TANESCO: Mtambo wa kuzalisha Megawati 20 za umeme umewasili Nchini ukitokea Marekani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,792
11,952
Ijumaa Desemba 2, 2022, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lilitoa taarifa ya jitihada za muda mfupi zilizokamilika pamoja na zinazoendelea kufanyika katika kukabiliana na upungutu wa umeme.

Leo Jumanne Desemba 6,2022, TANESCO imetoa ripoti kuwa tayari mtambo wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 20 za umeme umewasili Nchini ukitokea Marekani siku ya Jumamosi Desemba 3, 2022.

Mtambo huo utafungwa katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia cha Ubungo namba Ill.

Majaribio ya mitambo miwili katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba I yanaendelea vizuri, na kwa sasa mitambo hiyo inaingiza jumla ya Megawati 65 za umeme katika Gridi ya Taifa.

Wamesema kuwa wanategemea hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Desemba 2022, mitambo hiyo itakuwa ikizalisha jumla ya Megawati 90.

“Bado tunaendelea na kazi za matengenezo ya mitambo miwili ya Ubungo namba Ill ambapo baada ya kukamilika mwishonl mwa Desemba 2022, itazalisha jumla ya Megawati 40 za umeme.

Kuhusu jitihada za kati Tanesco wamesema “Tunategemea mitambo mingine miwili kuanza kufanyakazi katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba I kuanzia mwezi Februari 2023 ili kuingiza Megawati 90 za umeme katika Gridi ya Taifa.
2b35a12e-fd7f-4b0c-9a67-8b31b82d6fae.jpg
 
Movie inazidi kwenda mbele. Hapo mtambo unanunuliwa kilazima wakati issue ni maji yamepungua kama wasemavyo. Huo mtambo naamini utakuwa unafua umeme kwa kutumia unga wa dona sio maji wala.
Mwendazake mitambo ilikuwa inamuogopa kwelj maana hadi kuchoka, service na kuharibika ilikuwa inajitutumua.
TUMEPIGWA TU
Mtambo wa 123M hadhi yake ni 60M
Na utapokelewa na chief hangaya kwa sherehe
 
Ijumaa Desemba 2, 2022, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lilitoa taarifa ya jitihada za muda mfupi zilizokamilika pamoja na zinazoendelea kufanyika katika kukabiliana na upungutu wa umeme.

Leo Jumanne Desemba 6,2022, TANESCO imetoa ripoti kuwa tayari mtambo wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 20 za umeme umewasili Nchini ukitokea Marekani siku ya Jumamosi Desemba 3, 2022.

Mtambo huo utafungwa katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia cha Ubungo namba Ill.

Majaribio ya mitambo miwili katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba I yanaendelea vizuri, na kwa sasa mitambo hiyo inaingiza jumla ya Megawati 65 za umeme katika Gridi ya Taifa.

Wamesema kuwa wanategemea hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Desemba 2022, mitambo hiyo itakuwa ikizalisha jumla ya Megawati 90.

“Bado tunaendelea na kazi za matengenezo ya mitambo miwili ya Ubungo namba Ill ambapo baada ya kukamilika mwishonl mwa Desemba 2022, itazalisha jumla ya Megawati 40 za umeme.

Kuhusu jitihada za kati Tanesco wamesema “Tunategemea mitambo mingine miwili kuanza kufanyakazi katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba I kuanzia mwezi Februari 2023 ili kuingiza Megawati 90 za umeme katika Gridi ya Taifa.
View attachment 2437844
Hili swala niliwahi washauri humu:
Tujaribu kuongeza uzalishaji wa umeme wa gesi ili kutatua tatizo la kukatika kwa umeme
 
Miaka miwili nyuma kulikuwa na umeme wa uhakika na lugha ilikuwa ya majigambo tunaweza miradi ya megawatts 2000+ na mfano juu.yake

Leo tumerudi na hadithi za megawatts 20.

R.I.P shujaa Magufuli
Mambo ya masandarusi kama kazi !! Walisema mitambo ilikuwa haifanyiwi marekebisho kipindi kile !! Sasa ndio inafanyiwa matengenezo!! Na umeme ndiyo imekuwa shidaa !!
 
Njia ya mtu muongo siku zote huwa ni fupi.

Anyway kuna watu wengi ndani ya JF walishatuonya miezi kadhaa nyuma inatafutwa sababu ya kupigwa deal.

Ngoja sasa tuambiwe gharama ya huo mtambo.

Ajabu zaidi logistic tu ya kununua huo mtambo na kuuleta hadi Tanzania udhani ni kama chini ya miezi mitatu; ina maana walijua mapema nchi itakuwa na giza la muda mrefu kweli kweli kuweza kufanya yao.

Only in Tanzania
 
Hivi suala la umeme ni dharura kweli?
Hatujui hali ya hewa na hali ya mitambo yetu. Nchi hii tatizo la umeme ni Disemba.
Hii zima moto ni upuuzi.
Kwanini hii changamoto ya miaka nenda rudi is iishe.
Aliyesema bwana litatatua changamoto zote ni nani.
Tuwaze nje ya boksi
 
Back
Top Bottom