Mtabiri: Msichana ambaye hajaolewa asitoke nje sept 1

Mtabiri: Msichana ambaye hajaolewa asitoke nje sept 1

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,719
Reaction score
21,950
Ni mkosi mkubwa sana kwa msichana ambaye hajaolewa kushuhudia kupatwa kwa jua, elimu ya nyota inabainisha waziwazi kwamba kupata kwa jua ni tendo linaloendana na mwezi kupita kati ya dunia na jua,na hivyo mwezi kutambulika kama nyota mahaabat fitna, jua katika elimu ya nyota inajulikana kama shams na huwa inafananishwa na mwanaume wakati dunia ikijulikana kama najma ard ambapo hufananishwa na mwanamke.

Kuangalia kupatwa kwa mwezi ni sawa na kukaribisha mahaabat fitna katika penzi lako na hivyo kukaribisha migogoro ndani ya penzi,kwa wanawake ambao hawajaolewa kufanya hivyo ni sawa na hali inayojulikana kama
iighlaq al'abwab khayif hatta almawt katika elimu ya nyota, ambayo kwa lugha rahisi ni wanaume wote kukuona unatisha kama jini mauti.
Dada zangu ni wakati sasa wakuchagua unataka nini hasa?

Source :Ustaadhi Jumaa
 
Sio kila kitu tutasikiliza kisa elimu ya nyota, acha na wao waone. Hatuwezi kumuona mwanamke kama shetani
 
NASIKIA WEWE NDIO MWANZILISHI WA SINGELI HAPA BONGO....
NI KWELI???

[HASHTAG]#Chief[/HASHTAG] Eng
 
Hivi hadi leo kwenye karne ya 21 kuna watu bado wanaimani na hizi fikra taka?....kwahiyo wajifungie ndani wakihofia kutokuolewa badala ya kwenda kazini?....Hakuna kitu kama hicho!
 
Wanaofanya kazi wasiende wala chuo kisa ma mahaabat fitna, mmmmh sasa wale wadogo zangu wa kisafa na kinyakyusa ndo basi tena.
 
Sasa Kama Ni Askari JWTz Asifanye Usafi. Unataka Aadhibiwe. Adhabu Za Kijeshi Unazijua Mkuu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom