The silent smile
Senior Member
- Jul 17, 2025
- 124
- 206
Hili suala sijawahi kujua linatokana na nini, wataalamu watatuambia..
Pale inapotokea unamuogopa tuu mnyama (wanyama wadogo) au mdudu. Yaan ukiulizwa sababu za kumuogopa hata huna jibu lakueleweka bali unamuogopa tuu, hata kama uwe baunsa ila utashangaa unaogopa kajongoo😄
Sasa bana kila mtu atutajie mnyama au mdudu anayemuogopa na sababu za kumuogopa, huenda tukajifunza kitu.
Binafsi namuogopa sana PANYA, sio kwamba namuogopa kwamba ataning'ata, hapana... Namuogopa tuu bila sababu.
Kadhalika, sijawahi kuweza kumuua panya, hata umfunge kamba hlafu unipe fimbo au jiwe nimpige afe, siwezi kabisa, maana mikono ni kama inapata ganzi na kukosa nguvu na sitaki awepo/apite karibu yangu.
Nikifika sehemu hlafu nijue kuna panya, hapo sitokuwa na amani kamwe.
Na hata nimkute amekufa hlafu uniambie nimshike, utakuwa umenipa adhabu kubwa sana nisoiweza.
Karibuni kwenye mada.