na yeyote anaweza kuzipata popote na muda wowote, hapa suala ni maamuzi yako tu.
Lkn habari za wanamuziki wetu ( hasa wa zamani) zimeandikwa wapi mkuu. Wapi twende tukapate habari za tx moshi kwa upana? Au Nico Zengekala? Bila shaka hakuna!
 
ukisema hivyo unakosea mkuu watu wana stori za kinjekitile ngwale miaka mia iliyopita au mkwawa sembuse zengekara ambaye kafanya kazi na said mabera mpiga solo wa msondo useme hakuna mtafute mtu anaitwa mzee maftah au stazo wa magic fm atakupa stori za mwanamuziki salum abdala aliyefariki mwaka 1965 na hata ukienda morogoro leo dada yake na salum abdala bado yu hai atakupa stori za kaka yake,hiyo ndo kazi ya wachambuzi mkuu unatakiwa kuwa na vielement vya historians
 
Unapozungumzia muziki wa Tanzania ni pamoja na huyo Kitime, mwanamuzi wa Vijana Jazz ile uijuayo wewe. Wakati huo Vijana Jazz ndiyo ilikua kila kitu. RTD itakumbukwa kwa kukuza muziki wetu enzi zile
 
Wakuu,

Nimetulia getto namalizia ka weekend kangu nime tune 93.7 FM "namba ya bahati" nikiwa napata historia fupi ya Jabali la Muziki Marijani Rajabu.

Huyu mtangazaji nimekua nikimfatilia sana kila Jpili, the way anavoelezea huu muziki wa Enzi za baba yangu (Mungu akulaze mahali pema Amen) aisee jamaa ni kuwa alikuepo miaka hiyo ama anaingia google kupata story za wanamuziki.

Maana akianza kuchambua historia ya Ndala Kasheba, Maalim Ngurumo, Dar international, Tabora Jazz aisee atakuchambulia kuanzia mpiga gitaa wa bendi mpaka muimbaji alikua nani na sasa hivi yuko wapi....

Leo amechambua story ya Marijani na Fresh Jumbe aisee hata Baruan Muhuza (yule wa RFA kabla hajaenda TBC then Azam TV) haoni ndani....

Najiuliza jamaa atakua mzee sana eeh... Maana habari za wanamuziki wa zamani hapa bongo google hazipatikani kusema uingie upate kila kitu....

Kuna wimbo hapa wa "Makumbele nimevumilia mpenzi" umenikumbusha zile Cassette (kanda za radio) za Marehem Baba yangu... Alikua anaweka anaanza kucheza basi watoto tunacheka sana... Daaah

Dada Remmy dada sikilizaaa... Ndio bwana ndio bwana..
Nitakufa bure juu yako Remmy, Dada Remmy dada Remmy...
Tulia tuyajenge maisha Remmy, Bila wasiwasi Remmy...

"Tutu tutuu tututu tuuutuuuu" (hilo Gitaa sio sauti ya mtu)

E FM Bigup sana (Mawingu FM tupa kuleeee)
Mtangazaji huyo anaitwa John Kitime - mwanamuziki mahiri mzoefu. Pia wa wanamuziki wa The Kilimanjaro band (Njenje). Si mtu wakubahatisha anajua nini anachokifanya. Pia kuna huyu Masoud Masoud yupo TBC radio kwasasa nae ni mahiri sana. Uzuri wa hawa wawili wana background ya muziki. Wengine hujichomekea tu basi hapo ndio shida inaanza. Masoud Masoud jmosi iliyopita alimuongelea Marijani Rajabu, ilikuwa murua sana.
 
Back
Top Bottom