Mtaalamu wa mifugo (Dr. by Veterinarian): Karibuni kwa ushauri, tiba na dawa za mifugo tu

Ngombe wangu anashindwa kusimama, amezaa sasa ni miezi miwili. nifanyeje na hii ni siku ya 5 ameshindwa kusimama. Nisaidie please
upload_2017-8-31_7-58-23.png
upload_2017-8-31_7-58-53.png
upload_2017-8-31_7-57-52.png
 
Nashukuru sana kuja hapa. Kuna mengi mambo yanayohusu Mifugo na Wanyama ndani ya Tanzania.naomba darasa hili liwe endelevu Kwa manufaa ya wote.je nini tatizo Kwa mbuzi kutembea na kutingisha shingo.Ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
kama mbuzi wako anakula vizuri na anakuzalia na kukupa maziwa then huyo hana tatizo.... na kuhusu mbuzi kutembea huku akitikisa kichwa genetically wako hivyo mkuuu labda tuseme ni kama wewe binadamu unavyotembea huku ukirusha mikono mbele na nyuma hope nitakuwa nimekujibu swali lako mkuu
 
Aisee mkuu kuna ng'ombe wangu wawili nimewapoteza kila mmoja alipojifungua mtoto anakufa na mama baada ya siku kaa tano anakufa ningependa kujua tatizo,pia ng'ombe wangu mwingine alikula placenta nauliza madhara yapo?
Pia Kuku wangu inafikia mda hawawezi kusimama miguu yao inatetemeka na mwingine anashindwa kujisaidia! Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
kuhusu hilo la kwanza... kuna condition mbalimbali ambazo zinaweza pelekea hilo tatizo la kupelekea kufa kwa mama na ndama wake so kwa sasa siwezi kuwa specific ni kitu gani kilichopelekea hilo tatizo mpaka labda ningeweza pata sampuli i could state the cause mkuu

kuhusu hilo la pili.... hakuna effect yoyote mkuu.....

kuhusu hilo swali la tatu.... kuku wako wanaweza kuwa na ukosefu wa vitamini ambayo hupelekea kuku wako kushindwa kusimama vyema yaani " rubber legs" na treatment yake ni kuwapa vitamini iliyochanganywa na calcium plus phosphorus
 
kuhusu hilo la kwanza... kuna condition mbalimbali ambazo zinaweza pelekea hilo tatizo la kupelekea kufa kwa mama na ndama wake so kwa sasa siwezi kuwa specific ni kitu gani kilichopelekea hilo tatizo mpaka labda ningeweza pata sampuli i could state the cause mkuu

kuhusu hilo la pili.... hakuna effect yoyote mkuu.....

kuhusu hilo swali la tatu.... kuku wako wanaweza kuwa na ukosefu wa vitamini ambayo hupelekea kuku wako kushindwa kusimama vyema yaani " rubber legs" na treatment yake ni kuwapa vitamini iliyochanganywa na calcium plus phosphorus
Asante mkuu! Hiyo ya kushindwa kujisaidia kwa kuku wangu vipi naona kama hujanijibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
lipi hilo mkuu??

Mkuu Dr. tunashukuru kwa utayari wako wa kutaka kutusaidia. Sorry, nina ng'ombe dume mzuri chotara ambaye nia yangu ilikuwa kumtumia kwa mbegu ili kuendeleza mbegu lakini cha ajabu dume huyu mzuri hataki kuwapanda majike kutwa kucha ana attempt kuwapanda madume wenzie.

Hii hali kitaalamu huwa inatokea? Sababu yake ni nini? Na dawa yake ni nini? Hili hapa mkuu imebidi nilicopy.
 
mkuu kwa maelezo yako hapo juu.... ng'ombe wako ana ugonjwa unaoitwa downer's syndrome ambao ni ugonjwa pacha wa milk fever ambao husababishwa na upungufu wa madini ya calcium katika damu hivyo kupelekea ulegevu wa misuli na hivyo kupelekea ng'ombe kukaa chini kwa muda mrefu bila kunyanyuka

treatment yake inakuwa inasumbua tofouti na milk fever ambayo hutibika kirahisi embu fanya yafuatayo;
  • Mchome Calicium borogluconate kwa kiasi cha 800-1000ml nusu mwekee IV (mshipa wa damu jugular vein) na nusu nyingine mweke subcutaneous (chini ya ngozi)
  • Jaribu kumpa maji yaliyochanganywa na glucose
  • afu jitahidi sana kumnyanyua kama sehemu ya mazoezi ili aanze kuzoea kusimama tena
Asante sana, Nifanye kwa siku ngapi Dr.
 
Mkuu nipo huku kijiji mzee wangu ni mfugani lakini pale mvua zinapooanza kunyeesha ng'ombe wengi hasa wenye umri mkibwa huanza kuharisha na kukonda ghafla na wakati mwingine wakiwa marishoni anaweza akalala na kushindwa kuamka naomba ushauri mkuu nimsaidie mzee wangu

na kawaida kwa kipindi kama hicho hipoteza ng'ombe si 60 kwa mwaka kwa kipindi cha masika na vuli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Dr. tunashukuru kwa utayari wako wa kutaka kutusaidia. Sorry, nina ng'ombe dume mzuri chotara ambaye nia yangu ilikuwa kumtumia kwa mbegu ili kuendeleza mbegu lakini cha ajabu dume huyu mzuri hataki kuwapanda majike kutwa kucha ana attempt kuwapanda madume wenzie. Hii hali kitaalamu huwa inatokea? Sababu yake ni nini? Na dawa yake ni nini? Hili hapa mkuu imebidi nilicopy.
dume ana umri gani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom