Mtaka ndiye unayefuata

When the rippen time is due...!
 
Maisha yapo tu mlango ukifungwa Mungu anafungua dirisha nalo likigungwa vent zipo- hewa itavutwa tu kwa sababu ni ya bure
 
Duh! mamlaka ya uteuzi ikiwa inaondoa watendaji wazuri kwasababu ya majungu na kusagiana kunguni unakuwa ni udhaifu wa hali ya juu.

Ndio maana wale akina naniliu walikataa teuzi, na hata yule bosi wa zamani wa ile idara ya wale jamaa wanaojaza majina yao kwenye 'mikeka' 🫡

Wateule wapimwe kwa utendaji wao kulingana na malengo waliyokubaliana na kiongozi wao. Ujinga mwingine wote upuuzwe.
 
Unajua bora uwe na maamuzi ya kuamua unaweka wazi au husemi kabisa. Kama mtaka unamjua vizuri na hutaki kumwaga unga mfate kwake uongee nae kiume. Sio unatuletea mafumbo mafumbo ambayo sisi ambao hatuna interest na mtaka unatupotezea muda.

Be a man speak it out or stay quite. UMENIKERA. Halafu hizi aidii mpya zina shida sana
 
Atakuja mhunze mnadani mchome wote nyama za mbuzi.

Yes ni suala la Mda tu si
unaona Hata lile zengwe la mifuko hewa ya mbolea lilikuwa kwake

Team msoga wanamtafuta Kwa fujo Sana Huyu mzalendo
aliyebaki
 
Sasa Mzee Uzi ungeupitatu kwanini umeufungua!
 
Ila binafsi Mtaka namkubali kwenye msisitizo wa watoto kusoma
 
Kwa hiyo unataka wasomaji wako waelewe kitu gani hapa?

Unapopika majungu, haya ndiyo matokeo yake. Unaogopa kueleza chochote ili watu wajue na wajadili mada yako.

Huoni kwamba haya ungemfikishia yeye mwenyewe mhusika bila ya kutuhusisha sisi kama ulikuwa huoni umuhimu wetu kujua unaongelea jambo gani?

Kama wewe ni mkubwa kwa Mtaka, inaonyesha ni mtu wa makamo sana, lakini inaelekea akili imebaki kuwa ni ya kitoto kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…