Mtangazaji aliyeongoza Mapokezi ya Mbowe mkoani Kilimanjaro ni nani?

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,905
44,017
Habari za Jumapili.

Wakuu mimi ni miongozi mwa watu ninaopenda wachapa kazi, mahiri, weledi na wanaojituma hasa kwenye professional zao.

Jana nikipitia video clip mbali mbali zilizosambaa kuhusu Msafara wa Mwenyekiti Taifa Freeman Mbowe akirejea nyumbani kwao Machame nimeshuhudia Kijana shupavu mwenye mvuto ktk utangazaji.

Kijana huyu aliyeonekana akivalia T-sheti ya njano isiyoiva hivi alikuwa mchangamfu akipita hapa na pale kukusanya maoni ya makutano mbali mbali.

Kilichonivutia zaidi ni commitment persistence bila kuchoka anayoonesha.

Lakini pia namna anavyoweza ku-interact na watu wa level na hali mbali mbali wakati wowote

Hii imenikumbush mtangazaji Mahiri aliyepata kuvuma wakati wa Uchaguzi mwaka 2015 akiliripoti habari za Mgombea wa Ukawa Lowasa Bwana Sam Mahela akishirikiana na mkongwe presenter Anfrey wa ITV miaka hiyo.

Pia inanikumbusha watangazaji wengine Mahili kama Tido Muhando, Emanuel Buhohera, Prosper Kwigize waliowahi kulivuruga anga la Rediowave hapa Tanzania.

Huyu kijana wa jana ni nani??

Akiendelea hivi namuombea Atafika Mbali sana.

 
Sam mahela baadae aliajiriwa Tbc.

Nadhani baada ya hapo hakusikika tena sijui aliridhika au alivunjwa moyo na jambo gani.
 
Topic inaanzishwa kuhusu Mtangazaji wa Mbowe

Nyinyi mnaigeuza kuwa ya Sam mahela na maisha yake binafsi?

Kama topic haina tija...ya nini mnaianzisha?
Hapa mada ni Watangazaji Mahiri na wenye kujituma.
Mahela ametolewa kama Mfano tu.
 
Back
Top Bottom