Mtangazaji Masoud Masoud wa TBC

Zomboko mtu wa kujikomba sana..afu yeye anajua mziki wa bendi za Daresalama tu na ubabaishaji mwingiii
ha ha ha......Jamaa ni Mzaramo aise...jamii ya akina Mbwiga.

Ila anajitahidi kutukumbushia enzi zetu zile si haba......ila Masudi amebobea.
 
Jamaa ni manju wa muziki lakini aliniacha hoi pale alipochemsha simulizi za marehemu Papa Wemba. Yaani sijuwi alidanganywa na nani maana alikosea wasifu wa Papa Wemba vibaya sana. Mwingine ambaye alikuwa mtaalam wa muziki ni marehemu Maestro Freddy Mosha. Jamaa alikuwa noma sana, Mungu ailaze roho yake peponi.
weka wazi Masoud alipochemsha na sio kutuhumu tu... pengine hukumuelewa
 
weka wazi Masoud alipochemsha na sio kutuhumu tu... pengine hukumuelewa


Alisimulia kuwa Papa Wemba ndiye alikuwa muasisi wa Zaiko na alipiga muziki na Dindo Yogo Zaiko. Akaweka wimbo wa 'C'est La Verite," utunzi wa Papa Wemba uliotungwa mwaka 1974 akiwa na Zaiko. Waimbaji katika ule wimbo walikuwa ni Nyoka Longo, Papa Wemba, Mavuela Somo, Gina Efonge (Gina Wa Gina).....Cha kushangaza Masoud alisema Papa Wemba aliimba na Zaiko ule wimbo mwaka 1969 akiwa na Dindo Yogo, kitu cha uwongo kabisaaaaaa. yaani mengi aliyo ongea dhidi ya Papa Wemba ni kama alisimuliwa na Le Mutuz vile kutokana na jinsi alivyochemsha.
 
Ama hakika hili ni gulu la habari za mziki na wanamziki.
Anaujua mziki hasa wa enzi zile sio hawa vijana wa kileo na kelele kelele za bangi.
Kutangaza hawajui ujuaji mwingi, matusi na maisha yao yamegubikwa makandokando mengi.
Cc Adam Mchomvu&B12


Hawa wa sasa wamewekwa tu ili kugawa service kwa bosses na ndiyo maana hawajuwi chochote.
 
Katika quotes zake ndani ya MKASI kuna sehemu alisema MAOFISINI KUNA WAKE ZA WATU WENGI TU WANAJIUZA?

Kuna nyingine kuhusu mziki alisema: HAKUNA ANAEIJUA HISTORIA YA MUSIC WA EA KAMA YEYE!
 
anakwambia mwanamuziki wa kweli ni ally kiba tanzania chanzo mkasi wa eat tv.
 
Wanamwita manju wa muziki. Huyu ni mtangazaji mkongwe na nguli wa maswala ya muziki na wanamziki, kupitia TBC.

Ukimsikiliza Masoud, utaelewa umuhimu wa specialization katika utangazaji, uandaaji vipindi na uandishi habari kwa ujumla.

Masoud anaelewa ni nini anachofanya na kwa muktadha muafaka.

Ukifuatia simulizi zake kimuziki sio tu zina mizania ya kimantiki bali pia zina mtiririko kama movie fulani hivi inayokushawishi kuendelea kuitazama uone mwisho wake.

Hongera Manju,
MASOUD MASOUD !
uko sahihi , ukisikiliza mahojiano yake na wanamuziki wa enzi hizo utasikia burudani tu, anamjua muhojiwaji na anajua amuulize nini. niliwahi kumrekodi akimuhoji, marehemu Kabeya Badu, Dingituka Molay na wengine wengine, ni kati ya watangazaji wenye upeo mkubwa na kazi yake.
 
Tunahitaji Masoud masoud wa miziki ya kizazi hiki kipya,kila zama ina watu wake na tuache hii biashara ya kupondea sana kazi za kizazi kipya as if hakuna wanachofanya mkuu
Kisima,tujikumbushe kule walikoanzia na walipo sasa,mziki wao umekuwa sana kwa kwelli ,kwahiyo tutegemee mazuri pia kwenye miziki hii.
 
Back
Top Bottom