Mtandao wa Airtel sasa wanatuibia wateja wao bila woga

Mtandao wa Airtel sasa wanatuibia wateja wao bila woga

Airtel masaa 48 kwa 500Tsh
1.2 GB
Ila kama uliwasha ndo hivo wanakula
 

Attachments

  • 1435144145193.jpg
    1435144145193.jpg
    50.2 KB · Views: 167
Kwa kweli airtel wahudumu wake wanadhalau sana sana sana tena sana mimi airtel nina miaka 17 toka celtel ila hawa wa sasa hapana pangekua wanaweza wakabadilishana na voda au tigo mwezi mmoja tu wangenyooka ukipiga simu wakipokea same time wanakata wakipokea kama hamuelewani nao wanakwambia bonyeza 5 yaani uwaburudishe muziki uwapendao, kweli mteja unamjibu hivyo?

= wanadharau
 
Hata mimi ni muathirika wa huu wizi, Ukiweka salio kila siku wanakukata wakati sijajiunga na "takataka" yoyote. Hakuna kitu nachukia kama kuibiwa. Kwa nini jasho langu liibiwe hivi hivi? TCRA huwa wao hawalionagi hilo au line zao huwa hazikatwi?
 
Airtel wamesha niibia bandle ya sikumoja na wiki iliyofuata wakaniibia sh mia sita sasa ivi siweki hela kabisa. Angalieni cm zenu kila siku wanapitia salio wanaiba, haiwezekani una kifirushi alafu salio linatoweka. Wezi
 
Mbona Mimi huwa Siibiwi kijinga Jinga.. Maana Naweka Hela Yangu Kama Ni Airtel Money.. Tigo Pesa Au M pesa.. Then Kama Nataka Kujiunga Huwa najiuliza Haya

1. Nimekopa
2. Nimewasha Data
3. Simu yangu Ina Auto Update ya Apps
4. Kuna App Inaendelea Kudownload
5. Nimejiunga na Mahuduma Yao ya Kishenzi shenzi. Sijui Caller tune... Ofa sijui za Magazeti... N.k

Na Jibu Likija NO. Ndo natoa Pesa Kwenye Account yangu najiunga na Bundle.. Sinaga Mtindo wa Kununua Vocha Direct hata Siku Moja... Kama Nataka matumizi ya Mwezi natenga Bajeti ya Mwezi naweka Kwenye Account yangu ya Simu..

Mtakuwa Mnalia Kila Siku Sometimes ni Makosa YENU . unakuta Mtu una Madeni kibao halafu ukikatwa Unalalamika

sambamba na mie aisee sijawahi juta
 
Hao hao kuna mikoa wameibagua sana , Kama Iringa hamna Ofisi za Airtel so kama unahitaji huduma funga safari kwenda Mbeya au Dodoma ndo utakutana na hizo ofisi

Acha uongo wewe,ofisi za airtel iringa zipo maeneo ya nyuma ya jengo la asas karibu na iringa hotel
 
Back
Top Bottom