Mtambuzi apata mtoto, Baby Boy

sijui kama umekulia vijijini kama mie.

Tulikuwa hatuna mipira hii aina ya kuchezea tenesi.

Tulkuwa tunatumia mayai ya mijusi au nyoka fulani hivi kudunda dunda kama tenesi.

Ukifika umri kama huu wangu, mayai yanadunda tu na wala si unyanyapaa.

Pampzi tunapeleka wapi?

Mkuu mwenzako umri umesonga.....Nafuata maandiko yaliyosema "ENENDENI MKAZAANE MUIJAZE DUNIA"
Pampzi ziletwe MTAMBUZI PUB, pale viunga vya TABATA UBAYA UBAYA.....
 
Wadau wa MMU,
Taarifa zilizonifikia hivi punde ni kwamba mwanaJF mwenzetu Mtambuzi amejaliwa kupata mtoto wa kiume.

Tuungane pamoja kumpongeza Mtambuzi na mke wake(mama ngina)

Ahsante mkuu kwa kufikisha taarifa MMU, maana ulikuwa kama vile unaangalia mechi ili kusubiri matokeo..... vile kipenga cha mwisho kinalia tu, ukaruka hewani......LOL
 
Huyu Mtambuzi kumbe tapeli si amejitangazia uzee?? Mtoto wa nini sasa saa hizi??? Kuanzia leo wewe sio mzee yaani bado unatotolesha tuu??? Mie nimefunga miaka 16 iliyopita??? Kha!!!
 
87.gif

Congratulations Mkuu Mtambuzi
 
Last edited by a moderator:
kwanza niombe Mods wasiutoe huu uzi hapa mmu kwa heshima ya Mtambuzi katika jukwaa hili.

Pili naanza kuwaamsha wana Mmu wote tuanze kazi mapema kwa ajili ya kumkaribisha kichanga wetu siku ya leo. zifuatazo ni kazi za leo
King'asti mtoto mkubwa wa mzee Mtambuzi wewe utakaa nyumban kupokea wageni na kuwasaidia wakina mama watakaokuja kumsaidia mamam ngina kazi. jeneneke, Smile, Preta sweetlady nyie mtashughulika na kupiga nguo za mama ngina na za kichanga pasi mhakikishe mmezipanga vizuri. mwanangau Ronn M, ukisadiwa na wajomba zako platozoom Eiyer, Mentor, Excellent mtafunga baby Cort na kaauhakikisha imekuwa stable mtoto asije anguka.
cacico, @fp, wakiongozwa na ASHA dii hawa watamkanda mama mtoto maji ya leo siku ya kwanza baada ya dr MziziMkavu na dr riwa kumpatia discharge leo saa mbili.

kuhusu mapish BADILI TABIA akisaidiana na charming lady na eversmilinggirl watahakikisha kuko sawa. mwl mwenzangu snowhite wewe utahakikisha mambao yote yako sawa hapo nyumban manake mie si unajua sitoweza kuepo bado nauguza?

akina dada wengine wote kila mmoja abebe ndoo yake aende kumtekea maji manake tabata kuna shida ya maji sana.msichelewe wapenzi kuanza kazi mapema.
BAK na Boflo nyie mtampiga mtoto picha na mzee wetu Dark City na Asprin asali ya moyo ya wengi nyie mtahakikisha mnawah mnadani vingunguti kuleta mbuzi safi wa supu ya mzazi na hapa mchinjaji ni ma swtlo Kaizer akisaidiwa na Mr Rocky.

wakaka wengine wote hakikishen kwamba Mtambuzi anapata kampani ya kutosha manake aliugua sana toka jana utafikiri yeyey ndo alokuwa anataka kuzaaa so mpeni liwazo la kutosha na hapa kaka mkubwa SnowBall usimamie hili.

asubuhi njema mie ntakuwa napita tu kuangalia kama kazi zimeenda sawa.
 
Last edited by a moderator:
Wadau wa MMU,
Taarifa zilizonifikia hivi punde ni kwamba mwanaJF mwenzetu Mtambuzi amejaliwa kupata mtoto wa kiume.

Tuungane pamoja kumpongeza Mtambuzi na mke wake(mama ngina)

Hongera zao, Mungu amtunze na amjalie kukua katika HEKIMA NA KIMO kwa ufanisi wa hali ya juu sana aje kuwa kuwa GT baadaye
 
Hongera sana Mtambuzi. Mwenyezi Mungu amjalie mtoto afya njema akue katika kimo. Amlinde katika magonjwa na madhaifu mbalimbali. Hongera kwa mama Ngina pia. Mwita Maranya asante kwa taarifa aise.
 
Last edited by a moderator:
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom