Mtangazaji gani ulimjengea picha tofauti na jinsi alivyo, kuanzia kimuonekano, umri na uvaaji pindi ulipomsikiliza kwa mara ya kwanza radioni

Daah na kuna mwingine alikuwa anajiita Ezeden the rocker akitangaza asubuhi.Kiss fm ndo redio ambayo kiukweli ilikuwa inawatangazaji wanaovutia kuwaskiliza..De7 na demu mmoja hivi sijui akiitwa nani!
Ezden last time nilimuona akiwa anatangaza TV 1.
Speaking of D7 daaah alikua anatangaza na mdada mmoja sikumbuki jina lake ile kipindi ni African beats.. Top ujazo hahaha.
 
Ezden last time nilimuona akiwa anatangaza TV 1.
Speaking of D7 daaah alikua anatangaza na mdada mmoja sikumbuki jina lake ile kipindi ni African beats.. Top ujazo hahaha.
Au Huyo dada alikuwa anaitwa shalbano abubakari maana ili jina limekuja tu sijui limetokea wapi.
 
Vp mambo wakubwa, wana jf, vijana kwa wazeee
Ebhana leo nimekaa nimetafakari jinsi hii technolojia ilivyo kuwa na kusababisha mambo mengi kuwa mubashara, sijui kama nitakuwa nimeeleweka na Mada yangu.

Anyway me Kuna watangazaji wengi sana niliokuwa nawafuatilia miaka hiyo ya nyuma wakati huo hakuna hii mitandao ya kijamii na hata sasa ninapomsikiliza mtangazaji yeyote ktk Radio ikiwa sijawahi kumuona huwa namtengezea picha kuwa huyu mtu yupo hivi kuanzia muonekano umri na hata uvaaji wake

Wakwanza

1. Fredrick Bundala
Huyu jamaa kipindi hicho namfuatilia kupitia rfa ktk kipindi chake Cha sintosahau jinsi alivyokuwa anakifungua kipindi na alivyokuwa anajitambulisha basi nilikuwa namvutia picha kuwa huyu jamaa kava suti kali na nimtu mmoja ambaye anamuonekano kama mkurugenzi Fulani hivi yaani nilijuwa jamaa ni miongoni mwa wasomi wa level Fulani, kiukweli jamaa alinivutia Sana jinsi alivyokuwa anajitambulisha pindi anapofunga kipindi na hata alipokuwa anakifungua kipindi

2. Esielo Mafuru
Huyu jamaa kwa mara ya kwanza namsikia nilijuwa ni mtu Fulani ambae age imekwenda Sana, na hii nikutokana na sauti yake
Nakumbuka nilianza kumsikia ktk kipindi Cha habari na muziki pale Tbc taifa, Kumbe ni dogo tuu pia Kuna siku nilikuwa na ndg yangu tunasikiliza kipindi wakati huo esielo Mafuru alikuwa anatangaza nikamuuliza hivi huyu mtangazaji anayetangaza unahisi anamiaka mingapi? Yule ndg yangu akaniambia kama 70 hivi nilicheka Sana.

3. Milard eyoooi
Huyu jamaa kwa mara ya kwanza namsikiliza kupitia Amplifaya
Nilidhani ni jamaa Fulani kaenda hewani halafu anapenda kuvaa mashati ya mikono milefu na suruali,
Kumbe jamaa jamaa nikafupi na bishoo kishenzi yaani mitupio yake ni tshrt na bukta huku kapelo kageuza.

4.Fredwaa
RIP, kwakweli jinsi nilivyomjengea taswira na nikaja kumuona Leaders club kipindi Fulani kumbe ndivyo alivyo
Kwani kipindi ana host rfa ktk kipindi chake Cha sindano Tano za moto nilijuwa tuu huyu jamaa atakuwa mbavu halafu anamwili mkubwa ndivyo alivyokuwa kimtindo nilimuotea.

5.Miliamu Migomba
Huyu mwanadada nilimjengea taswira Fulani hivi, kuwa ni msicha mwembamba na anapenda kuvaa vitopu na hiyo ni kutokana na sauti yake kuwa nyororo na nyembamba
Nimekuja kumuona kwenye Tv Kumbe ni bonge la mama na nguo zake ni madera.

Wapo wengi ila acha niishie hapo
Note; wakati nawasikiliza hao presenters nilikuwa nipo mbwinde huko ambako ukinunua maji ya kandolo mfuko unaambiwa urudishe au ukinunua ubuyu vimbegu unaambiwa urudishe.
Mimi wala sitaki kusema maana ni kama wote wananiboa haswa mademu, redio inawaficha sana hawa mazezeta. Sielewi kwanini kila demu mtangazaji anavaa magunia kichwani na mwili mzima, wanaboa sana na hawana mvuto kutokana na uvaaji wao wa kizee. Utakuta demu yuko under 30 anavaa kama kibibi cha kijijini chenye miaka 70, full dera ama gunia kichwani mpaka chini. Hapa Tanzania mko free hamko Uarabuni kuvaa mivitu ya hajabu mwilini.
 
Back
Top Bottom