Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,039


Leo nimekumbuka hii ngoma ilivuma Sana enzi zile wakati bado blackberry na apple ni matunda hayajawa simu.

Title ya wimbo ilitokana namsemu wa aliyekuwa raisi wa JMT awamu ya 3 Bwana Ben Mkapa kuwa anapenda kusema "mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe."

Pia ukanikumbusha uncle yangu alikuwa anasafiri kutoka Bkb Kuna Dar wakapita kwenye pori la kasindaga. Kipindi hicho kusafiri kwa Basi ulikuwa noma Barbara mbovu unachukua hata wiki kufika. Simu za mkononi hakuna Yani maisha bado Sana.

Sasa wakatekwa kwenye pori, halafu wake wazee wa kazi wakiwa namitutu wakawa wanawatandika abiria bakora huku wakiwaambisha huo wimbo "mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe."

Baada ya kuchukua Mali zao, wakawambia pelekeni salami kwa Mkapa, mwambie site ni wezi ila sisi tunatumia bunduki yeye kalamu.

Salami zilifika Mkapa akashusha jeshi, Kama ulikuwa unakisiwa kuwa jambazi ukiamka asubuhi unakuta gari la wanajeshi wamekata njeya nyumba yako wanakusubiri, wanakubeba na kwenda nawe kambini.

Kweli mtaji wa masikini ni nguvu yake mwenyewe. Banza Stone alikuwa mkali Sana RIP
 
Jamani jamani,,Banza stone ame dead?..!!!
Chanzo nini asee....!!
Bro ulikua jela nini? Alikufa 2015.

IMG_20210207_232428.jpg
 
Back
Top Bottom