Mtangazaji wa Clouds tv 360 awataka Wasomi wadaiwa HESLB wakauze Ice Cream walipe deni

Je, sidhani kama ni sahihi kuanza kunikata mkopo kwa asilimia 15 wakati Mimi na wao tuliingia mkataba wa kukatwa asilimia 8. Hii haivumiliki, kwa kweli. Sheria hii ya 15% ilitakiwa itumike wakati gani? Nadhani hapa kuna changamoto, tunaomba wanasheria mtusaidie
 
Pengo la Kamoga halijazibika

Na sijui kwanini na yeye alikubali Uteuzi wa kwenda kuwa DED huko Mbulu na matokeo yake kutuleta matatizo mapya sasa 360 Clouds tv. Watangazaji wenzake aliowakuta na ambao kimsingi wanamzidi kwa kila kitu akina Babie Kabae na Sam Sasali tokea tuwajue hapo 360 hawajawahi hata siku moja kuwadharau na kuwadhihaki Watanzania kwa namna moja au nyingine ila huyu Hassan Ngoma hata miezi sita ( 6 ) hajamaliza tayari ameshaanza kututibua. Nakubaliana kabisa na Wewe tena 100% kuwa pengo la Hudson Kamoga bado halijazibika.

Halafu na Wewe Poti wangu Joseph Kusaga na Mtani wangu Ruge Mutahaba hebu muwe mnaangalia basi na Watu wa kuwaajiri hapo kwenu kwani kuna wengine watawaharibia na Vituo vyenu kuonekana ni vya hovyo hovyo. Tunamwomba huyu Mtangazaji wenu wa 360 Hassan Ngoma aombe radhi kwa kauli yake hiyo ambayo kiukweli imetukera sana na mno Watazamaji wenu na atumie platform hiyo hiyo ya tv yenu kuomba radhi.

Mimi ni Mdau wenu mkubwa tu ila kwa hii kauli ya Mtangazaji Hassan Ngoma nimesikitika kwa kiasi kikubwa. Msomi gani huyo asiyejua kuchuja maneno ya kujua wapi aseme nini na wapi apotezee?
 
Huyo Mtangazaji hajitambui. Anatafuta sifa za kijinga. Na huyo Mkurugenzi wa bodi ya mikopo anatafuta sifa. Tangu lini Wadaiwa wa Bodi ya mikopo wakaonekana ni wahalifu!. Anatakiwa ajue wanufaika wengi hawana Ajira mpaka sasa na wale walioajiriwa na wenyewe hali zao ni mbaya sana. Mishahara haijaongezwa, madaraja watu hawapandishwi bali wimbo wa UHAKIKI usiokwisha unaendelea!, Pesa mitaani hamna then hao Bodi wanapiga mikwala kila kukicha! .,Maisha ni magumu kwa sasa So waache MATAMKO YA KUTISHANA. Kudaiwa siyo kitu cha ajabu.
 
Kwani alicho sema cha ajabu hapo nin...ukidaiwa unatakiwa ulipe na anaekudai hapaswi kujua unatoa wapi pesa ya kumlipa...kwa hiyo kwan kuuza ice cream ni kosa...hapa ndo unaona hata wew ulivo mweupe kichwan...kazi ni kazi...kinachotakiwa ni walipe madeni...tena kawashauri vizr sana
 
Hao bodi ya mikopo washamba tu wanataka eti wapite nyumba kwa nyumba na ikibidi kwenye kumbi za starehe sasa izo ni akili kweli,cha kufanya wasamehe madeni waaendelee na hawa walioko vyuoni sasa kama ilivyo kwa serikali na mafisadi! Nadhani mafisadi wanne ni bora zaidi kuliko hawa maelfu ambao hatujui walipo maana yake ni kwamba kama tukiwabana mafisadi wanne tu tunaweza kupata pesa nyingi kuliko maelfu ya hawa masikini na kama basi tumeweza kuwasamehe hawa kwa nini tusiwasamehe na hawa wengine kuliko kujitoa akili kama hivyo kwa sababu wanachotaka kufanya naamini watafeli tu
 
KWANI KUUZA ICE CREAM SIYO KAZI HEBU ACHENI UJINGA,FANYENI KAZI MLIPE MADENI

Kuuza Ice Cream siyo dhambi ila ukimwangalia msemaji na body language yake unaweza ukaelewa kile ninachokilalamikia hapa ila kwakuwa bahati mbaya sana mfumo wako mzima wa kufikiri unaanzia kunakotoka Kinyesi badala ya Ubongoni huwezi elewa tunachokilalamikia hapa.

Sawa kuuza Ice Cream siyo mbaya je hizo Ice Cream utaweza kuziuza Mikoa ambayo ina baridi kwa nyakati nyingi za Mwaka? au unadhani Wadaiwa wote wa HESLB wako tu Dar es Salaam? Na hata kama akiuza hapa Dar unataka kuniambia anaweza kweli kuziuza na kuweza kulipa deni lake kwa spidi ambayo HESLB inataka?

Halafu na Wewe kwa upuuzi wako huu huko ulipo unajiita Msomi na Great Thinker? Ni aibu sana Mtu mzima kama Wewe unashindwa tu kujua kujenga hoja kwa suala kama hili ambalo linahitaji sana utulivu wa akili ili uweze kulijibu.

Namalizia kwa kusema tena kuwa Mtangazaji Hassan Ngoma wa Clouds tv 360 aombe radhi kwa hiyo Kauli yake ya Kifedhuli kabisa.
 
Na sijui kwanini na yeye alikubali Uteuzi wa kwenda kuwa DED huko Mbulu na matokeo yake kutuleta matatizo mapya sasa 360 Clouds tv. Watangazaji wenzake aliowakuta na ambao kimsingi wanamzidi kwa kila kitu akina Babie Kabae na Sam Sasali tokea tuwajue hapo 360 hawajawahi hata siku moja kuwadharau na kuwadhihaki Watanzania kwa namna moja au nyingine ila huyu Hassan Ngoma hata miezi sita ( 6 ) hajamaliza tayari ameshaanza kututibua. Nakubaliana kabisa na Wewe tena 100% kuwa pengo la Hudson Kamoga bado halijazibika.

Halafu na Wewe Poti wangu Joseph Kusaga na Mtani wangu Ruge Mutahaba hebu muwe mnaangalia basi na Watu wa kuwaajiri hapo kwenu kwani kuna wengine watawaharibia na Vituo vyenu kuonekana ni vya hovyo hovyo. Tunamwomba huyu Mtangazaji wenu wa 360 Hassan Ngoma aombe radhi kwa kauli yake hiyo ambayo kiukweli imetukera sana na mno Watazamaji wenu na atumie platform hiyo hiyo ya tv yenu kuomba radhi.

Mimi ni Mdau wenu mkubwa tu ila kwa hii kauli ya Mtangazaji Hassan Ngoma nimesikitika kwa kiasi kikubwa. Msomi gani huyo asiyejua kuchuja maneno ya kujua wapi aseme nini na wapi apotezee?
Kadhihaki wapi...katoa ushauri....anaeona unafaa afanyie kazi kama haufai apotezee....au na wew ni mdaiwa
 
Je, sidhani kama ni sahihi kuanza kunikata mkopo kwa asilimia 15 wakati Mimi na wao tuliingia mkataba wa kukatwa asilimia 8. Hii haivumiliki, kwa kweli. Sheria hii ya 15% ilitakiwa itumike wakati gani? Nadhani hapa kuna changamoto, tunaomba wanasheria mtusaidie
Jaman kweli hili linakuaje?kwan naomba mwanasheria atusaidia.huwez sain mkpo wa 8%afu baadae unatakiwa ulpe 15%kwan sheria inavyotungwa kwny vtu kama hv inakuaje???napata shda mm nisaidien
 
Back
Top Bottom