kasharunga
Senior Member
- Feb 28, 2013
- 128
- 28
Ni jambo la kushangaza kuona mtambo wa Richmond na sasa unaitwa Symbion bado upo nchini na unafua umeme na kuingiza umeme kwenye Grid ya Taifa baada ya kuwauzia Tanesco.
Madhara ya mtambo huo ni kwamba bei ya umeme imekuwa ikipanda kila kukicha baada ya gharama za uendeshaji zinapopanda km gas,vilainishi,mishahara na kadharika.
Gharama zote hizo anabebeshwa Mtanzania. Ikumbukwe ya kwamba Kamati iliyoundwa kuchunguza kashfa ya mtambo iliagiza mtambo huo urudishwe ulikotoka na maagizo hayo hayakutekelezwa na mtambo huo ulibakia Tanesco Ubungo .
Hii ilikuwa siri kubwa ambayo mpaka sasa tunajiuliza imekuwaje mtambo chakavu umeungwa kwenye Grid ya Taifa na unazalisha umeme mfululizo sasa ni mwaka wa nne?
Hii imekaaje Mama Clinton alikuja nchini kuuzindua rasmi , je mweshimiwa kama yule angekuja nchini kuzindua mtambo chakavu na kusifia mtambo huo?
Haiingii akilini haya makamati tunayounda ndiyo yanayotupeleka kubaya. Aidha inawezekana mikataba tunaiangalia kwa mtazamo finyu au wajanja wanatumia mwanya huo kuhujumu uchumi.
Tujiangalie kwa mapana mtindo kama huo IPTL imetushika pabaya .Inavyooneka Rais wetu aliyepo au ajaye mitambo kama hii itaifishwe au tuinunue tuachane na maumivu haya