Mtaji wa kwanza ili uweze kufanikiwa ni kuwa na Shahuku ya kufanikiwa

sylivesteralmas

New Member
Mar 4, 2019
2
45
Habari ndugu. Natumai u mzima wa afya kabsa,

Leo Ni siku njema kabisa ambayo ningependa kukushirikisha kitu kimoja ambacho vijana wengi wa kitanzania na Afrika kwa ujumla tumekikosa katika ulimwengu wa kutafuta mafanikio. Hicho kitu si kigeni Sana, nacho ni Shahuku ya kufanikiwa.

Shahuku ya kufanikiwa.

Hii ni silaha kubwa ambayo tajiri yeyote duniani na wote waliofanikiwa katika Mambo mbalimbali wanayo, Hii Shahuku huanza kwa mtu kuamua toka ndani, Muandishi mkubwa wa vitabu, Robert Kiyosaki katika moja ya vitabu vyake alielezea kwamba, alipofikisha umuri wa miaka 27 aliamua kuwa anataka kuwa tajiri, maamuzi yake yalimfanya atamani kufikia kile alicho kihitaji na mpaka Sasa ni mtu aliyefanikiwa.

Hiki nikitu ambacho natamani Sana vijana wengi wa kiafrika tuwenacho. Tuache kulaumu serilkali, hali duni, kutokuwa na mitaji na Sababu ya kuzaliwa bara masikini, Hakuna atakae fanya bara hili liwe tajiri bali sisi, Tuamke tukijua Bara letu limejaliwa utajiri wa Kila aina ni sisi ndiyo tunatakiwa tuinue vichwa vyetu huku tukiwa na Shahuku ya kufika mbali kimafanikio na Mungu atatusaidia.

Kumbuka mtaji bila Shahuku bado ni bure tu, Akhsante.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom