mbongowakweli
JF-Expert Member
- Aug 24, 2011
- 845
- 675
Wakuu msaada, najua kuna vichwa humu, naombeni msaada wa biashara gani nifanye, nina capital ya 2.5m/-.
Asanteni
Asanteni
Hizi thread za biashara mtaji milioni, laki, elfu kumi sasa zimezidi!
Biashara nyingi zishasemwa humu ni swala la wewe kuangalia kama mwenzio alikuwa na 2m akashauriwa afuge kuku basi na wewe wa 2.5m biashara hiyo itakufaa.
Mwenye 10m anaweza fanya biashara sawa na mwenye 2m ila scale yenu ya b'ness ndio mkatofautiana.
Hizi thread za biashara mtaji milioni, laki, elfu kumi sasa zimezidi!
Biashara nyingi zishasemwa humu ni swala la wewe kuangalia kama mwenzio alikuwa na 2m akashauriwa afuge kuku basi na wewe wa 2.5m biashara hiyo itakufaa.
Mwenye 10m anaweza fanya biashara sawa na mwenye 2m ila scale yenu ya b'ness ndio mkatofautiana.
Taja mambo yafuatayo na utapata msaada wa mawazo:
1) Upo mji gani?
2) Una ujuzi gani lengo ni kujua strengths na weaknesses zako
3) Je umetenga muda gani kui supervise business yako?/ je, hujaajiriwa sehemu full time.
4) Aina gani ya biashara inayokujia kichwani? Na unatamani uifanye?
sijasahau chochote, ngoja nisome kama kuna mtu atakuja na business idea mpya kabisa ambayo sijawahi kuisoma jf.Umesahau kwamba business environment ni dynamic, umesahau pia mawazo ya biashara gani ufanye yanabadilika kila sekunde, kumbuka pia wachangiaji wanaongezeka au kupungua katika jukwaa la biashara na mengineyo kila siku.
Mkuu, anzisha outlet ya nyama choma, mishkaki ya utumbo, kongoro special....something of the kind.
Kwa vile una bucha, utaqweza kupata malighafi safi sana.
What you need to do is make something different, chukua jiko kwenye bar ya kawaida tu....utanambia mkuu.
Ndg yangu Mbogowaukweli, sema tu una Sh. 2,500,000.00 ambazo hujui uzifanyie nini!
Hiyo ni hela ya kula na siyo capital aslan!
Umesema una Masters haya jiandalie mchanganuo wa biashara kama fedha hiyo haiishii kwenye mchakato tu wa biashara na siyo kuanzisha biashara? Hapa ndo maana tunakushauri fedha hiyo we kaifanyie shopping familia yako next time ukipata capital ndo uombe ushauri.
Nakushauri tena mtoe out my wife wako mkatumie hela hiyo ikuzoee ndo utapata maarifa ya kutafuta CAPITAL.
Boss wewe una hatari kweli, ungejua tu jinsi nilivoweza kuidunduliza io hela usingesema ivyo!
Anyway ndio maana ya kuomba msaada, itabidi nimeze mate na ushauri wa wazee wanaoona hii hela ndogo!