Mtafute Mungu wakati anapoweza kupatikana

Mtafute Mungu wakati anapoweza kupatikana

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
4,014
Reaction score
6,770
Watu wanasema Awamu Mpya imeanza, tutakuwa na maridhiano, Mwendazake ameondoka, sasa tumeanza zama mpya za maridhiano, hiyo siyo kweli.

Mtafute Mungu wakati kuna nafasi. Kama watu wamekasirika kama watu wameghadhibika, haiwezekani kuwepo maridhiano.
Kama watu wamebembelezwa lakini hawataki kuacha fujo, dirisha la kupatana linafungika.

Mpangaji mpya Ikulu hawezi kubadili sera ya nchi. Sera itabadilika pale tu; yale mambo yaliyoleta mambo kandamizi yataondolewa.
Watu hawawezi kubadilika overnight.

Hakuna kitu kilichobadilika. Unataka kuridhiana na nani? Kuhusu nini?

Sijui watu wangapi wanamfahamu Marie Antoinette. Alikuwa Malkia wakati wa Mapinduzi ya Ufaransa miaka mia mbili iliyopita. Watu wenye njaa walipoandamana kwenda Ikulu kuomba mkate, akasema,"Hao watu kama hawana mkate, kwanini hawali keki?" Anashindwa kuelewa watu ambao hawana mkate hawawezi kupata keki.

Ndio hapa, watu wanadhania watakuwa na maridhiano ghafla. Maneno matamu yanazunguzuzwa lakini ishara zote zinaonyesha kwamba yale mambo yote ya Awamu ya Tano yataonekana kama tu michezo ya watoto wadogo.

Mtafute Mungu wakati anapoweza kupatikana. Mungu hakuumba ulimwengu huu ili acheze. Angetaka kucheza angefanya jambo jengine
"Seek The Lord while He may be found."imeandikwa sehemu fulani katika Biblia.
 
Ujumbe wako haujanyooka mkuu, kuna mahali umejing'ata mkia
 
Wewe ni Ganesh?
Unaendeleaje kwa Sasa?
Ulipotea muda mrefu sana ikiwa wewe ndie
Ile verified I'd yako umeamua kuachana nayo?
Poleni sana na msiba wa binti wa mdogo wako.
 
Back
Top Bottom