Mtalii afariki dunia baada ya kujaribu kujipiga "SELFIE"

wizodg

Member
Dec 24, 2018
95
90
Mwili wa Mtalii mmoja kutoka Saudia alikufa maji baada ya kutumbukia kwenye mto Nile nchini Uganda siku ya Jumamosi , sasa umepatikana.

Kwa mujibu wa polisi nchini humo, Alsubaie Mathkar alikuwa na marafiki zake katika eneo la maporomoko ya Kalagala lakini kwa bahati mbaya mahali alipokanyaga akipokuwa anajipiga picha ya Selfie palikuwa na utelezi jambo lililosababisha yeye kuteleza na kuanguka mtoni.

Imechukua juhudi nzito za vikosi vya wanamaji na wavuvi kuupata mwili wake ambao ulikuwa umesombwa na maji yaliyokuwa yakipita kwa kasi mmno.

Kumekuwa na ongezeko la ajali wakati watu wakichukua selfie katika maeneo tofauti tofauti duniani tangu kujiri kwa mitindo hiyo ya kujipiga picha kwa kutumia simu za mkononi, na baadhi ya wasimamizi wa maeneo ya kitalii wamechukua hatua za kupiga marufuku ya jumla.

Je hatua gani za kiusalama zapaswa kuzingatia unapopiga picha ye
 
Ajali kazini. Umauti upo tu snappika ww. Hatutaki taifa la watu waoga waoga. Selfikeni bhana km cm yko ipo smart
 
Mwili wa Mtalii mmoja kutoka Saudia alikufa maji baada ya kutumbukia kwenye mto Nile nchini Uganda siku ya Jumamosi , sasa umepatikana.

Kwa mujibu wa polisi nchini humo, Alsubaie Mathkar alikuwa na marafiki zake katika eneo la maporomoko ya Kalagala lakini kwa bahati mbaya mahali alipokanyaga akipokuwa anajipiga picha ya Selfie palikuwa na utelezi jambo lililosababisha yeye kuteleza na kuanguka mtoni.

Imechukua juhudi nzito za vikosi vya wanamaji na wavuvi kuupata mwili wake ambao ulikuwa umesombwa na maji yaliyokuwa yakipita kwa kasi mmno.

Kumekuwa na ongezeko la ajali wakati watu wakichukua selfie katika maeneo tofauti tofauti duniani tangu kujiri kwa mitindo hiyo ya kujipiga picha kwa kutumia simu za mkononi, na baadhi ya wasimamizi wa maeneo ya kitalii wamechukua hatua za kupiga marufuku ya jumla.

Je hatua gani za kiusalama zapaswa kuzingatia unapopiga picha ye
Inatakiwa taasisi zinazosimamia hifadhi za Taifa ziandae maeneo maalumu ambapo watalii wa ndani na nje watapatumia kupiga picha za selfie na SIYO kila mahali mtalii anapoona yeye panafaaa..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom