TANZIA Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde afariki dunia. Azikwa makaburi ya Kinondoni,Dar es Salaam

Kama wanayompa ruge maana hata huyu alifariki bado ni mfanyakazi wa CLOUDS
ruge alikuwa nani? na huyu ni nani

ruge alikuwa mmoja waanzilishi huyu n mtangazaji heshima yake huwez taka iwe kama ya ruge
 
Juzi kwenye miaka miwili ya kifo cha Ruge,uliona Kusaga family hata mmoja akiwa Bukoba??

Ruge alikua ameajiriwa na Clouds kama alivyokua Kibonde! Sema Ruge was a mastermind za shughuli zote za Clouds!
umewahi fatilia historia ya clouds fm,mwanzilishi ni nani
 

Habari za hivi punde ni kuwa mtangazaji maarufu wa Clouds FM, Ndugu Ephraim Kibonde amefariki dunia alfajiri ya leo tarehe 7 Machi 2019.

Kibonde alianza kusumbuliwa na presha akiwa katika msiba wa marehebu Ruge Mutahaba huko Bukoba mkoani Kagera na kuhamishiwa hospitali ya Bugando jijini Mwanza ambapo mauti yamemkuta. kifo chake kimetokana na kusumbuliwa na shinikizo la damu ambalo lilianza tangu akiwa mkoani Kagera alipokuwa akishiriki katika maziko ya aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza pamoja na Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM, Sebastian Maganga wamethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Baba mzazi wa aliyekuwa mfanyakazi wa Clouds FM Ephraim Kibonde amezungumzia kuhusu kifo cha mtoto wake na kusema kuwa ni mtoto wa pili katika familia na amezaliwa mwaka 1972 Upanga jijini Dar es Salaam.

Vilevile amesema kuwa Ephaim Kibonde amesoma hapa Dar es Salam na ameacha watoto watatu ambao ni Junior, Hilda na Illaria.

Kibonde pia alikuwa MC maarufu na mahiri katika shughuli mbalimbali amefariki dunia ikiwa imepita miezi saba tangu aondokewe na mke wake aliyejulikana kwa jina la Sara Kibonde wakati anapatiwa matibabu katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam

Bwana ametoa, Bwana ametwaa

Mwaka jana Ephraim Kibonde alimpoteza mkewe mama Sara Kibonde. Zaidi soma >TANZIA: Ephraim Kibonde afiwa na Mke wake Sara Kibonde - JamiiForums

View attachment 1039958
Ephraim Kibonde akiwa na mkewe enzi za uhai wao​
Endelea kupumzika kwa amani
 
Back
Top Bottom