muvika online
JF-Expert Member
- Nov 27, 2016
- 374
- 283
Mtandao wa Yahoo kwa mara nyingine tena umetangaza kwa wateja wake kuwa huwenda akaunti zao zikawa haziko salama kutokana na kugundulika kwa udukuzi mwingine uliofanyika kati ya kipindi cha mwaka 2015 na 2016.
Katika hudukuzi huu Yahoo ilituma meseji maalum kwa watumiaji wake ikiwataka kuchukua hatua za kuongeza ulinzi kwenye akaunti zao kwa mujibu wa tovuti za bgr na thenextweb kwenye shambulio hilo wadukuzi hao hawakutumia password ili kupata uwezo wa kuingia kwenye akaunti yoyote bali walitumia mtindo wa forged cookie ambapo wadukuzi hao walipata uwezo wa kuingia kwenye akaunti ya mtu bila hata kuhitaji password.
Tovuti hizo zinaendelea kuandika kuwa wadukuzi hao waliweza kuiba programu maalum kutoka kwa kampuni ya yahoo ambapo baadae waliweza kubadilisha programu hiyo na kuitumia kutengeneza forged cookie ambapo baadae ndizo zilizotumika kudukua mtandao huo maarufu. Hii ni mara ya tatu kwa mtandao huo kudukuliwa baada ya mtandao huo kudukuliwa na akaunti bilioni moja kuathirika, pamoja na shambulizi lingine lililofanyika miaka ya nyuma. Mtandao wa yahoo unaonekana kukubwa na matatizo mengi sana kipindi hichi wakati kampuni ya Verizon ikataka kununua mtandao huo. Ni vyema kuchukua hatua mapema kama unatumia Email ya Mtandao huo.